Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana

Mmeanza drama!

Fictional short story mixed with propaganda!

Ukiisoma habari yenyewe utagundua ni habari iliyojaa uwongo ambao kama hutumii fikra pana huwezi kugundua.

Ukiangalia kwa jicho la pili utagundua kuna uwezekano CHADEMA wanataka kufanya maovu au kumteka/kumficha mgombea/wagombea wao ili waseme, mmeona tuliwaambia mapema kuwa haya yatatokea.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wameanza kuwajenga kisaikologia ''makamanda'' katika mipango yao.

Wajumbe aliowataja ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ambayo ni kawaida kukaa ili kutathmini hali ya usalama katika mkoa.

Tokea mwaka 1996 mmnatuambia taifa linaelekea kubaya! huko kubaya ni wapi ambako hatufiki?

Ninajua baada ya uchaguzi mtakuja na nyimbo zilezile za kuibiwa kura.
Mkuu Herry James naye ni mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama?. Halafu hoja siyo ujumbe kwa mwenye akili hoja ni yaliyojadiliwa na wajumbe. Kwani watu sahihi hawawezi kujadili na kupanga upuuzi, au wajumbe sahihi wakikutana na kupanga mambo ya hovyo siyo kosa wala hakuna shida kwasababu ni wajumbe sahihi?. Wewe ni hopeless , huna uwezo wa kufikiri ,umepofushwa na njaa ya kutaka uteuzi na kwa unafiki huu utakufa mdomo wazi kama mzoga.
 
Kamanda, inaelekea wewe unawajua waliomuua, na ni kwa nini ameuawa?!


Ili kuwaondoa UKAWA kwenye akili na muelekeo wa uchaguzi na badala yake wazielekeze msibani na hivyo lupunguza kasi yao. Ilishatokea Arumeru Mashariki (marehemu Mbwambo) na Geita (marehemu Mawazo) na mifano mingine mingi tu.
 
cocochanel Sesimba

cocochanel,
Hapa hakuna uchochezi wala dada yake uchochezi,
These are facts. Kama hawa waliotajwa RC,RPC,OCD,OCS,DC na Mbunge , hawahusiki basi wajitokeze na wakanushe hiyo taarifa...!!!
Unakumbuka sakata la madiwani Arusha na jinsi Mhe. Nassari alivowaumbua kina M-Nyeti na mikakati yao ya kununua MADIWANI wa CHADEMA??? The info tech have changed and advanced to a stage whereby a very small camera(audio/viedo) to a size of a mustard seed can record anything anywhere to the required quality standards.....!!

Kuna kitu Rais Magufuli na hii anayoita Serikali ya CCM anatakiwa kujua..! Kwamba asifikiri/wasifikiri au kujidanganya kwamba Wapinzani wanachukiwa na kila mtu.....!!!Kuna watu wapo ndani ya CCM, Serikali na vyombo vya Usalama hawapendi huu ushenx na unyama wanaofanyiwa ndugu zao wa Upinzani. Hivi kwa akili ya Magufuli anafikiri familia zote na koo zote ziko CCM?? Unaweza kuwa CCM lakini mtoto wa mjomba, shangazi, bamdogo/mkubwa wakawa CHADEMA...!!Hivi unategemea nitakubali ndugu yangu kiukoo auawe au adhulumiwe HAKI yake kisa yuko upinzani??Hilo ni jambo lisilowezekana....!!

Kilichotokea kwene hiyo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza kuna mtu ameigia na Camera na kuerkodi kila kitu mwanzo mwisho....na ana siri zote na picha za Wahusika. Tunajua CCM na Policcm watajitetea na kucheza mchezo wao mchafu wa kujilinda kama walivyopotezea kwa Ushahidi wa Nassari....Lakini UMMA WA WATANZANIA UNAONA, UNAJUA NA UNAFAHAMU kinachoendelea hapa Tanzania kwa sasa....!!!

