Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana

Anaandika Ansbert Ngurumo

*Very important Tip:*

CCM na polisi jana usiku kuanzia saa 2:37 walijifungia katika ukumbi wa BoT Mwanza kupanga wizi wa kura.

1. Kikao kilianza saa 2:37
2. Washiriki walikuwa 36.
3. Kiliongozwa na John Mongela, mkuu wa mkoa.
4. Miongoni mwa washiriki ni hawa wafuatao:

1. Mkiti CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athumani

2. Mkuu wa mkoa, John Mongela

3. Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Mary Tesha

4. OCD Nyamagana, Ochieng Aiago

5. OCS wa kituo cha Mirongo, Ayub Khaji

6. Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa

7. Mbunge wa Nyamagana, Stanislaus Mabula

9. Mkiti wa UVCCM Taifa, Heri James

10. RPC wa Mwanza, Ahmed Msangi

Mbunge wa Ilemela (Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Angelina Mabula, *HAKUWA KIKAONI*

*Kinondoni*

Walijadili Kinondoni kwa kifupi sana, kwamba:

- Dalili zinaonyesha kuwa Salum Mwalimu atashinda. Hivyo, CCM wameamua kutumia mbinu waliyotumia kwenye Kata za Arumeru mwezi Novemba 2017. Kuzuia au kuondoa mawakala wa UKAWA.

*Siha* haikujadiliwa kabisa.

Lakini waliambizana kuwa serikali imeamua kufanya chaguzi ndogo kwa awamu ili wapinzani wenye kiherehere wapate fursa ya kukusanyika mahali pamoja, washughulikiwe mmoja mmoja. Kufikia 2020 upinzani utakuwa umekosa watu wa kuuamsha kwa sababu wenye nguvu watakuwa wameondolewa.

Pili, walikiri kwamba mgomo wa Chadema kutoshiriki uchaguzi uliopita umewaonyesha kwamba wapinzani wana nguvu, wanaungwa mkono na umma, kwa kuwa wapigakura walipungua sana.

Kwa hiyo, shabaha ya CCM sasa ni kuwashugulikia kijeshi ili viongozi wa upinzani wapotee.

Tatu, walilaumiana kwamba kuna watu wanapewa majukumu makubwa yanawashinda kukamilisha.

Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*

*Isamilo,* Mwanza

Kuhusu Kata ya Isamilo, wamekiri kwamba mgombea wao hauziki, na kwamba wakazi wengi wa kata hiyo ni washashi (watu wa Mara). Lakini wakasema amri imetoka juu kwamba lazima CCM washinde kwa kuwa kata hiyo ipo eneo na makazi ya mkuu wa mkoa na ndipo Ikulu ndogo inakohamishiwa, na kwamba rais hapendi kuishi kwenye kata inayoongozwa na wapinzani.

Waliazimia yafuatayo:

1. Kuteka mgombea wa Chadema wakati wowote kuanzia sasa, hasa nyakati za asubuhi.
2. Kuanza patrol za polisi usiku ili kukamata vijana wanaodhaniwa kuwa wanaunga mkono Chadema.
3. Kazi ya kuteka mgombea imekabidhiwa kwa mtu anaitwa Banny, mkazi wa Lucherere, ambaye sasa amepewa makazi ya muda katika kata hiyo, akiwa mgeni wa aliyekuwa mwenyekiti wa Kata ya Nyakabungo, ambaye sasa hivi ana uongozi katika ngazi ya kata.
4. Usiku wa tarehe 16 kuamkia 17, polisi na green guard watafanya doria maalumu kwa ajili ya kukamata wana Chadema na kuwatisha.

Magari matatu yamepangwa kutumika - Noah, na Landcruiser mbili.

Moja itakuwa maeneo ya *Kwa Malisa,* katika mpaka wa Nyamanoro na Isamilo. Nyingine itakuwa gengeni kwa Wahema. Nyingine itakaa kwenye makutano ya Isamilo na Thaqafa.

5. Noah itatumiwa kubeba sukari na sabuni kwa ajili ya kuhonga wapigakura (kipande cha sh. 300 na robo kilo ya sukari sh.650).

