Apple waja na iphone ya bei nafuu iphone SE (2020)

Miki123

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
288
502
Apple wameamua kula sahani moja na makampuni yanayotengeneza budget phone.

Apple wamezindua simu ya iphone inayoitwa iphone SE.

Kitu kinachovutia kwa toleo jipya la simu hii ni bei nafuu kulinganisha na matoleo mengine ya hivi karibuni. Bei yake ni $399.

Hii bei ni kubwa kwa sisi watumiaji wa simu za kichina hasa Tecno lakini simu za iphone huwa ni gharama. kwa hiyo bei, ni nafuu sana.

images (1).jpeg


Sifa za iphone SE 2020 second generation.
Inatumia chip mpya ya a13 bionic ambayo mara ya kwanza ilitumika kwenye iphone 11 series.

Japo chip ina hexacore (core 6) ila imeipita chip snapdragon 855 kwenye performance ya single core kwa mujibu wa geekbench 4.4

Ukubwa wa RAM ni 3 gb.

Size ya screen ni inch 4.7 (simu kiportable).

Uwezo wa battery ni 1821 mAh (kama betri ndogo sana)

Simu ina uwezo wa kuzuia maji yasiingie ndani ya simu hata ukitia kwenye ndoo iloyojaa maji kwa dakika 30 kwani ina ip67 certification.

Sifa zingine kiundani zaidi gsmarena.

Apple iPhone SE (2020) - Full phone specifications

Kwa wajuvi, hivi hii price kweli inafaa kulinganisha na hizi specification? Kwani kuna za bei hii ziko njema.
 
Samsung, huwaei na oneplus wamewakalia pabaya wazee wa apple hata ubunifu umeisha kabisa, simu hiyo ni basic sana kwa huu mzigo wa pesa.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom