UNAI EMERY ASIVYOTABILIKA NA KUWAPA MAKOCHA WAPINZANI SHIDA
Moja ya lawama kubwa alizopewa Wenger kipindi chote akiwa Arsenal kucheza style moja haijalishi anacheza na Fulham au Barcelona. Nimeiangalia Arsenal kwa miaka 22 lkn Arsenal ya 14 iliyopita ungebet kwamba ktk kila mechi kubwa lazima wafungwe goli la counter attack. Ungebeti pia kwamba magoli 10 watakayofungwa matano yatakuwa set pieces.
Kipindi cha Wenger ulikuwa huna haja ya kuuliza line up au sub gani itaingia. Ilifahamika kama baba yetu uliye mbinguni kwa wakristo. Nakumbuka rafiki yangu moja marehemu Jumbe alinishangaa kila mechi nikipatia lineup na sub mpaka dakika ya sub.
Unai mfumo na tactics hata wachezaji wenyewe wanajua siku moja kabla ya mechi. Lineup wachezaji wanaijua masaa mawili kabla ya mechi. Yeye anaamini kwamba mpira ni vita kama nyingine na kwamba jinsi mpizani wako anavyojua mbinu yako mapema ndivyo inavyokuwa rahisi kwake kukudhibiti.
Mfano mdogo alivyo wa surprise Tottenham...
Pochettino Unai atakuja na washambuliaji wawili Auba na Laca, kwa hiyo yeye akaja na back four. Unai akaja na mshambuliiaji moja naye hakwenda kusimama kama namba 9 bali kama force 9 na Iwobi, Miki na Ramsey wakipishana mbele yake.
Pochettino alipongundua ameingia chaka akafanya tactical switch na kucheza na wing backs. Unai akafanya counter sub ya Ozil na Auba na kuharibu kabisa na kama si makosa binafsi ya Mustafi, Auba na refa Arsenal wangeondoka na point 3.
Ni msimu wa kwanza na mabadliko makubwa anaendelea kuyafanya. Bado ninaamini top 4 inawezekana. Nadhani itakuwa zawadi kubwa kwake
Sent using
Jamii Forums mobile app