Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana

Katika hali ya sasa ni vigumu mtu kuibuka na tuhuma nzito kama hizo pasipo kuwa na ushahidi wa kutosha au kuwa na uhakika na unachokisema kwasababu hata wao wakijua unachokisema ni sahihi,wataogopa kukushitaki maana watakuwa na hofu ya wewe kuwalipua mahakamami na zaidi watakuwa na wasiwasi na mtandao mzima uliokupa habari hizo.

Binafsi naamini hii itakuwa ni kazi ya baadhi ya watu waliopokelewa kwa mbwembwe wakidhani wana mapenzi na chama chao kumbe walivutiwa tu na vipande thelathini vya fedha na haya ndio yanaweza kuwa ni matokeo na malipo ya kufanya mambo kwa kukurupuka.

Mabwana hawa si lazima wawepo kwenye kikao husika ila wanaweaza kupokea taarifa kutoka kwa walioshirika katika kikao hicho na wao kuzivujisha maana hawana mapenzi ya dhati na upande uliopo na hivi wako wengi ni vigumu hata kujua nani anaweza kuhusika.

Sitashangaa mipango yao mingi ikaendelea kuvuja kwasababu walifanya kosa la kupokea watu wengi na wote wakawaamini wakasahau watu hawa hawakuhamia huko kwa mapenzi yao bali kwa ushawishi fulani.

Namalizia kwa kusema, "apandacho mtu, ndicho avunacho na damu ni nzito kuliko maji."
Mkuu Salary Slip,
kuna huu msemo, "If you cant beat them, join them", sasa baada ya kushindwa kuwashinda, wamewatuma vijana wao wawajoin!, na kazi ndio imeanza!, sasa kitendo cha wewe kuwasema kuwa hii ndio kazi yao, utawaponza bure, sasa wataishia kibarazani tuu hata sebuleni watakatazwa kuingia ili wasisikie ya chumbani!.

Usiponze watu!.
P.
 
Wala msiwasingizie hao waliohamia, kwani mnafikiri miongoni mwetu wote tunawaza pamoja kama mazombie?
Hata miongoni mwetu kuna migawanyiko mikubwa unatafutwa muda sahihi tu. Katika siasa mkakati ni tafuta taarifa, kamata taarifa, hakiki taarifa , tunza tasrifa na ushahidi juu ya taarifa.
Then relax, subiri muda na wakati sahihi.

Ila rafiki ninaitamani ile Tanzania yenye upendo furaha na amani.Haijalishi ulikuwa mrengo upi mwisho wa siku vita na ahsira vinaishia kwenye mitandao tukifika mtaani ni wamoja.Leo ukiona Mpinzani wako umamkimbia kwa maana hujui kama siyo wale wasiojulikana.

Ni wakati wa kuirudisha ile Tanzania yetu.Hatuihitaji hii Tanzania yangu,tunahitaji Tanzania yetu,hatuihitaji Serikali yangu/Serikali ya CCM au Serikali ya JPM tunaihitaji Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Hayo maneno hata tumbili anayaandika

Teknolojia ya sasa ndio yote

Huyo mchochezi arushe kideo tuwasikie huku tukiwaona na sura zao zote na iambatane na audio pia kivyake.

Yaani chadema wamekuwa alosto kweli kweli..

Kesho mwingine atabeba picha baada ya kumuua mtu akidai kauliwa na chama tawala.. kumbe yeye ndie anahusika kisa kulilia kura kwa kuua wenzao.. ila mwisho wao uje haraka watu wajue maovu yao.. chama bomu kila siku uongo na kusingizia.

Siasa zimewashinda mumegeukia ugaidi sasa.
 
Ila rafiki ninaitamani ile Tanzania yenye upendo furaha na amani.Haijalishi ulikuwa mrengo upi mwisho wa siku vita na ahsira vinaishia kwenye mitandao tukifika mtaani ni wamoja.Leo ukiona Mpinzani wako umamkimbia kwa maana hujui kama siyo wale wasiojulikana.

