Mbunge Stanslaus Mabula: Lini Serikali Itakamilisha Mchakato wa Kuanzisha Tarafa za Igoma na Mkolani - Nyamagana

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

Mbunge Stanslaus Mabula: Lini Serikali Itakamilisha Mchakato wa Kuanzisha Tarafa za Igoma na Mkolani - Nyamagana

SERIKALI imesema kuwa Mchakato wa kuanzisha tarafa za Igoma na Mkolani Nyamagana ulijadiriwa na kuithinishwa katika ngazi ya Kata, Baraza la madiwani, Kamati ya Ushauri ya Wilaya na baadae katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika tarehe 05/11/2018.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa TAMISEMI alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula alipouliza Je, lini Serikali itakamilisha mchakato wa kuanzisha Tarafa za Igoma na Mkolani - Nyamagana

Aidha amesema kuwa Maombi hayo, yaliwasilishwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa barua ya tarehe 18/03/2019.

"Kwa sasa, Serikali imetoa kipaumbele katika kuboresha na kukamilisha miundombinu kwenye maeneo yakiutawala yaliyopo, ili yaweze kutoa huduma kwa ufanisi zaidi na baadae kuendelea na maeneo mengine kwa kufuata taratibu na vigezo vilivyoainishwa,"

Hivyo, maombi ya kuanzisha Tarafa za Igoma na Mkolani katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza yatafanyiwa kazi na Serikali itakapoanza kuanziasha maeneo mapya ya utawala," amesema.
 

Attachments

  • buuu.jpg
    buuu.jpg
    102.2 KB · Views: 2
Tarafa zilizopo zinatosha, tarafa hazina maana yoyote, sijawahi kusikia mwananchi wa kawaida anamuulizia Afisa Tarafa wao huwa ni VEO/WEO
Mie nilijua wana mpango wa kuzifutilia mbali hizi wilaya na Tarawa,zilizojaa uchafu mwingi, wananchi wanahitaji services delivered, sio utitiri wa mikoa na wilaya, Botswana almost tunalingana kwa ukubwa wa eneo ila wana mikoa 4 tu na population ya less than 4M!,sisi tunazaana kama simbilisi
 
Back
Top Bottom