Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,484
- 4,824
Nawatakia wadau wote wa soka Christmas njema na mwaka 2011 wenye mafanikio.
Wazee wote wa darajani Stamford, Rev Masa, EL NINO, Rev Kishoka, Sanda Matuta, Ab-Titchaz, AljuniorTz na Invisible, bila kusahau wakongwe wa Old Trafford, Manda, Belo, Eqlypz, Idimi na Ngongo, pia washika bunduki wa Emirates, Arsene Wenger, Mbu, Kweli, Wacha1, Balantanda, Baba Mkubwa, Genekai, Questt, Bubu Ataka Kusema na Ng'wanza Madaso,....mzee Shedafa wa WHL na Acid wa Anfield na wengine wote ambao sikuweza kuwakumbuka kwenye post hii, I wish you and your loved ones a Merry Christmas and Happy New Year.
Asante sana jirani......Nami niungane nawe kuwatakia Heri ya Krismas na Mwaka Mpya wadau wote wa jukwaa hili Pendwa hapa jamvini,Kila la heri na mafanikio kwa vilabu vyenu kwa mwaka 2011
Merry Christmas wakuu wote na familia zenu,Mungu awalinde wakati huu wakusheherekea sikukuu zote.Merry Xmas and Happy New Year 2011 wapenzi na mashabiki wote wa Arsenal😛arty:. Inshaaalah mwaka 2011,uwe wa mafanikio kwetu sote! Walau tunyakue kikombe hata kimoja.Merry Christmas & Happy New Year kwa wadau wote wa Emirates...
...Thanks very much wadau wote, kila la heri kwenu nyote na familia!
Pamoja, kama kawaida!
Robbie Van Persie :teeth: Belated Christmas wishes and prosperous new year to all! Tunamalizia mwaka kwa kuanzia na kuwachapa Chelsea,Didier Drogba
Robbie Van Persie :teeth: Belated Christmas wishes and prosperous new year to all! Tunamalizia mwaka kwa kuanzia na kuwachapa Chelsea,
Tunawaombea kwa Mungu
Arsenal leo ni lazima ishinde.
Ili kuweka matarajio yetu hai leo ikiwa tupo nyuma kwa 5 points na Man United wana kiporo cha mechi moja na Blackpool, Arsenal haina budi kushinda mechi hii muhimu kwani ndio utakuwa mwanzo wa msimu wa Arsenal baada ya kungojea kombe hilo kwa miaka inaenda sita sasa.
Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti leo ataiagiza timu yake icheze mchezo wa kujilinda na kuziba maeneo yote ya uzalishaji mashambulizi kutoka kwa Andrei Arshavin, Samir Nasri na Cesc Fabregas huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza kwa Arsenal wakimwacha Didier Drogba peke yake mbele. Ni mbinu nzuri ambayo Chelsea walitumia kwenye mechi yake ya kwanza na Arsenal pale uwanja wa Stamford Bridge na ilifanya kazi na Arsenal wakalazwa 3-0.
Mbinu hii ya kucheza kwa kujilinda huku mchezaji mmoja akiachwa peke yake mbele pia ilitumiwa na Jose Mourinho na timu yake ya Inter Milan dhidi ya Barcelona kwenye nusu fainali ya Champions League mapema mwaka huu na Inter ikashinda na kwenda kunyakua kombe hilo la Uefa Champions League. Inter walimwacha mbele Samuel E'to na Diego Milito akimsaidia na katikati nahodha wa Inter Javier Zanetti alikuwa akihakikisha back four yake haisumbuliwi.
Kama utakuwa na "well organised back four" hata timu nzuri kuliko zote haitaweza kuwafunga na Barcelona walifungwa na Inter Milan. Ni mbinu nzuri sana ambayo inatumiwa na timu zote zinazocheza na Arsenal na timu hizo huishia kuifunga Arsenal au kutoa sare. Tayari mwaka huu West Brom waliwafunga Arsenal tena kwao na baadae Newcastle na Man United mara mbili na Arsenal wakatoa sare na Sunderland na wote huwapa Arsenal uwezo wa kumiliki mipira kwa muda mrefu walingoja kupata nafasi walau moja au mbili na kutumia nafasi hizo kuwafunga Arsenal.
Leo baadae tunaelekea Emirates kushuhudia Arsenal ikicheza mchezo uleule na "free flowing" na hii inazifanya timu kama Chelsea zisiwe na wasiwasi sana. Mbinu ya "10 men behind the ball" inaisaidia Chelsea wanakuwa na mwelekeo mmoja wa mashambulizi huku wakiwachanganya mabeki, na pia wanakuwa wanapeleka mipira mingi ya juu kwa Didier Drogba na pembeni wanawatumia mabeki wanaokwenda mbele Ashley Cole na Branislav Ivanovic.
Kwahio matokeo yoyote yale yasio ushindi kwa Arsenal basi itakuwa ni mwisho wa ndoto ya kunyakuwa kombe la ubingwa baada ya miaka sita.
Tusikibiane kesho mkuu