Chizi Jambazi
JF-Expert Member
- Sep 22, 2017
- 1,869
- 1,470
Nikitaka kupata vichekesho vingine kama hiki nafanyaje?
Lala kifudifudi.Nikitaka kupata vichekesho vingine kama hiki nafanyaje?
Well saidinteluginccia koko ya chadema isiyojua
Diwani yupi au mbunge yupi atahama oya oya oya mzushi at work hamjui yenu ndio mtayajua ya CCM?
Niliwahi kusema kauli huumba, sasa kauli hii inatimia!, taifa tunaelekea kubaya!.Kiukweli mimi ni kama Tomaso, siiamini taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, lakini hoja hii ya Lissu,
"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa walifanya makosa.", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.
Sababu ya kutoiamini kauli hii ni kwa sababu inabeba criminal liability za aina mbili
Accessories After The Fact: Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, Jeshi letu la polisi limeshindwa kufanya chochote kwa sababu limekosa pa kuanzia baada ya kukosa shuhuda yoyote wa kumuhoji, na kuna camera za CCTV zilirekodi, zimetoweka, hivyo hakuna kabisa pa kuanzia uchunguzi!.
Kumbe kuna watu wamejifungia katika ukumbi wa BOT Mwanza akiwemo RC na RPC ambao ndio walihusika na shambulio lile!.They are all, accessories after the fact, wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa kuhusu sambulio la Lissu!.
Kwa vile RPC nae ni mhusika, hivyo hakuna mahali pa kuanzia, ila naamini kwa vile Mwigulu ni member wetu humu, atawatuma vijana wake wakawahoji wahusika waliotajwa, tena nawaomba wasimsumbue kabisa Ngurumo kumtaja source wake, kama ameitoa taarifa hii kwa kofia yake ya uandishi wa habari, kwa sababu sisi waandishi tuna kinga ya kihabari ya "the confidentiality of the source".
Kama ameitoa kama Makamo Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa, alipaswa kesho yake kuondoka Mwanza kwa ndege ya kwanza na kufikia mezani kwa Mwigulu, kisha kwenda mezani kwa Kipilimba kuripoti, halafu ndipo ailete humu!.
Criminal liability ya aina ya pili, ni accessories before the fact, ambapo watu wakubwa, wazito wa mkoa wamekutana kupanga kufanya jinai!.
Any good citizen akisikia ni wajibu wake kuripoti, kwa vile RC na RPC ni wahusika, waliosikia wakaripoti kwa Ngurumo, kwa vile Ngurumo sio Mlinzi wa Amani, tariffs hiyo ni very sensitive ilibidi Ngurumo amuongoze mtoa taarifa wake kwa mlinzi wa amani, Waziri aelezwe, IGP aelezwe, na Amiri Jeshi aelezwe, ili wahalifu hawa, watiwe mbaroni haraka kabla hawajatekeleza jinai hii!.
NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, ambao wana mamlaka ya kumkaribisha mtu yoyote kwenye kikao chao hata kama sio mjumbe. Hivyo hii isijekuwa ni leakage ya taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mila, imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!. Hivyo this leaves much to be desired, kumbe hizi ndizo kazi za kamati zetu za ulinzi na usalama za mikoa!. Nimemkumbuka Kamanda Mawazo!' RIP Kamanda Alphonce Mawazo, damu yako haitapotea bure, sasa imeanza kuchemka na kuibua madudu yanayofanyikaga!.
Ila pia sisi raia wema wa nchi hii, tufanye responsible blogging kwa self censorship ya sensitive info, tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, nyingine ni political capitalization tuu!, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.
P
Kuhusu madudu ya Kamati za Ulinzi na Usalama, nimeyazungumza hapa
TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!
Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
Paskali
😆 😆 😆 hebu acha kutuchekesha mkuuNiliwahi kusema kauli huumba, sasa kauli hii inatimia!, taifa tunaelekea kubaya!.
Hili tukio la kifo cha huyu mzee, kwa mujibu wa taarifa za tukio lenyewe, mimi nimejiridhisha wahusika sio watu wasiojulikana, ni 'wasiojulikana'
Nashauri kwa negligence iliyofanywa na Jeshi letu la polisi kuhusu kadhia hii ya kifo cha Mzee Ali Mohamed Kibao, Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu , kukutwa ameuwawa na watu 'wasiojulikana' na mwili wake kutupwa eneo la Kunduchi Ununio, kwa kuanzia nashauri watu wwanne hawa wawajibike!.
1. Waziri - kwa ajali kazini
2. IGP - kwa negligence ya RPC wake
3. RPC -DSM - negligence
4. OCD Kinondoni - negligence, na hawa wawili wa mwisho RPC na OCD wanaweza kufikishwa kwa Pilato!.
Ni wakati sasa Rais Samia kukasirika kama enzi za Nyerere!.
P