Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Nyie ndo munataka mcheze UEFA mnashindwa kuipiga liverpool na mko kamili..hahaha
Sisi tulipigwa tulikuwa pungufu..
Japo wote tumepigwa ila nyie ni matakataka ya kudumu.😂😂😂😂
 
Adjustments.jpg
 
Tumepigwa ili tusajili wachezaji wapya. Wachezaji wetu wengi jana walitepeta haswa.
Sasa ni muda wa kuleta wale quality players.
Hatuwezi kushinda ligi kama tunategemea adui yetu atachezaje halafu na sisi ndo tumkabili.
 
Mkuu japo sikufanikiwa kucheki game yote ila nimejitahidi kupitia highlights kwa kiasi kikubwa kupata insight ya what happened na hii ndiyo observation yangu.

Liverpool were better in all aspects, if we are to compete in the same level atleast to start with tunawahitaji both Partey na Aouar.

Japo bado wenzetu wako ahead of us, project yao inaelekea mwaka wa tano na wamekuwa wakisajili kwa usahihi na kuboresha viwango vya wachezaji wao almost kila season.

Defensively:
Arsenal were much exposed due to lack of balance in the midfield. Xhaka anapokutana na runs za kutosha kama jana inampa ugumu sana na sio yeye tu bali midfielder yoyote atakayepewa defensive role huku anatumia left foot.

Tazama ligi zote kubwa Ulaya utakuta ni midfielders nadhani wawili tu (Xhaka na Fred wa Utd) wanaotumia miguu ya kushoto ndio wanacheza kama defensive midfielders, kwa asili mguu wao wa kulia ni very weak kuliko mguu wa kushoto wa player anayetumia mguu wa kulia.

Midfield:
Tumekuwa na almost one way ya kuattack kama mtakumbuka yale magoli ya Auba yanayofanana kila kitu jambo linalofanya tunakuwa very predictable.

Japo huwa tunatumia wing backs kushambulia lakini kwa jana huwezi panda kizembe against Liverpool's Mane na Mo Salah, kwa hiyo tulibaki na option moja.

Utaona jana wamemdhibiti Auba kirahisi ikamfanya Lacca apate nafasi kadhaa ambazo naye hakuwa makini kuzitumia.

Pia sababu wamejua tuna attack kwa long balls tukitegemea speed ya strikers wetu especially Auba, wamecheza offside tricks za kutosha na walifanikiwa sana (5 offsides).

Elneny ameonesha ni mtu muhimu sana pale kati na alijitahidi kufanya kazi yake vema, akicheza mtu kama Partey watatengeneza very solid midfield.

Attacking:
Sina shaka tuna strickers wazuri japo jana Willian hakucheza vizuri na pia Pepe(kama kawaida yake). Bado strikers wetu hawawezi kufanya vema sana kama midfielders hawako vizuri.

Matatizo yetu mengi jana yametokana na midfield kushindwa kulink na strikers wakati wa kushambulia na pia kushindwa kutoa cover kwa defenders especially kushindwa kuwapress vizuri wapinzani na kuwapa nafasi ya kutushamulia kwa moves toka nyuma.

Hatuna cha kujilaumu, tumefungwa na timu bora na wametusaidia kuona gap lililopo kati yetu na wao. Japo sikutegemea tungekuwa exposed kiasi hicho, nilitarajia atleast point moja pale Anfield.

Bravo Liverpool!!

Castr
DullyJr
Aaron Arsenal
Will jr
computerarsenal
14Henry
Relief Mirzska
gspain

Ndugu zanguni hii mechi kweli tumefungwa lakini maisha lazima yaendelee,katika ujengaji wa timu ajali Kama hizi lazima zitokee,

Bila shaka arteta atakua amejifunza sth juu ya style yetu ya kufanya 'build up' dhidi ya time zinazofanya press Kama Liverpool,

Laccazzette! Laccazzette! Dah!! Sijui Jana aliwaambia nini wenzake!,double open chances afu katika mechi Kama Ile hauwezi ukakosa kipuuzi vile,

Anyway let's look to another fixture.
 
Roma haikujengwa kwa siku moja.....
Arsenal ina wachezaji wengi wa kiwango cha daraja namba mbili huku liverpool wanawachezaji wengi wa kiwango cha daraja la kwanza.