Ni swala la muda tu, hawa wanaojifanya kuitetea CCM na Serikali yao itakula kwao. Wao ni binadamu tu kama hawa binadamu walioko Upinzani ambao kwa vile wako CHAMA TWAWALA wanawaona UPINZANI ni Wahaini, Wasaliti na Wapinga Maendeleo ilhali ni kinyume chake. Hizi CHUKI zinazotengenezwa na CCM wakisaidiana na POLICCM zitakapoanza kutoa matokeo HASI kwa CCM wawe tayari kuyakubali na kuyapokea. Kama Utawala wa MAKABURU(The Boers)waliokuwa WACHACHE ilifika mahali ukasalimu amri kwa Wana South Afrika seuze Utawala wa WALIO WACHACHE TOKA CCM...????

Anacho kijenga,kuki tengeneza na kukilea Rais Magufuli ajue tu kwamba kitakuja kumgharimu kwenye awamu yake hii au hata baada ya kuondoka madarakani....!!Rwanda na Burundi walianza ujinga kama huu na mwisho wake ilikuwa ni mauaji ya KIMBARI. Magufuli aisifikiri Watanzania anawanyanyasa, kuwakandamiza na kuwaonea sasa kwa vile tu wako upinzani wana mioyo ya MAWE...!!!Hawa ni Watanzania kama yeye(not sure if he's Inatarahamwe or a Tanzanian) wanapata maumivu na uchungu na iko siku WATALIPIZA KISASI!! Haiwezekani DAMU ya ndugu zetu Watanzania iwe inamwagika kwasababu za kijinga kama hizi....halafu watu waendelea kunyamaa!
 
Wewe uliyekohuko umechukua hatua gani kabla ya kuja humu jf?

Pili,unataka wananchi wakusaidie nini labda au waipigie kula chadomo?
 
Katika hali ya sasa ni vigumu mtu kuibuka na tuhuma nzito kama hizo pasipo kuwa na ushahidi wa kutosha au kuwa na uhakika na unachokisema kwasababu hata wao wakijua unachokisema ni sahihi,wataogopa kukushitaki maana watakuwa na hofu ya wewe kuwalipua mahakamami na zaidi watakuwa na wasiwasi na mtandao mzima uliokupa habari hizo.

Binafsi naamini hii itakuwa ni kazi ya baadhi ya watu waliopokelewa kwa mbwembwe wakidhani wana mapenzi na chama chao kumbe walivutiwa tu na vipande thelathini vya fedha na haya ndio yanaweza kuwa ni matokeo na malipo ya kufanya mambo kwa kukurupuka.

Mabwana hawa si lazima wawepo kwenye kikao husika ila wanaweaza kupokea taarifa kutoka kwa walioshirika katika kikao hicho na wao kuzivujisha maana hawana mapenzi ya dhati na upande uliopo na hivi wako wengi ni vigumu hata kujua nani anaweza kuhusika.


Sitashangaa mipango yao mingi ikaendelea kuvuja kwasababu walifanya kosa la kupokea watu wengi na wote wakawaamini wakasahau watu hawa hawakuhamia huko kwa mapenzi yao bali kwa ushawishi fulani.

Namalizia kwa kusema, "apandacho mtu, ndicho avunacho na damu ni nzito kuliko maji."
 
Molembe Watu kama nyie ndiyo mnataka mpewe dhamana ya kuiongoza nchi hii kweli?

Kwa style hii ya majibu sahauni kabisa kutawala au kuongoza nchi hii upumbavu wenu pelekeni kwenye familia zenu
 
Kiukweli mimi ni kama Tomaso, siiamini taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, lakini hoja hii ya Lissu,

"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.

Sababu ya kutoiamini kauli hii ni kwa sababu inabeba criminal liability za aina mbili
Accessories After The Fact: Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, Jeshi letu la polisi limeshindwa kufanya chochote kwa sababu limekosa pa kuanzia baada ya kukosa shuhuda yoyote wa kumuhoji, na kuna camera za CCTV zilirekodi, zimetoweka, hivyo hakuna kabisa pa kuanzia uchunguzi!.

Kumbe kuna watu wamejifungia katika ukumbi wa BOT Mwanza akiwemo RC na RPC ambao ndio walihusika na shambulio lile!.They are all, accessories after the fact, wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa kuhusu sambulio la Lissu!.

