Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,649
- 25,648
Wakati mwingine ni vema kutoa hoja bila ushabiki wowote ule. Hii inapendeza sn! Lkn km MTU anaamua kutoa tu maoni kiushabiki na kwa mapenzi Yake haipendezi!
Ntajibu hoja yako kwa kukutolea mfano wa Ryan Bertrand.
Huyu Bertrand alichukuliwa na Chelsea mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 16 umri tosha kabisa kuanza kuendelezwa kimpira. Hio ni sawa na Arsenal walipomchukua Cesc Fabregas kutoka Barcelona akiwa na umri huohuo wa miaka 16.
Kati ya mwaka 2005 na 2010 Chelsea walimtoa Bertrand na kumpeleka kwenye timu mbalimbali eti kuendeleza mpira wake wakati ilitakiwa aendelee kumsoma (understudy) Ashley Cole ambae Chelsea ndio waliuwa wametoka kumnunua kutoka Arsenal wakti huo ili Ashley kama hayupo basi Bertrand anakuwa anaingia kucheza.
Lakni hata kwenye Carling Cup Bertrand hakuweza kuchezea Chelsea hadi mwaka 2011 (baada ya miaka 6), sasa Fabregas yupo timu kubwa ya Chelsea na anachezea timu ya nchi yake ya Spain na Bertrand bado yupo katika timu ya Southampton na hapati namba kwenye timu ya England.
Unapomtoa mchezaj kwenda timu ingine kwa mkopo ili apate uzoefu inatakiwa iszidi miaka miwili na nadio maana Jack Wilshere alikwenda Bolton kwa msimu mmoja na wengine wengi tu walipelekwa kwenye timu zingine lakin hawajazidisha miaka miwili.
Wale wachezaji ambao wanakuwa walionyesha vipaji hasa kama Fabregas ambae alizna kucheza mechi kubwa baada ya Vieira, Edu na Gilberto Silva kuumia mwaka 2004.
Huu si ushabiki mkuu ni facts tu, halafu mimi sio shabiki tu ni mtaalam khasa wa haya masuala ya uchambuzi hasa mpira.