kagwima
JF-Expert Member
- Jun 6, 2016
- 1,310
- 1,672
Mchezo wa Jana dhidi ya Burnley tulicheza vizuri mno hadi Granit Xchaka alipopata kadi nyekundu kwa kushindwa kujizuia hasira zake dhidi ya mchezaji wa Burnley.
Binafsi naamani timu yetu haitashuka daraja na wala haitatokea Arsenal kushuka daraja, sisi ni wajuu. Hakuna wa kutushusha chini, hiki tunachopitia ni kipindi cha mpito ambacho hakina muda mrefu tutakivuka.
Hawa ambao wanatabiri eti Arsenal mwaka huu inashuka daraja, wanaota ndoto ya mchana. Tumecheza almost mechi 12, bado tuna mechi zaidi ya 26.
Tuna nafasi ya kumaliza top 4 mwaka huu iwapo tutafanyia kazi mapungufu madogo yaliyopo. Bado tunakikosi kizuri zaidi ya timu ya Man utd, Chelsea, pamoja na Spurs waliopo juu yetu.
Tuendelee kuisupport timu yetu.
Forever Gunners![]()





acha kutufurahisha Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app