Kwa vile RPC nae ni mhusika, hivyo hakuna mahali pa kuanzia, ila naamini kwa vile Mwigulu ni member wetu humu, atawatuma vijana wake wakawahoji wahusika waliotajwa, tena nawaomba wasimsumbue kabisa Ngurumo kumtaja source wake, kama ameitoa taarifa hii kwa kofia yake ya uandishi wa habari, kwa sababu sisi waandishi tuna kinga ya kihabari ya "the confidentiality of the source".

Kama ameitoa kama Makamo Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa, alipaswa kesho yake kuondoka Mwanza kwa ndege ya kwanza na kufikia mezani kwa Mwigulu, kisha kwenda mezani kwa Kipilimba kuripoti, halafu ndipo ailete humu!.

Criminal liability ya aina ya pili, ni accessories before the fact, ambapo watu wakubwa, wazito wa mkoa wamekutana kupanga kufanya jinai!.
Any good citizen akisikia ni wajibu wake kuripoti, kwa vile RC na RPC ni wahusika, waliosikia wakaripoti kwa Ngurumo, kwa vile Ngurumo sio Mlinzi wa Amani, tariffs hiyo ni very sensitive ilibidi Ngurumo amuongoze mtoa taarifa wake kwa mlinzi wa amani, Waziri aelezwe, IGP aelezwe, na Amiri Jeshi aelezwe, ili wahalifu hawa, watiwe mbaroni haraka kabla hawajatekeleza jinai hii!.

NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, ambao wana mamlaka ya kumkaribisha mtu yoyote kwenye kikao chao hata kama sio mjumbe. Hivyo hii isijekuwa ni leakage ya taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mila, imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!. Hivyo this leaves much to be desired, kumbe hizi ndizo kazi za kamati zetu za ulinzi na usalama za mikoa!. Nimemkumbuka Kamanda Mawazo!' RIP Kamanda Alphonce Mawazo, damu yako haitapotea bure, sasa imeanza kuchemka na kuibua madudu yanayofanyikaga!.

Ila pia sisi raia wema wa nchi hii, tufanye responsible blogging kwa self censorship ya sensitive info, tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, nyingine ni political capitalization tuu!, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.
P
Kuhusu madudu ya Kamati za Ulinzi na Usalama, nimeyazungumza hapa

TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!

Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Paskali
Na wewe mayala amuamoja kutumia kiingereza chao au kiswahili chako,habari ya kutuchanganyia lugha humu ni upuuzi kabisa,tambua jamii yako ndiyo wahusika wa hii habari zaidi siyo wazungu.

Badilika
 
Wala msiwasingizie hao waliohamia, kwani mnafikiri miongoni mwetu wote tunawaza pamoja kama mazombie?
Hata miongoni mwetu kuna migawanyiko mikubwa unatafutwa muda sahihi tu. Katika siasa mkakati ni tafuta taarifa, kamata taarifa, hakiki taarifa , tunza tasrifa na ushahidi juu ya taarifa.
Then relax, subiri muda na wakati sahihi.
 
Huyu Ansbert anapaswa KUMPA MSAADA Kamanda MSANGI kwani hayo aliyoyaeleza hasa kuhusu LISSU yanahitaji UFAFANIZI WA KINA, " WALIPANGA KUMUUA" ???

kwa ufilirivu wako ktk hilo shambulio walitaka kumjeruhi tu na siyo kumuua? nyie watu IQ zetu sijui mnazitumiaga wap
 
Wala msiwasingizie hao waliohamia, kwani mnafikiri miongoni mwetu wote tunawaza pamoja kama mazombie?
Hata miongoni mwetu kuna migawanyiko mikubwa unatafutwa muda sahihi tu. Katika siasa mkakati ni tafuta taarifa, kamata taarifa, hakiki taarifa , tunza tasrifa na ushahidi juu ya taarifa.
Then relax, subiri muda na wakati sahihi.
Hata hili unalolisema linawezekana maana huenda wako ambao hawaridhishwa na mambo haya ingawa wako kimya.
 
Duh mbona tunakoelekea siko hiv ikijafikia wakati viongozi wa ccm nao wakianza kuwawa serikali itasemaje
 
Back
Top Bottom