Aomba talaka kisa kapata kazi

Aomba talaka kisa kapata kazi

Kuna kesi ngumu kidogo hapa.

Jamaa yangu amekaa na Mke wake kwenye ndoa miaka 9 sasa. Kumbe Mke alikuwa anatafuta kazi sasa amepata.

Baada ya kumletea mume majibu amemnyima ruhusa kuajiriwa.

Mke anataka kazi, Mume hataki. Sasa Mke anataka talaka ili akafanye kazi. Je! Ampe?

AMpe tu mwana kwenda ,hao watu % kubwa wapo na sisi kwenye ndoa kwasababu hawajajipata ,wakijipata wanataka waishi wenyewe ila wakienda huko wakipigika ndipo wanakumbuka kurudi ila yakiwanyookea huwaoni.

Ukiona mwanamke ana pesa na anaishi kwenye ndoa basi jua huyo mme wake anajiweza kuliko yeye na kuna vitu anampa backup.
 
Mtaniii!!
Kukubaliana nini? Mke apewe talaka, kuna maisha nje ya ndoa.
Uhuru wa kiuchumi ni muhimu kuliko ndoa.

Au wee unasemajee? 😂😂😂😂😂
Nilichomaanisha kukubaliana kumtimizia mke wake kile ambacho mwanamke anaweza kukifanya akiwa na ajira yake.

Hahahaaa. Ni kweli uhuru wa kiuchumi ni muhimu Mtani japo mwenzio kuachana huwa sikubariki sijui ndo uzee. 🤪

Yaani napenda watu waachane ikiwa hamna suluhisho lingine. 😅
 
Mtaniii mie sipendi kuachana zaidi ya neno lenyewe. Ila inapobidi hakuna namnaa.

Uhuru wa kiuchumi ni muhimu kuliko chochote kile.
Sasa mume hataki mke, afanye kazi ya ajira yake why? Na hadi mke adai talaka km hatakiwi kufanya kazi, means huyo mume kuna mapungufu anayo ktk uwajibikaji kwenye ndoa yao

😂😂😂😂
 
Itakuwa alikuwa anateswa sana....
Kupata kazi kwa mke mna watoto wawili ni baraka, hata mume atapata muda wa kuchepuka.....
Hapo waachane ili mwanamke apate muda wa kufanya kazi free au aondokane na mateso? Watoto vipi
 
Nikiwa kama mume mwenye uwezo wa kumhudumia mke wangu kwa kadri ya kipato kwangu itakuwa ngumu kukubali mke wangu akafanye kazi........lakini pia siwezi kumshikilia mateka mtoto wa watu ambaye wazazi au walezi wamemsomesha kwa gharama kubwa.......nitampa taraka yake ili akawe huru kufanya kazi zake!!!!
 
Kwangu binafsi siwezi muacha mke wangu akafanye kazi unless nimemfungulia biashara mwenyewe ambayo ninauwezo wa kuifunga nikishaona kuna uwalakini ila kumuacha akaajirowe HAPANA.
 
Binafsi siwezi kubali akaajiriwe hata siku moja maana atabadilisha kila mtazamo chanya kuwa hasi......hapo alitakiwa kumfungulia biashara ambayo itamfanya awe busy kutafuta pesa tu na sio kumfanya mama wa nyumbani
 
Ndo upate somo hapo kabla hujamuoa huyo family friend wako.
 
Ndo upate somo hapo kabla hujamuoa huyo family friend wako.
Family friend wangu tayari ana kazi ambayo mimi ndio nimemuweka hapo, akiketa ABCD naipiga chini hiyo kazi, nashukuru Mungu anafanya kazi yangu mwenyew kwa kivuli cha jina lake.
 
Ampe TU!

Wanawake wanajua WWanachokitafuta Kwa sisi wanaume!lakini sisi ni vigum kujua kwanini waliamua kuishi na sisi Hadi pale malengo yanapotimia!!!

Ukiona ameanza kusema TUACHANE TUACHANE,NENDA TU UNIACHE NA WANANGU!MARA WEWE KWANI KITU GANI WEWE!!

Ukianza kuona haha kwenye majibizano ya hasira!go just go brother move on!your not a hero anymore!
 
Kuna kesi ngumu kidogo hapa.

Jamaa yangu amekaa na Mke wake kwenye ndoa miaka 9 sasa. Kumbe Mke alikuwa anatafuta kazi sasa amepata.

Baada ya kumletea mume majibu amemnyima ruhusa kuajiriwa.

Mke anataka kazi, Mume hataki. Sasa Mke anataka talaka ili akafanye kazi. Je! Ampe?
Hivi ile Toyota vip inunue faster shem apunguzie munkari wakutaka talaka 😅
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom