Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,021
- 2,478
Hayati Apson Mwang'onda akisalimiana na Mwamba
Kuna wakati Profesa Tibaijuka, Waziri wa Ardhi wakati huo, alikuwa anaratibu mradi kabambe wa Kigamboni.
Wamarekani ndio walitaka kuujenga kwa mfumo wanaoutaka wao ili wautumie kwa namna wanavyotaka wao.
Ndani ya kivideo cha awali kwa ajili ya kuunadi mradi huo kulikuwa na sentensi kwamba kuna eneo litakuwa "a university for whites only."
Baada ya kelele za wananchi, "eagle eyed guys" walifuta hiyo sentensi.
Lakini pia Wamarekani walitaka kuitumia Kigamboni kama kituo chao cha ukachero wa kijeshi duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, wa wakati huo, Hayati Apson Mwang'onda aliuchinjia baharini mradi huu.
Profesa Tibaijuka alikubaliana na hoja za Apson.
Na sasa kwa sababu ya uzoefu huo, Prof anatwambia kwamba huu Mkataba wa Dubai na Tanzania ni "zimwi" kama lile "dude" la Kigamboni. Anashauri tuachane na mkataba wa Dubai.
Tunaomba busara za Apson zimtembelee DG wa TISS wa sasa tunapojadili mkataba wa awali wa DP World.