Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Everton imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot katika mkataba ulio na thamani ya £20m katika kandarasi ya miaka mitatu na nusu.
Walcott, 28, ni mchezaji wa pili kusajiliwa na mkufunzi wa Everton Sam Allardyce katika dirisha la uhamisho la Januari baada ya mshambuliaji Cenk Tosun aliyesajiliwa kwa dau la £27m kutoka Besiktas.
Hatua hiyo inakamilisha huduma za Walcot za miaka 12 katika klabu hiyo ambapo alifunga magoli 108 katika mechi 397
"Kuna kitu muhimu kuhusu uhamisho huu najihisi vyema sana'', alisema
Klabu ya zamani ya Walcott Southampton pia walikuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo.

Lakini Walcott, ambaye hajaanza mechi yoyote ya ligi ya Arsenal msimu huu anaamini kwamba Allardyce anaweza kuimarisha mchezo wake.
''Nilihisi kwamba ni wakati nilifaa kuondoka'', alisema.
Ni uchungu lakini ni vyema na nataka kuimarisha mchezo wangu na kuisaidia Everton kushinda mataji kama ilivyokuwa awali.
Aliongezea: Mkufunzi amekasirika lakini hiki ndicho nilichotaka.
''Nilizungumza naye na nilihisi hasira aliyokuwa nayo na kile alichotaka kutoka kwangu''.
Katika taarifa yake , Arsenal ilisema: Sote tunamshukuru Walcott kwa mchango wake kwa Arsenal na tunamtakia kila la kheri.
 
Mchezaji anayelengwa kusajiliwa na Arsenal katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari Malcom anakabiliwa na kesi ya utovu wa nidhamu katika klabu ya Bordeaux.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alionyeshwa katika mitandao ya kijamii akicheka na kufanya utani pamoja na wachezaji wenza Cafu na Otavio baada ya timu yao kushindwa na klabu ya Caen siku ya Jumanne.
Bordeaux waliomsajili mchezaji huyo wa Brazil kutoka Corinthians 2016 ilisema kuwa wachezaji hao walionyesha ukosefu wa ukomavu, umoja na heshima kwa taasisi hiyo.
Klabu hiyo ilisema kuwa inashutumu vikali kanda ya video na kwamba mashtaka ya kuwachukulia adhabu yataanzishwa.

Malcolm amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal kutoka Bordeaux ambapo amefunga magoli 18 katika mechi 80.
Hatahivyo makubaliano yoyote yataafikiwa iwapo mshambuliaji wa Gunners Theo Walcot atajiunga na Everton.
Arsenal pia inamtaka kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang na haiwezekani kwamba watawasajili wachezaji wote watatu.
 
After 12 years,all the best Theo on your new chapter and Alhamdullilah tumeweza ku-off-load angalau.
IMG_3333.jpg
 
Mkuu cha tatu ndo chenyewe sasa..welbeck hafai kuanza.. Ila kama Pierre atasajiliwa..,anatakiwa atafutiwe nafasi pale mbele...huyo ni mnyama magoli anafungia kiungo chochote kile,na popote pale..na defender mmoja wa nguvu anatakiwa aongezeke....
Hapo tutakuwa tumeua..

Mkuu hawa Mikh na Auba mmewatoa wapi tena au mna imani na bodi yetu yenye longolongo kibao...?
 
Mkuu hawa Mikh na Auba mmewatoa wapi tena au mna imani na bodi yetu yenye longolongo kibao...?
Mkuu mikhi tayari hiyo labda Pierre.. Nasikia tena mahrez cjui...
Sahivi naona wamekuwa serious kidogo akili ishaanza kuwaingia...
 
Kama wameoffload walcott na sanchez lazma wafanye jambo la maana kidogo,ukizingatia giroud nae haeleweki
 
Mkuu mikhi tayari hiyo labda Pierre.. Nasikia tena mahrez cjui...
Sahivi naona wamekuwa serious kidogo akili ishaanza kuwaingia...
Ishu ya Mikhi wanadai wakala wake kakaza mpaka sasa ila Auba ni chaguo sahihi tatizo wakitajiwa tu mpunga basi bodi inatoka nduki

Kama wameoffload walcott na sanchez lazma wafanye jambo la maana kidogo,ukizingatia giroud nae haeleweki
Natamani kuona Sanchez anasepa hata sasa ivi sijui kwa nini deal yake inachelewa ivi,bado kazi ya ku-offload haijaisha mzee naamini wapo wengi hawastahili kuvaa jezi ya Arsenal naungana na Henry kua wachezaji wetu wengi ile jezi kwao ni nzito.
 
Ishu ya Mikhi wanadai wakala wake kakaza mpaka sasa ila Auba ni chaguo sahihi tatizo wakitajiwa tu mpunga basi bodi inatoka nduki

Natamani kuona Sanchez anasepa hata sasa ivi sijui kwa nini deal yake inachelewa ivi,bado kazi ya ku-offload haijaisha mzee naamini wapi wengi hawastahili kuvaa jezi ya Arsenal naungana na Henry kua wachezaji wetu wengi ile kezi kwao ni nzito.
Exactly kabisa mkuu...,kuna wachezaji utoto bado mwingi..
Huyo Sanchez ni kheri aende tu anApoenda ili tupate fursa ya kuleta majembe mengine...
Sababu ya huyo raiola kugoma ni IPI????
 
Tatizo ni Wenger.
Tatizo ni Kroenke Wenger hana tatizo, washabiki wengi wa Arsenal wanadhani wenger ndiye asiyetaka kuwanunua kina ronaldo na griesman, yenye timu inabania hela ya usajili, kuuza timu haitaki, Wenger ameifanya club iwe kubwa kila mtu anaifuatilia. Mbona madrid yenye ma star chekwa hata uropa mwakani wataisikia redioni. Wenger in.
 
Ishu ya Mikhi wanadai wakala wake kakaza mpaka sasa ila Auba ni chaguo sahihi tatizo wakitajiwa tu mpunga basi bodi inatoka nduki

Natamani kuona Sanchez anasepa hata sasa ivi sijui kwa nini deal yake inachelewa ivi,bado kazi ya ku-offload haijaisha mzee naamini wapi wengi hawastahili kuvaa jezi ya Arsenal naungana na Henry kua wachezaji wetu wengi ile kezi kwao ni nzito.
Wale kina iwobi,chambers,maitland niles,per, n.k ni wachezaji wa kalabao.....
 
Back
Top Bottom