Ila ni suala la muda tu.

"Samaki mdogo ipo siku atakuwa mkubwa"

Liverpool pongezi kwao walicheza vizuri
 
hamna sehemu nilisema hii game tunashinda. Ila nilisema naprefer point kutoka katika meetings zetu na hawa jamaa. Arteta alikua wazi tangu day one alisema "tuna misimu 3 kabla ya kua na timu ya kugombea ligi"

Souness akasema "Arsenal haionyeshi kama ni mshindani wa ligi labda short term tournament" kuna jamaa aliandika humu kua msimu huu ligi yetu nikamjibu "Arsenal haina mpango na ubingwa" so kama kuna mtu anadhani eti hii loss ni pigo kwa Arsenal au bodi anajidanganya, labda mashabiki kwakua tunataka kutambiana lakini kocha na kikosi wao wanajifunza.

kuna plastic fan mmoja wa chelsea (hata kumtaja naona uvivu) kamuambia plastic mwenzie kwamba tunakutana na liva Alhamisi halafu mwenzake akajibu "Liva hayupo serious na Carabao ndiyo maana anachezesha kikosi cha pili"

Game na Leicester Arsenal tulianzisha regular starters wa first XI watatu tu. liva akicheza na ile timu ambayo najua mshaisahau jina alinzisha watano akiwemo Van Dijk sisi Gabriel ambaye definitely alihitaji game time alikua benchi. Auba, Ceballos, Guendouz, Ozil, Tierney hata kwenye benchi hawakuwepo.

dzinga
 
Hivi bado kuna mtu ana shaka na Elneny? Xhaka alikua utumbo ikabidi ale bench. Pengine he had too much birthday sex si kwa komedi ile.

diogo jota kapelekewa mpira hakufikiria mara mbili akashuti. angalia wachezaji wetu walivyokua wanajivuta something I said hatukutakiwa kuacha kufanya. jota kapata chansi 3.

ya kwanza one vs one kazingua.

ya pili one vs one salah akanyang'anya mpira.

ya tatu katikati ya mabeki akascore.

Halafu kuna Lacazette...
 
Hivi bado kuna mtu ana shaka na Elneny? Xhaka alikua utumbo ikabidi ale bench. Pengine he had too much birthday sex si kwa komedi ile.

diogo jota kapelekewa mpira hakufikiria mara mbili akashuti. angalia wachezaji wetu walivyokua wanajivuta something I said hatukutakiwa kuacha kufanya. jota kapata chansi 3.

ya kwanza one vs one kazingua.

ya pili one vs one salah akanyang'anya mpira.

ya tatu katikati ya mabeki akascore.

Halafu kuna Lacazette...

Kaka relax, ebu angalia mpira kwa angle ingine (quality ya Opponent) na mpira wanaocheza na jinsi walivyoweka mkakati wa kutuzuia

High press, mane, bobbi, salah hawa walihakikisha hakuna Kupiga pasi kuanzia golini zenye madhara kwenda kiugo ya arsenal

mwishowe TUKAWA TUNABUTUA
 
UKIBUTUA mbele mpira unashikwa na VVD au Fabinho, liverpool walihakikisha arsenal hapigi pasi walau nne mfululizo wawe wameunasa mpira

ilikuwa ni Total DOMINATION down the middle, high press yao sio ya kawaida, Lets BE HONEST

liverpool wako VIZURI
 
NIMEAMINI YULE MUHINDI WA BETTING ATAENDELEA KUMALIZA HELA ZA VIJANA KAMA HAWA...YAANI ULIAMINI KABISA UTAMFUNGA mane,firminho,salah UKIWA NA KINA elnany na kipepe?
Mbona unanifokea binti? Herufi kubwa za kazi gani? Huoni niliandika '.... tukienda suluhu ya bila bila half time...' au kusoma haujui?
 
kuna post niliandika humu juu ya default settings za liva kwenye PES 20 ya PS4. Kama huijui style ya kukaba ya Gegenpress sasa ndiyo ile ya jana.
 
Hata hivyo msijifanye mmesahau huu ndiyo msimamo wa Ligi. Watafute majirani zetu Chelsea, Tottenham na wale wengine wale.
 

Attachments

  • CaptureJf.JPG
    CaptureJf.JPG
    53.5 KB · Views: 6
Back
Top Bottom