6. Land cruiser moja itabeba green guard ili kukamata watu wa Chadema watakaokuwa kwenye patrol usiku. Magari hayo yataegeshwa kwa Wahema na Mikoroshini.

7. Siku ya kupiga kura, green guard, ambao katika mikutano ya mgombea wamekuwa wanajitokeza kama wasanii, ndio watatumika kutisha, kupiga na kuzuia watu njiani wanaokwenda kupiga kura.

Kikundi hiki kinafadhiliwa na mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula. Na jana alitoa taarifa kikaoni kuwa kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya posho, lakini sasa amefaulu kuimaliza.

INFORMATION IS POWER. TUJIPANGE.

*Ansbert Ngurumo*
Makamu Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Victoria
14:02:2018
wanachadema bwana sometimes mnaboa sana,kama mnadetails za namna hii,kwanini uziweke hapa? Mfano huyo aliyekabidhiwa jukumu la kuteka wengine yeye hana roho? Why msimuanze yeye,hayo magari? Petrol imeosha kwenye vituo vya mafuta? Kama unasema police walikuwa kwenye hicho kikao unalialia mini badala ya kujihami? Hivi nyie mnadhani boko haramu waliibuka from no where?
 
Mmeanza drama!

Fictional short story mixed with propaganda!

Ukiisoma habari yenyewe utagundua ni habari iliyojaa uwongo ambao kama hutumii fikra pana huwezi kugundua.

Ukiangalia kwa jicho la pili utagundua kuna uwezekano CHADEMA wanataka kufanya maovu au kumteka/kumficha mgombea/wagombea wao ili waseme, mmeona tuliwaambia mapema kuwa haya yatatokea.

Mmeanza kiuwajenga kisaikologia ''makamanda''.

Wajumbe aliowataja ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ambayo ni kawaida kukaa ili kutathmini hali ya usalama katika mkoa.

Tokea mwaka 1996 mmnatuambia taifa linaelekea kubaya! huko kubaya ni wapi ambako hatufiki?

Ninajua baada ya uchaguzi mtakuja na nyimbo zilezile za kuibiwa kura.
1996 ni uwongo, labda uwadanganye ambao walikuwa hawajazaliwa, awamu hii ndio inayopeleka taifa kubaya
 
Kiukweli mimi ni kama Tomaso, siiamini taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, lakini hoja hii ya Lissu,

"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.

NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, hivyo hii isijekuwa ni taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!.

Tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.
P
Siku hizi nafatilia saana michango yako kwenye jukwaaa.
What can I see, you're no longer neutral!!!!

Kuna mtu kakuweka gia namba 1 na kakanyaga mafuta mpaka mwishoo.
Mwendo mdogo kelele kibao.

RIP free speech in Tanzania
 
Kiukweli mimi ni kama Tomaso, siiamini taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, lakini hoja hii ya Lissu,

"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.

NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, hivyo hii isijekuwa ni taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!.

Tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.
P
Mkuu Pasco jitahidi kuwa objective. Hii hai-qualify kuwa taarifa ya Kamati ya ulinzi na usalama. Sababu, moja, Kheri James si mjumbe wa kamati hiyo. Mbili, Mwenyekiti wa CCM mkoa si mjumbe pia. Na wengine wengi.

Jambo lingine ni kwamba, hata kama NI SIRI. Ila hatuna siri ktk udhalimu wowote. Pia kumbuka wkt wa ukatibu mkuu wa Dr. Slaa, ndiye alikuwa kinara wa kuanika siri tena za ndani kabisa.

Mwisho, unashangaa watu kutoa huo mfano. Hivi unawaelewa polisi na hawa wakuu wa mikoa.
Nitafute nikuthibitishie walivyo na uwezo mfu ktk kufikiri na kusema. Kwani huyo Mongella hawezi kusema hivo?!!. anasema sana na huo mfano usikute ni yeye alitoa.

Anyway sijui unaionaje hali ya nchi saivi. Mimi nipo mtaani, wengi wamejaa hofu. Hivi unafikiri waTz milion 50 watajaa hofu for nothing?. Subirini siku wakianza kujitetea. Ndo mtajua kwamba wana Mungu.

