Wakuu wenzangu wa Gunners mpoo!
Kesho tunaingia Old Traford tukiwa na lengo moja tu kupata 3 points na kutimiza malengo ya kucheza vizuri kwenye mwezi huu wa November.
November kwa kawaida si mwezi wa kheri kwa Arsenal ukiangalia rekodi ya huko nyuma lakini mwezi huu tumefanya vema tena kwa asilimia karibu 60.
Tukicheza na Man Utd,tunakumbana na Southampton, halafu Marseille na tutamaliza mechi za mwezi kwa kucheza na Cardiff City ya Wales.
Kesho tunaingia Old Traford tukiwa na rekodi nzuri ya ushindi dhidi ya Liverpool na Borussia Dortmund ya Germany.
Timu yetu itaingia uwanjani ikiwa na imani na kujiamini kwamba itapata ushindi kwa kumiliki mpira na kuuchezea watakavyo na kufunga magoli pindi wapatapo nafasi.
Arsenal kesho tunaingia Old Traford tukiwa hatuna shinikizo lolote kwani tunawazidi Man Utd kwa 8 points na ni wao wenye shinikizo la kuhakikisha hawamalizi mchezo wakiwa nyuma yetu kwa 11 points.
Kuhusu timu inayotarajiwa kuingia dimbani kwenye "theatre of dreams" ni ile ile ya kikosi cha kwanza iliyoifunga Liverpool na Borussia Dortmund, ingawa kama Flamini ataanza itabidi Thomas Rosicky apishe na aanze kwenye bench.
Hivyo basi timu inayotarajiwa ni ileile "killer machine" inayoundwa na wachezaji wafuatao:
Szczesny; Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs; Arteta, Flamini; Ozil, Ramsey, Cazorla; Giroud.
Tukutane tena hapa kesho jioni kwenye mida ya saa 12 za jioni kwa saa za Afrika Mashariki au saa 10 za jioni kwa saa za Ulaya hasa Uingereza.