Ni wakati wa kuirudisha ile Tanzania yetu.Hatuihitaji hii Tanzania yangu,tunahitaji Tanzania yetu,hatuihitaji Serikali yangu/Serikali ya CCM au Serikali ya JPM tunaihitaji Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Tanzania Yetu itarudi tu ila kwa gharama kubwa sana!
 
Tanzania Yetu itarudi tu ila kwa gharama kubwa sana!

Ingeweza kurudi kwa gharama ndogo sana kama WATANZANIA tungekumbuka SHUKA mapema,kwa maana kwamba kuungana ili kuikomboa Tanzania yetu.Leo Mbunge wa CCM anaona RAHA Mbunge mwenzake aumizwe bila ya sababu za msingi
 
hahahahaha kwani Da Mange kasemaje? ukiona chadema wanaanza haya mambo ya story ujue wameona dalili ya kushindwa sasa wana tafuta sababu ,,,,
Kanusha kama ni ya uongo acha kuleta taarabu kama kibajaji wewe mtoto wa kiume unakuwa kama shaka mke wa kiongozi mwenzio huko tanga?
 
"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*".

Hii siamini!.
P
Pascal huamini nini na kinachotokea ni kitu gani??!!! CCM wasipopata upinzani wa nguvu ni waungwana. Tabu ni pale wanapohisi kushindwa ni zaidi ya wanyama!!! Ref uchaguzi ambao cdm walijitoa hawakuwa na neno, tabu ni pale kikiwepo chama kinachotishia uhai wao, hugeuka na kuwa zaidi ya fisi
 
Mkuu Salary Slip,
kuna huu msemo, "If you cant beat them, join them", sasa baada ya kushindwa kuwashinda, wamewatuma vijana wao wawajoin!, na kazi ndio imeanza!, sasa kitendo cha wewe kuwasema kuwa hii ndio kazi yao, utawaponza bure, sasa wataishia kibarazani tuu hata sebuleni watakatazwa kuingia ili wasisikie ya chumbani!.

Usiponze watu!.
P.
Kuna kipindi nilisoma Ngurumo kakimbilia Nairobi aliogopa 'kuuawa'. Amesharudi kutoa maandiko hayo?
 
Anaandika Ansbert Ngurumo

Very important Tip:

CCM na polisi jana usiku kuanzia saa 2:37 walijifungia katika ukumbi wa BoT Mwanza kupanga wizi wa kura.

1. Kikao kilianza saa 2:37
2. Washiriki walikuwa 36.
3. Kiliongozwa na John Mongela, mkuu wa mkoa.
4. Miongoni mwa washiriki ni hawa wafuatao:

1. Mkiti CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athumani

2. Mkuu wa mkoa, John Mongela

3. Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Mary Tesha

4. OCD Nyamagana, Ochieng Aiago

5. OCS wa kituo cha Mirongo, Ayub Khaji

6. Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa

7. Mbunge wa Nyamagana, Stanislaus Mabula

9. Mkiti wa UVCCM Taifa, Heri James

10. RPC wa Mwanza, Ahmed Msangi

Mbunge wa Ilemela (Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Angelina Mabula, HAKUWA KIKAONI

Kinondoni

Walijadili Kinondoni kwa kifupi sana, kwamba:

- Dalili zinaonyesha kuwa Salum Mwalimu atashinda. Hivyo, CCM wameamua kutumia mbinu waliyotumia kwenye Kata za Arumeru mwezi Novemba 2017. Kuzuia au kuondoa mawakala wa UKAWA.

Siha haikujadiliwa kabisa.

Lakini waliambizana kuwa serikali imeamua kufanya chaguzi ndogo kwa awamu ili wapinzani wenye kiherehere wapate fursa ya kukusanyika mahali pamoja, washughulikiwe mmoja mmoja. Kufikia 2020 upinzani utakuwa umekosa watu wa kuuamsha kwa sababu wenye nguvu watakuwa wameondolewa.