Tupo katika nchi ambayo mbunge wa CCM anatibiwa kwa hela za serikali huku mwingine wa CHADEMA anakosa sifa za kugharamikiwa matunzo/matibabu. Wewe huoni hiyo tu ni ishara mbaya.
 
"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*".

Hii siamini!.
P
Nikuulize kama Mnyeti RC wa Manyara kasema hatashirikiana na diwani wa upinzani [CHADEMA] (na Ikulu haijamkemea mpaka sasa..!!), unafikiri hajasetiwa/kutumwa kuyasema hayo?. Nimesikia TAMISEMI walimwambia awape ufafanuzi, akawajibu hivyo hivyo, sasa sijui watatoa mwongozo gani.

Niambie Hayati Baba wa Taifa JKN angevumilia kauli ya namna hii kweli?. Hivi uongozi wa awamu ya tano unataka kuijenga tanzania kuwa nn?. Kwani vitu ambavyo huondoa amani ktk nchi sio utengano na ubaguzi?

...ubaguzi ni dhambi mbaya sana,ni sawa na kula nyama ya mtu, ..... Mwl. JKN (RIP)
 
Anaandika Ansbert Ngurumo

*Very important Tip:*

CCM na polisi jana usiku kuanzia saa 2:37 walijifungia katika ukumbi wa BoT Mwanza kupanga wizi wa kura.

1. Kikao kilianza saa 2:37
2. Washiriki walikuwa 36.
3. Kiliongozwa na John Mongela, mkuu wa mkoa.
4. Miongoni mwa washiriki ni hawa wafuatao:

1. Mkiti CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athumani

2. Mkuu wa mkoa, John Mongela

3. Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Mary Tesha

4. OCD Nyamagana, Ochieng Aiago

5. OCS wa kituo cha Mirongo, Ayub Khaji

6. Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa

7. Mbunge wa Nyamagana, Stanislaus Mabula

9. Mkiti wa UVCCM Taifa, Heri James

10. RPC wa Mwanza, Ahmed Msangi

Mbunge wa Ilemela (Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Angelina Mabula, *HAKUWA KIKAONI*

*Kinondoni*

Walijadili Kinondoni kwa kifupi sana, kwamba:

- Dalili zinaonyesha kuwa Salum Mwalimu atashinda. Hivyo, CCM wameamua kutumia mbinu waliyotumia kwenye Kata za Arumeru mwezi Novemba 2017. Kuzuia au kuondoa mawakala wa UKAWA.

*Siha* haikujadiliwa kabisa.

Lakini waliambizana kuwa serikali imeamua kufanya chaguzi ndogo kwa awamu ili wapinzani wenye kiherehere wapate fursa ya kukusanyika mahali pamoja, washughulikiwe mmoja mmoja. Kufikia 2020 upinzani utakuwa umekosa watu wa kuuamsha kwa sababu wenye nguvu watakuwa wameondolewa.

Pili, walikiri kwamba mgomo wa Chadema kutoshiriki uchaguzi uliopita umewaonyesha kwamba wapinzani wana nguvu, wanaungwa mkono na umma, kwa kuwa wapigakura walipungua sana.

Kwa hiyo, shabaha ya CCM sasa ni kuwashugulikia kijeshi ili viongozi wa upinzani wapotee.

Tatu, walilaumiana kwamba kuna watu wanapewa majukumu makubwa yanawashinda kukamilisha.

Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*

*Isamilo,* Mwanza

Kuhusu Kata ya Isamilo, wamekiri kwamba mgombea wao hauziki, na kwamba wakazi wengi wa kata hiyo ni washashi (watu wa Mara). Lakini wakasema amri imetoka juu kwamba lazima CCM washinde kwa kuwa kata hiyo ipo eneo na makazi ya mkuu wa mkoa na ndipo Ikulu ndogo inakohamishiwa, na kwamba rais hapendi kuishi kwenye kata inayoongozwa na wapinzani.

