Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Ligi kuu ya England imeendelea hii leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbalimbali huko Emirates klabu ya Arsenal imeweza kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 4 – 1 bila mshambuliaji wake raia wa Chile Alexis Sanchez ambaye yupo mbioni kujiunga na Manchester United.

Wachezaji waliyokuwa mwiba katika mechi hiyo ni Monreal akiiyandikia The Gunners bao la mapema kabisa dakika ya 6 kabla ya Iwobi kutupia dakika ya 10, Koscielny na Lacazette kila mmoja akishindilia msumari wa moto kwa Crystal Palace na kuifanya timu hiyo kupoteana kabisa uwanjani.

Kwa matokeo hayo Arsenal anakuwa na pointi 42 ikishika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya England huku wakiwa wamecheza michezo 24.
 
Klabu ya Manchester United imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Alexis Sanchez kutokea Arsenal na kutarajiwa kufanyiwa vipimo jioni ya leo katika viunga vya uwanja wa mazoezi wa United wa Carrington.

Dili ambalo pia linamuhusisha Henrikh Mkhitaryan ambaye tayari kila kitu kipo sawa na Sanchez tayari ameshaanza safari ya kwenda Kusini mwa jiji la Manchester kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya afya leo siku ya Jumamosi huku akitarajiwa kupokea mshahara wa paundi 450,000 kwa wiki.

Timu nzima ya watabibu wa United walikuwa na kikosi huko Turf Moor kwaajili ya mechi yao lakini wanampango wa kukutana na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile baada ya mchezo huo.

Ingawa mpaka sasa timu nzima iliyosimamia zoezi hilo haijazungumza chochote meneja wa kikosi hicho, Jose Mourinho akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wao dhidi ya Burnley amesema watu watarajie hivi karibuni ujio wa mchezaji huyo.

Watarajie hivi karibuni, kama hautofanikiwa basi hautokuwepo tena usajili huo, nafahamu watu wangu hufanya mambo kwa uhakika ninahakika watafanikiwa katika zoezi hili,” amesema Mourinho akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya Burnley.
 
Kwa matokeo haya ninavyomjua Wenger pengine asisajili tena dirisha hili
 
Naona dili la abemuyang linakufa taratibu wenger fala sana

Nilisema mwanzoni kabisa tatizo wanataka wachezaji kwa bei ya biscut ndio matokeo yake wamepeleka ofa ya kibwege Dortmund wamebidua meza ya majadiliano.... nimeona picha za Mikhi akiwa London ingawa sina uhakika na kama ni za kweli au wahuni washatengeneza.
 
FB_IMG_1516463778229.jpg
 
Nilisema mwanzoni kabisa tatizo wanataka wachezaji kwa bei ya biscut ndio matokeo yake wamepeleka ofa ya kibwege Dortmund wamebidua meza ya majadiliano.... nimeona picha za Mikhi akiwa London ingawa sina uhakika na kama ni za kweli au wahuni washatengeneza.
Mikhi hana ujanja, mkataba wake utafidiwa na Net Profit, ila Pierre-Emerick Aubameyang nina wasiwasi, Emirates wana tabia ya ku balance the books ile mbaya..Ila pressure ya Gooners labda itaweza kumleta..
 
Wachezaji wengine watanuna. Aombe Mungu apaform beyond expectations.....
 
Mshambuliaji kutoka Chile Alexis Sanchez amepigwa picha akiwa amevaa jezi ya Manchester United kwa mara ya kwanza huku akikaribia kuhamia Old Trafford kutoka Arsenal. (Metro)


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema uhamisho wa Sanchez kutoka Arsenal kwenda United ulichochewa na 'tamaa' ya fedha. (Telegraph)


Arsene Wenger amekiri kuwa wasiwasi kuhusu mustakabali wa Sanchez Arsenal uliteteresha morali ya timu nzima. (Guardian)
 
Back
Top Bottom