Pili, walikiri kwamba mgomo wa Chadema kutoshiriki uchaguzi uliopita umewaonyesha kwamba wapinzani wana nguvu, wanaungwa mkono na umma, kwa kuwa wapigakura walipungua sana.

Kwa hiyo, shabaha ya CCM sasa ni kuwashugulikia kijeshi ili viongozi wa upinzani wapotee.

Tatu, walilaumiana kwamba kuna watu wanapewa majukumu makubwa yanawashinda kukamilisha.

Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa walifanya makosa.

Isamilo, Mwanza

Kuhusu Kata ya Isamilo, wamekiri kwamba mgombea wao hauziki, na kwamba wakazi wengi wa kata hiyo ni washashi (watu wa Mara). Lakini wakasema amri imetoka juu kwamba lazima CCM washinde kwa kuwa kata hiyo ipo eneo na makazi ya mkuu wa mkoa na ndipo Ikulu ndogo inakohamishiwa, na kwamba rais hapendi kuishi kwenye kata inayoongozwa na wapinzani.

Waliazimia yafuatayo:

1. Kuteka mgombea wa Chadema wakati wowote kuanzia sasa, hasa nyakati za asubuhi.

2. Kuanza patrol za polisi usiku ili kukamata vijana wanaodhaniwa kuwa wanaunga mkono Chadema.

3. Kazi ya kuteka mgombea imekabidhiwa kwa mtu anaitwa Banny, mkazi wa Lucherere, ambaye sasa amepewa makazi ya muda katika kata hiyo, akiwa mgeni wa aliyekuwa mwenyekiti wa Kata ya Nyakabungo, ambaye sasa hivi ana uongozi katika ngazi ya kata.

4. Usiku wa tarehe 16 kuamkia 17, polisi na green guard watafanya doria maalumu kwa ajili ya kukamata wana Chadema na kuwatisha.

Magari matatu yamepangwa kutumika - Noah, na Landcruiser mbili.

Moja itakuwa maeneo ya Kwa Malisa, katika mpaka wa Nyamanoro na Isamilo. Nyingine itakuwa gengeni kwa Wahema. Nyingine itakaa kwenye makutano ya Isamilo na Thaqafa.

5. Noah itatumiwa kubeba sukari na sabuni kwa ajili ya kuhonga wapigakura (kipande cha sh. 300 na robo kilo ya sukari sh.650).

6. Land cruiser moja itabeba green guard ili kukamata watu wa Chadema watakaokuwa kwenye patrol usiku. Magari hayo yataegeshwa kwa Wahema na Mikoroshini.

7. Siku ya kupiga kura, green guard, ambao katika mikutano ya mgombea wamekuwa wanajitokeza kama wasanii, ndio watatumika kutisha, kupiga na kuzuia watu njiani wanaokwenda kupiga kura.

Kikundi hiki kinafadhiliwa na mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula. Na jana alitoa taarifa kikaoni kuwa kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya posho, lakini sasa amefaulu kuimaliza.

INFORMATION IS POWER. TUJIPANGE.

Ansbert Ngurumo
Makamu Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Victoria
14.02.2018
Nchi imefikia patamu sana !
 
Hii ngumu sana. Ni ishu nzito. Wahusika wameshtukizwa na ukweli huu. Huko Mwz ni mtafutano na mtafunano saivi..
 
Kiukweli mimi ni kama Tomaso, siiamini taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, lakini hoja hii ya Lissu,

"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.

Sababu ya kutoiamini kauli hii ni kwa sababu inabeba criminal liability za aina mbili
Accessories After The Fact: Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, Jeshi letu la polisi limeshindwa kufanya chochote kwa sababu limekosa pa kuanzia baada ya kukosa shuhuda yoyote wa kumuhoji, na kuna camera za CCTV zilirekodi, zimetoweka, hivyo hakuna kabisa pa kuanzia uchunguzi!.

Kumbe kuna watu wamejifungia katika ukumbi wa BOT Mwanza akiwemo RC na RPC ambao ndio walihusika na shambulio lile!.They are all, accessories after the fact, wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa kuhusu sambulio la Lissu!.