Waliazimia yafuatayo:

1. Kuteka mgombea wa Chadema wakati wowote kuanzia sasa, hasa nyakati za asubuhi.
2. Kuanza patrol za polisi usiku ili kukamata vijana wanaodhaniwa kuwa wanaunga mkono Chadema.
3. Kazi ya kuteka mgombea imekabidhiwa kwa mtu anaitwa Banny, mkazi wa Lucherere, ambaye sasa amepewa makazi ya muda katika kata hiyo, akiwa mgeni wa aliyekuwa mwenyekiti wa Kata ya Nyakabungo, ambaye sasa hivi ana uongozi katika ngazi ya kata.
4. Usiku wa tarehe 16 kuamkia 17, polisi na green guard watafanya doria maalumu kwa ajili ya kukamata wana Chadema na kuwatisha.

Magari matatu yamepangwa kutumika - Noah, na Landcruiser mbili.

Moja itakuwa maeneo ya *Kwa Malisa,* katika mpaka wa Nyamanoro na Isamilo. Nyingine itakuwa gengeni kwa Wahema. Nyingine itakaa kwenye makutano ya Isamilo na Thaqafa.

5. Noah itatumiwa kubeba sukari na sabuni kwa ajili ya kuhonga wapigakura (kipande cha sh. 300 na robo kilo ya sukari sh.650).

6. Land cruiser moja itabeba green guard ili kukamata watu wa Chadema watakaokuwa kwenye patrol usiku. Magari hayo yataegeshwa kwa Wahema na Mikoroshini.

7. Siku ya kupiga kura, green guard, ambao katika mikutano ya mgombea wamekuwa wanajitokeza kama wasanii, ndio watatumika kutisha, kupiga na kuzuia watu njiani wanaokwenda kupiga kura.

Kikundi hiki kinafadhiliwa na mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula. Na jana alitoa taarifa kikaoni kuwa kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya posho, lakini sasa amefaulu kuimaliza.

INFORMATION IS POWER. TUJIPANGE.

*Ansbert Ngurumo*
Makamu Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Victoria
14:02:2018
Kwani tulikuwa pazuri?
 
Kujitoa mtajitoa nyie mliozoea vya kunyonga. Sasa hivi ni kuwataarifu makamanda kutembea ni viberiti na petrol, tendo lolote la sintofahamu ni kumaliza game on the spot.
Ahsante mkuu tindo. Mimi na wewe tukipewa uongozi CDM kwa kweli huyo mtekaji atakuwa ni kitoweo kwa vijana wetu.
Hii mbinu ya kuwa na petrol kidogo na kiberiti ni nzuri. Yani anaangamizwa kwenye ulingo wa mapambano na mapanga/mashoka yao.
Vitu hivi vinatia hasira sana. Nchi yetu inaharibiwa na hawa CCM wao utafikiri sio waTz..
 
Jamani hilo tukio la lisu lenye uzito wake kitaifa na kimataifa lijadiliwe mbele ya watu wengi hivo pamoja na watoto wadoga kama akina Heri hapo jamaa ndo alipochochora kuunda propanganda
Kwani hujui Kheri ni 'kitengo'. Au kwa vile ana mwamvuli wa UVCCM?... Haya kuwa uyaone..
 
Hayo maneno hata tumbili anayaandika

Teknolojia ya sasa ndio yote

Huyo mchochezi arushe kideo tuwasikie huku tukiwaona na sura zao zote na iambatane na audio pia kivyake.

Yaani chadema wamekuwa alosto kweli kweli..

Kesho mwingine atabeba picha baada ya kumuua mtu akidai kauliwa na chama tawala.. kumbe yeye ndie anahusika kisa kulilia kura kwa kuua wenzao.. ila mwisho wao uje haraka watu wajue maovu yao.. chama bomu kila siku uongo na kusingizia.
Nyie ccm niviumbe vya kiuaji kabisa hamna huruma na taifa la masikini unaweza kuniambia ile video ya mnyeti mliifanyia kazi gani?

Mungu yupo ipo siku nyie simna act watemi.siku yaja tutavurugana mpaka heshima ijengeke ktk hili taifa.
 
Una macho?? Naam maana usingeandka upuuz huu au la umeandikiwa Kama pabaya had Leo huoni tukisema tumefika pabaya ni pabaya kweli
Kaa ujitathimini au ufute huu ujumbe maana hakuna hata point au lah majizi menzio yatakukana mbele ya safari
Ni kweli mkuu tumefika point mbaya sana. Ila wao wana CCM wanajitia hawaoni. Nahisi wana ushirikiano na shetani.
 
