Apona ghafla tu baada ya Gari ya Wagonjwa iliyokuwa ikimkimbiza Hospitali kupata Ajali na Kuua Muuguzi na Dereva

MGONJWA aliyekuwa akiwahishwa katika Hospitali ya Wilaya Same, Ester Paresetwi (35) na gari likapinduka na kuua muuguzi na dereva amepona mara tu baada ya ajali.

Katika ajali hiyo ya gari la wagonjwa, muuguzi wa zahanati ya Kisiwani wilayani humo, Joshua Jacob (29) na dereva, Jumanne Makumbe (48) walikufa na wengine watatu walijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema jana majeruhi akiwemo mgonjwa aliyekuwa akipelekwa hospitali wanaendelea vizuri katika Hospitali ya Wilaya ya Same.

Alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Majevu Kata ya Kisiwani wilayani Same Agosti 7 mwaka huu saa 10 jioni wakati tairi la nyuma la gari lilipopasuka, likapoteza mwelekeo na kupinduka.

Chanzo: HabariLeo
Dah, hii hatari.....yaani mgonjwa kageuka kuwa muuguzi tena?
 
Alikua anatoka damu masikioni na mdomoni

Ila baada ya ajali damu zikakata

Akapona yeye na ndugu zake (wasindikizaji) dereva na nesi wakang'ata vumbi

Tena ilikua mita chache kufika hospitali ya wilaya (Destination )
Aliponea hospitali, Soma vizuri maelezo ya polisi
 
Back
Top Bottom