Kwa vile RPC nae ni mhusika, hivyo hakuna mahali pa kuanzia, ila naamini kwa vile Mwigulu ni member wetu humu, atawatuma vijana wake wakawahoji wahusika waliotajwa, tena nawaomba wasimsumbue kabisa Ngurumo kumtaja source wake, kama ameitoa taarifa hii kwa kofia yake ya uandishi wa habari, kwa sababu sisi waandishi tuna kinga ya kihabari ya "the confidentiality of the source".

Kama ameitoa kama Makamo Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa, alipaswa kesho yake kuondoka Mwanza kwa ndege ya kwanza na kufikia mezani kwa Mwigulu, kisha kwenda mezani kwa Kipilimba kuripoti, halafu ndipo ailete humu!.

Criminal liability ya aina ya pili, ni accessories before the fact, ambapo watu wakubwa, wazito wa mkoa wamekutana kupanga kufanya jinai!.
Any good citizen akisikia ni wajibu wake kuripoti, kwa vile RC na RPC ni wahusika, waliosikia wakaripoti kwa Ngurumo, kwa vile Ngurumo sio Mlinzi wa Amani, tariffs hiyo ni very sensitive ilibidi Ngurumo amuongoze mtoa taarifa wake kwa mlinzi wa amani, Waziri aelezwe, IGP aelezwe, na Amiri Jeshi aelezwe, ili wahalifu hawa, watiwe mbaroni haraka kabla hawajatekeleza jinai hii!.

NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, ambao wana mamlaka ya kumkaribisha mtu yoyote kwenye kikao chao hata kama sio mjumbe. Hivyo hii isijekuwa ni leakage ya taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mila, imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!. Hivyo this leaves much to be desired, kumbe hizi ndizo kazi za kamati zetu za ulinzi na usalama za mikoa!. Nimemkumbuka Kamanda Mawazo!' RIP Kamanda Alphonce Mawazo, damu yako haitapotea bure, sasa imeanza kuchemka na kuibua madudu yanayofanyikaga!.

Ila pia sisi raia wema wa nchi hii, tufanye responsible blogging kwa self censorship ya sensitive info, tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, nyingine ni political capitalization tuu!, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.
P
Kuhusu madudu ya Kamati za Ulinzi na Usalama, nimeyazungumza hapa

TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!

Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Paskali
Hivi Mayalla pamoja na kijielimu mbuzi ulichonacho unadhani kuna mjinga yeyote humu JF unayeweza kumpotosha ? Kama wapo si kwenye jukwaa hili.

Unaandika as if ni binadamu asiye na aibu kabisa , yaani ni kama msela wa Tandika aliyevuta puli mbili za bangi , ni kitu gani usichokijua kuhusu shambulio la Lissu ? Yaani kweli mtu mzima bila aibu unaleta uongo hapa ? Huna wazazi wakukanye ? Ni bora usiandike chochote kuhusu Lissu utaheshimiwa .
 
Hii si habari mpya,ndiko nchi ilipofikia.

Wakuu wa mikoa zamani tulifikiri wanakazi kubwa ya kusukuma gurudumu la maendeleo katika mikoa yao lakini siku hizi kazi kubwa imekuwa kuratibu manunuzi ya wapinzani na kuiponda ponda demokrasia.

Muda ni mwalimu muzuri sana yetu macho na masikio.
 
Hii si habari mpya,ndiko nchi ilipofikia.

Wakuu wa mikoa zamani tulifikiri wanakazi kubwa ya kusukuma gurudumu la maendeleo katika mikoa yao lakini siku hizi kazi kubwa imekuwa kuratibu manunuzi ya wapinzani na kuiponda ponda demokrasia.

Muda ni mwalimu muzuri sana yetu macho na masikio.
Pascal Mayalla haamini jambo hili , bila shaka atakuwa karogwa au yeye mwenyewe ni mchawi .
 
Back
Top Bottom