.....
....sadaka ntapeleka nako juwa ni upumbavu wa kiwango cha sherani mnakula na kusaza
 
"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*".

Hii siamini!.
P
Pascal kuna mengine ata hutaki kuamini una amini kimya kmya tuu.maana hii nchi inaelekea kubaya Kama mtu anakamatwa na rushwa live na anapandishwa ngazi,mtu ana tamka hataki ushilikiano na upinzani lakini still yupo anapeta sasa ntashangaa usiamini hili.

Serikali hii niya hovyo kabisa nabila kukemea ipo siku litatokea la kutokea.kumwaga damu nikitu kdogo sana ila kunawatu wanazani labda mpaka litokee giza la ajabu navitu vingi vya hatari.

"Muwa ulizamisha meli."
 
Anaandika Ansbert Ngurumo

*Very important Tip:*

CCM na polisi jana usiku kuanzia saa 2:37 walijifungia katika ukumbi wa BoT Mwanza kupanga wizi wa kura.

1. Kikao kilianza saa 2:37
2. Washiriki walikuwa 36.
3. Kiliongozwa na John Mongela, mkuu wa mkoa.
4. Miongoni mwa washiriki ni hawa wafuatao:

1. Mkiti CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athumani

2. Mkuu wa mkoa, John Mongela

3. Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Mary Tesha

4. OCD Nyamagana, Ochieng Aiago

5. OCS wa kituo cha Mirongo, Ayub Khaji

6. Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa

7. Mbunge wa Nyamagana, Stanislaus Mabula

9. Mkiti wa UVCCM Taifa, Heri James

10. RPC wa Mwanza, Ahmed Msangi

Mbunge wa Ilemela (Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Angelina Mabula, *HAKUWA KIKAONI*

*Kinondoni*

Walijadili Kinondoni kwa kifupi sana, kwamba:

- Dalili zinaonyesha kuwa Salum Mwalimu atashinda. Hivyo, CCM wameamua kutumia mbinu waliyotumia kwenye Kata za Arumeru mwezi Novemba 2017. Kuzuia au kuondoa mawakala wa UKAWA.

*Siha* haikujadiliwa kabisa.

Lakini waliambizana kuwa serikali imeamua kufanya chaguzi ndogo kwa awamu ili wapinzani wenye kiherehere wapate fursa ya kukusanyika mahali pamoja, washughulikiwe mmoja mmoja. Kufikia 2020 upinzani utakuwa umekosa watu wa kuuamsha kwa sababu wenye nguvu watakuwa wameondolewa.

Pili, walikiri kwamba mgomo wa Chadema kutoshiriki uchaguzi uliopita umewaonyesha kwamba wapinzani wana nguvu, wanaungwa mkono na umma, kwa kuwa wapigakura walipungua sana.

Kwa hiyo, shabaha ya CCM sasa ni kuwashugulikia kijeshi ili viongozi wa upinzani wapotee.

Tatu, walilaumiana kwamba kuna watu wanapewa majukumu makubwa yanawashinda kukamilisha.

Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*

*Isamilo,* Mwanza

Kuhusu Kata ya Isamilo, wamekiri kwamba mgombea wao hauziki, na kwamba wakazi wengi wa kata hiyo ni washashi (watu wa Mara). Lakini wakasema amri imetoka juu kwamba lazima CCM washinde kwa kuwa kata hiyo ipo eneo na makazi ya mkuu wa mkoa na ndipo Ikulu ndogo inakohamishiwa, na kwamba rais hapendi kuishi kwenye kata inayoongozwa na wapinzani.

Waliazimia yafuatayo:

1. Kuteka mgombea wa Chadema wakati wowote kuanzia sasa, hasa nyakati za asubuhi.
2. Kuanza patrol za polisi usiku ili kukamata vijana wanaodhaniwa kuwa wanaunga mkono Chadema.
3. Kazi ya kuteka mgombea imekabidhiwa kwa mtu anaitwa Banny, mkazi wa Lucherere, ambaye sasa amepewa makazi ya muda katika kata hiyo, akiwa mgeni wa aliyekuwa mwenyekiti wa Kata ya Nyakabungo, ambaye sasa hivi ana uongozi katika ngazi ya kata.
4. Usiku wa tarehe 16 kuamkia 17, polisi na green guard watafanya doria maalumu kwa ajili ya kukamata wana Chadema na kuwatisha.

