Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Dakika ya 90

Southampton 1-1 Arsenal

Gibbs vipi?????

Dakika 3 za nyongeza
 
Sagna katuangusha leo ile clearance ni ya kizembe ... ..... .... .... tumepoteza points muhimu hapa ... ... .
 
Mechi zinazofuata: Ugenini kwa Man City, Ugenini kwa Chelsea, Emirates na West Ham kisha kuikaribisha Liverpool.
 
ashukuriwe mwamuzi wa pembeni kwa kuwabeba, mlishachapya leo
Dah!........Mshikaji una GUBU ka'a Asha Ngedere ati.....

Hivi goli la SOTON lililokataliwa kutokana na washambuliaji wa wawili wa SOTON kuzidi na lile la Wigan lililofungwa na Wigan muamuzi wa pembeni akakataa lipi lina afadhali?....

Ama ndo kunya anye kuku akinya bata kaharisha?
 
Lack of consistency is an understatement to this club.Last match we witnessed a 7 goals fiest against NU,today only a single own goal(O.G) to get a lucky draw...What a joke!!!
 
Mechi zinazofuata: Ugenini kwa Man City, Ugenini kwa Chelsea, Emirates na West Ham kisha kuikaribisha Liverpool.

Swansea vs Arsenal (away)-FA cup alafu Arsenal Vs City (home)-EPL then Chelsea vs Arsenal (Stamford bridge) kisha Arsenal vs Liverpool (home)

rekebisha hapo
 
Swansea vs Arsenal (away)-FA cup alafu Arsenal Vs City (home)-EPL then Chelsea vs Arsenal (Stamford bridge) kisha Arsenal vs Liverpool (home)

rekebisha hapo
Asante mkuu.

Nilisahau kusema mechi za premiership zinazofuata (nimeona ya Man city itakuwa nyumbani).. Mechi ya Arsenal WestHam 23 Januari ni kiporo cha mzunguko wa kwanza day 19. Mengine hamna tofauti kati ya niliyoandika na uliyoandika wewe.

Point yangu ni kuwa mzunguko wa pili wa ligi unaanza na mechi ngumu, Januari ikipita kwa mafanikio Arsenal itakuwa na confidence kubwa ya kumalizia hizo mechi nyingine
 
Kwa kweli niwe mkweli tu,hii timu mimi huwa siku zote naifananishaga na west ham,reading,qpr na si na chelsea,man zote nk,timu gani kubwa jinga,hata mipango haina hadi inawasononesha fans wake,hv kwa staili hii kweli hata tano bora itakuwepo,wenga,itendee haki hii timu
 
matokeo sio mabaya kihivyo tuangalie mbele man city kalizwa juzi nani alitegemea mpira unadunda na leo siku ilikuwa mbaya kwani wachezaji karibia wote hawakucheza vizuri
 
gooners mi hua nawaambia ukweli ndio maana mnamaindi sidanganyi kama mnavyojidanganya wenyewe kwa wenyewe hapa...sasa theo 100k per week ya nini...si bora mngempa rvp 200K coz at least mnajua mngekua mnafunga magoli mengi...mediocre manager mediocre team :biggrin1:
 
Wakuu Kashengo na wengine mambo niaje?

Dogo Theo Walcott usiku huu katia saini mkataba wa miaka minne.

Atakuwa akilipwa paundi 90000 kwa wiki.

Arsenal FC watatangaza kesho.

Pia deal la mshambuliaji Adrian Lopez nalo linaweza kukamilishwa kesho au mwishoni mwa wiki.

Kesho ntakuwepo hapa kutoa data.
 
Back
Top Bottom