Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tunashukuru kwa taarfa njema, Wenger akaze maana ligi ya mcm huu ngum sana
 
1472206385355.jpg
pale unapogundua mzee wenger anamleta Mustafi na perez full ma confidence
 
Richard, unapata wapi habari za ndani za club ya arsenal??

Mkuu, mimi nipo around Scouting system hiyo imenisaidia sana kupata ujuzi na pia kuwapatia kidogo nyie wakuu hapa JF.

Pili, mimi ni mwanachama wa Arsenal, hivyo nnayo access ya AST au Arsenal Suppoters Trust ambao nao huwa na info fulani za mambo yanaojiri around the club.

Habari niiletayo humu huwa inakuwa imekamilika ila media kwa kuwa hazina uhakika zaidi ndiyo huifanya habari ya usajili kama ndiyo habari yenyewe ili kuuza gazeti.

Chkodran Mustafi alikuwa ndio target ya Arsenal kwa sehemu ya ulinzi lakini Valencia walikuwa wanasumbua kwenye ada, lakini hilo lilipata break-through jana jioni.

Perez nae baada ya kusikia Arsenal wameingia kwenye biding system maana Everton ndiyo walikuwa wa kwanza, basi akasema anataka timu inayocheza Champions League.

Hivyo biashara imekwisha na tunasubiri gale lijalo.
 
Poa tu mkuu mimi nipo natathmini msimu wa timu yetu safari hii.

Ya, msimu wa 2015/2016 kwenye La Liga Perez alifunga magoli 17.

Huyu ndie mshambuliaji pekee wa Depor lakini wamemwachia tu kwa sababu ya kifedha.

Ila kwa kuwa Everton na timu zingine zilikuwa zikifukuzia, maskauti wa Arsenal nao walikuwa wakiwinda kwa mbali.

Ndio leo wakaamua ku-move for a kill walipoona Everton wanasita kwenda zaidi ya 17M, hivyo kwa kiasi Fulani hii ni bargain kuzingatia umri wake.

Kwa kuwa Giroud yupo, Walcott na baadae Welbeck akipona, angalau Wenger atakuwa na options na pia Perez ataleta copetition baina yao.

Hivyo is fair to say ni good move ingawa sio ya zaidi ya 30M au 40M

Wenger anatufundisha economics yaani unakaa mpaka mwisho wa mnada, lol
Huyu mzee kashatuchosha bora asepe tu. Furaha yetu sisi ni ushindi na hatuwezi shinda kwa kuwa na kikosi kibovu
 
Usajili Updates: Perez afanyiwa medical na imekuwa OK.

Lucas-perez-1.jpg


Mshambuliaji Lucas Perez Martinez jioni hii amefanyiwa medical na kufaulu utaratibu huo hivyo kuelekea kukamilisha taratibu zote za uhamisho kutoka Deportivp La Coruna.

Perez amegharimu kiasi cha paundi milioni 17 pamoja na ads on kama ufanisi uwanjani na matangazo ambapo kiasi kamili kinafikia kuwa pauni milioni 20.

Chkodran Mustafi nae hadi jioni hii alikuwa akifanyiwa medical hiyo ambayo hufanywa kwenye uwanja wa mazoezi wa Arsenal wa London Colney.


Valencia-CF-Vs-AC-Fiorentina-Pre-Season-Friendly.jpg


Mustafi anatarajiwa kugharimu kiasi cha pauni za uingereza milioni 35.

Arsenal ilitenga kiasi cha pauni milioni 100 kwa ajili ya usajili wa msimu wa 2016/2017 na walikuwa wameweka kipaumbele kwa sehemu ya kiungo, ulinzi na ushambuliaji hivyo hadi sasa kuwa wamekamilisha suala hilo kwa asilimia 100.

Hata hivyo Arsenal ilisajili wachezaji wengine ambao ni Takuma Asano ambae sasa atachezea timu ya Stutgart ya Ujerumani kwa mkopo.

Rob Holding imebidi asaidie kwenye kikosi cha kwanza hivyo kuwa ni miongoni mwa mabeki wa kuaminika kwa sasa.

Mchezaji mwingine aliesajiliwa na Arsenal ni Kelechi Nwakali kutoka Nigeria ambako ni nahodha wa timu ya vijana chini ya miaka 17.

Joel Campbell amepelekwa Sporting Lisbon kwa mkopo na Arsenal watakuwa wakilipa gharama zake.

Hivyo tusubiri mechi ya jumamosi kati ya Arsenal na Watford itakayofanyika uwanja wa Watford ulipo barabara ya Vicarage jijini London.

COYGs!
 
Richar

Jana ulisema Mustaf chaguo la tatu sasa imekuaje?

Tena siyo chaguo la tatu pekee bali kulikuwa na mabeki wanne ambao wengine niliwataja jana wengine ni Costas Manolas, Mateo Musacchio na Omer Toprak beki mshahara wa Bayern Leverkusen.

Kufikia mchana wakachujwa na kubakia Toprak na Mustafi na Leverkusen wakasema wanataka 40M in full!

Ndipo simu zikapigwa kati ya London, Germany na Valencia na Arsenal wakasema hawatalipa hizo 40M kwa Toprak na wakati huohuo Mustafi akasema anataka kwenda Arsenal kwa ushauri wa Ozil na Mertasacker ambao ni wajerumani wenzie.

Ikaamuliwa liwalo na liwe maana Mustafi bado ni majeruhi tangu kwenye Euro 2016 na Arsenal wakaamua kulipa 35M short ya 5M kama wangeenda nje ya bajeti yao ya 100M, kama wangeenda kwa Toprak.

509328930.jpg

Omer Toprak ndie beki mshahara wa kutisha kwenye Bundesliga kwa sasa na anagharimu pauni milioni 40.

Ila ukiangalia sana utaona kwamba Mustafi anakuja kuwa beki msaidizi mpaka Gabby na Mertasacker watakapopona na kwa kuwa tayari Rob Holding yupo, basi timu itakayocheza na Watford jumamosi itakuwa na mabeki walewale walocheza na Leicester
 
Back
Top Bottom