Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tetesi
ARSENAL YAPIGANA VIKUMBO NA UNITED KUMSAJILI RUGANI

Arsenal wameingia kwenye mbio za kumsajili beki wa Juventus Daniele Rugani, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United, the Sun limeripoti.
 
Sanchez hakuna namna ya kumzuia kuondoka,na hizi mbilinge zake ni bora angesepa tu hata januari naona mjadala wake unaigawa tu timu.
Kweli kabisa mkuu..
Ila ningependa kujuwa mawazo yako kuhusu Ozil, maana mshenzi mpira anaopiga sasa si mchezo...
 
Kweli kabisa mkuu..
Ila ningependa kujuwa mawazo yako kuhusu Ozil, maana mshenzi mpira anaopiga sasa si mchezo...

Ozil ni lazima AW apambane kumbakiza hakuna namna tunamhitaji sana yule muarabu na kwa perfomance yake ya sasa anazidi kutufanya tumtegemee ila jamaa bado anaonyesha anahitaji kubaki maana mpaka sasa ameruhusu mazungumzo kuendelea.
 
Yeah, its now or never
 
Kweli kabisa...
 
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa haogopi kumpoteza Alexis Sanchez mnamo mwezi Januari licha ya mshambuliaji huyo kuifungia Arsenal mabao mawili dhidi ya Crystal Palace.
Baada ya Andros Townsend kusawazisha bao lililofungwa na Shkrodan Mustafi katika kipindi cha kwanza , Sanchez alifunga mabao mawili.

Mshambuliaji huyo wa Chile alificha mkwaju mkali karibu na mwamba wa goli na kufanya mambo kuwa 2-1 kabla ya kuongeza bao la pili kupitia pasi nzuri iliopigwa na kiungo wa kati Jack Wilshere.
James Tomkins alifungia Palace bao la pili katika dakika za lala salama lakini mabao hayo ya Sanchez yalitosha kuipatia ushindi Arsenal ambayo sasa iko katika nafasi ya sita katika jedwali la ligi ikiwa sawa kwa pointi na Tottenham ambao wako katika nafasi ya tano na pointi moja nyuma ya Liverpool iliopo katika nafasi ya nne.

Kandarasi ya Sanchez inakamilika mwishoni mwa msimu huu na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amehusishwa na uhamisho kwa viongozi wa ligi Manchester City ambao walishindwa kumsajili katika dirisha la uhamisho lililopita.
''Siogopi, lakini hilo kitakuwa swala la baadaye kutokana na hali ya kandarasi yake'', alisema Wenger, ambaye alifikisha idadi ya mechi 810 alizosimamia katika ligi ya Uingereza sawa na aliyekuwa mufunzi wa Manchester United Sir Alex Furguson.
 
Tetesi
Arsenal inajiandaa kumnunua winga wa Algeria na Leicester Riyad Mahrez, 26, huku mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo (Le Buteur - in French)
 
Tetesi
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa mazungumzo ya kuandikisha kandarsi mpya ya kiungo wa kati Jack Wilshere, 25, yamepangiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Januari. (Mail)
 
Most valuable clubs do mundo (via Forbes): 2017

1 - Manchester United £2.7b/$3.7b
2 - Barcelona £2.6b
3 - Real Madrid £2.6b
4 - Bayern de Munique £2.0b
5 - Manchester City £1.5b
6 - Arsenal £1.4b
7 - Chelsea £1.3b
8 - Liverpool £1.1b
9 - Juventus £930m
10 - Tottenham £780m
 
Tetesi
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anajiandaa kumnunua winga wa Ivory Coast na Crystal Palace Zaha ili kuchukua mahala pake mshambulijai wa Chile Alexis Sanchez, 29. (Daily Star)
 
Tetesi
Wachezaji kadhaa wa Arsenal walidaiwa kumshutumu mshambuliaji Alexi Sanchez kwa kuwa na tabia mbaya baada ya mechi dhidi ya Burnley mwezi Novemba. (Guardian)
 
BIFU zito linatokota katika kikosi cha Arsenal kati ya Alexis Sanchez na baadhi ya wachezaji wenzake, ambao wanataka aondoke klabuni hapo.

Ugomvi kati ya Sanchez na wenzake ulianza kwenye mechi dhidi ya Southampton, mwanzoni mwa mwezi huu.

Katika mchezo huo, ambao Arsenal ilitoka sare ya 1-1 inasemekana nyota wenzake hawakufurahishwa na kiwango cha Sanchez na hasa alivyokuwa anapoteza mipira mara kwa mara.

Nyota aliyejitolea kumpa makavu Sanchez alikuwa Jack Wilshere, ambaye alimlaumu kwa kucheza ovyo.

Sanchez inadaiwa amekuwa na uhusiano mbovu na nyota wenzake, ambao wanatamani aondoke Januari hii.

Kali ya yote ilikuwa Alhamisi iliyopita wakati baadhi ya mastaa wa Arsenal walipogoma kwenda kushangilia na Sanchez alipofunga kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace, ambayo Arsenal ilishinda mabao 3-2.

Wenger alikwepa kuzungumzia suala hilo alipoulizwa na waandishi wa habari.

“Sikuona kwa kweli kilichotokea baina ya wachezaji wangu,” alisema Wenger, ambaye timu yake inakabiliana na West Bromwich leo.

Mtu mmoja ndani ya klabu hiyo alidai kuwa Sanchez ni mkorofi na ni ngumu kuishi naye.

Wenger inasemekana ameingiwa na wasiwasi kuwa chuki dhidi ya Sanchez inaweza kuyumbisha timu hiyo.

Kuna taarifa kuwa anaweza kumuuza kwenye dirisha dogo ingawa Sanchez anataka amalize msimu ili aondoke bure na kujiunga na Manchester City
 
Line up
5c803beb0556a4cd241017721b3e317a.jpg

Muarabu (Ozil) majeruhi.
 
Hoax.....!
Media za UK kama kawaida yao wanataka kutengeneza habari,ni sawa Sanchez hataki kubaki Arsenal ila sio kila tukio watafute namna ya kuigawa Arsenal na hawajaanza leo.
dfd6fde3b74537f9896b2fdb0d1de65e.jpg

Napita tu
 
Back
Top Bottom