Wana GUNNERS tuna vigongo vya mechi kuanzia January 27th ambazo ama zitaendelea kutufanya tuendelee kuwemo katika timu zinazowania ubingwa wa EPL 2010 au ndiyo ndoto zetu kupotea. Tutakuwa ugenini na Aston Villa Jumatano ya tarehe 27/01, tutakuwa nyumbani na MANU J'pili ya taehe 31/01, J'pili ya 6/02 tutakuwa ugenini na Chelsea na J'tano ya 10/02 tutakuwa nyumbani ya L'pool. Katika hizi wiki mbili za mechi hizi kama tukiweza kujikusanyia points kati ya nane na kuendelea basi kwa maoni yangu tutakuwa katika nafasi nzuri sana na pia kushinda zile mechi ambazo tunastahili kushinda kati ya sasa na mpaka kipindi hicho cha wiki mbili za vigongo vya mechi.