Magari matatu yamepangwa kutumika - Noah, na Landcruiser mbili.

Moja itakuwa maeneo ya *Kwa Malisa,* katika mpaka wa Nyamanoro na Isamilo. Nyingine itakuwa gengeni kwa Wahema. Nyingine itakaa kwenye makutano ya Isamilo na Thaqafa.

5. Noah itatumiwa kubeba sukari na sabuni kwa ajili ya kuhonga wapigakura (kipande cha sh. 300 na robo kilo ya sukari sh.650).

6. Land cruiser moja itabeba green guard ili kukamata watu wa Chadema watakaokuwa kwenye patrol usiku. Magari hayo yataegeshwa kwa Wahema na Mikoroshini.

7. Siku ya kupiga kura, green guard, ambao katika mikutano ya mgombea wamekuwa wanajitokeza kama wasanii, ndio watatumika kutisha, kupiga na kuzuia watu njiani wanaokwenda kupiga kura.

Kikundi hiki kinafadhiliwa na mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula. Na jana alitoa taarifa kikaoni kuwa kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya posho, lakini sasa amefaulu kuimaliza.

INFORMATION IS POWER. TUJIPANGE.

*Ansbert Ngurumo*
Makamu Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Victoria
14:02:2018
Asante sana mkuu kwa taarifa, hizi ni taarifa za ndani kabisa hazin chembe ya shaka.

Intellijensia yako ni kubwa kuliko ya magufuli.
 
Kiukweli mimi ni kama Tomaso, siiamini taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, lakini hoja hii ya Lissu,

"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.

NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, hivyo hii isijekuwa ni taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!.

Tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.
P
Taarifa za ulinzi na usalama ni siri lakini kilichotajwa hapo sio siri.
 
Mmeanza drama!

Fictional short story mixed with propaganda!

Ukiisoma habari yenyewe utagundua ni habari iliyojaa uwongo ambao kama hutumii fikra pana huwezi kugundua.

Ukiangalia kwa jicho la pili utagundua kuna uwezekano CHADEMA wanataka kufanya maovu au kumteka/kumficha mgombea/wagombea wao ili waseme, mmeona tuliwaambia mapema kuwa haya yatatokea.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wameanza kuwajenga kisaikologia ''makamanda'' katika mipango yao.

Wajumbe aliowataja ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ambayo ni kawaida kukaa ili kutathmini hali ya usalama katika mkoa.

Tokea mwaka 1996 mmnatuambia taifa linaelekea kubaya! huko kubaya ni wapi ambako hatufiki?

Ninajua baada ya uchaguzi mtakuja na nyimbo zilezile za kuibiwa kura.
Unaona kuchelewa kufika huko tunako elekea ? Subili tutafika
 
Unaposema fiction story, hebu nikuulize swali moja tu ndogo, hivi yule Katibu wa Chadema wa Hananasif ambaye alitekwa na watu WASIOJULIKANA na baadaye kuuawa, nayo utaiita ni fiction story??

Nchi inakwenda kubaya sana, kwa kuwa maana ya uchaguzi ni kuchagua mtu anayekubalika katika eneo husika.....

Lakini kwa MAAGIZO toka juu kwa POLISI na NEC kuwa ni LAZIMA atangazwe mshindi wa CCM kwa hali yoyote ile, ama sivyo WATEULE wa Rais wa maeneo husika watapoteza kazi zao, ndilo tunalolisema kuwa nchi inakwenda KUBAYA SANA!

Nimeamini maneno yaliyotolewa na Mbunge wa Kigoma mjini kuwa nchi tumewakabdhi WASHAMBA na MALIMBUKENI!
 
Huyu Ansbert anapaswa KUMPA MSAADA Kamanda MSANGI kwani hayo aliyoyaeleza hasa kuhusu LISSU yanahitaji UFAFANIZI WA KINA, " WALIPANGA KUMUUA" ???
 
Back
Top Bottom