Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana

Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana

Sesimba

Senior Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
189
Reaction score
383
Anaandika Ansbert Ngurumo

Very important Tip:

CCM na polisi jana usiku kuanzia saa 2:37 walijifungia katika ukumbi wa BoT Mwanza kupanga wizi wa kura.

1. Kikao kilianza saa 2:37
2. Washiriki walikuwa 36.
3. Kiliongozwa na John Mongela, mkuu wa mkoa.
4. Miongoni mwa washiriki ni hawa wafuatao:

1. Mkiti CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athumani

2. Mkuu wa mkoa, John Mongela

3. Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Mary Tesha

4. OCD Nyamagana, Ochieng Aiago

5. OCS wa kituo cha Mirongo, Ayub Khaji

6. Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa

7. Mbunge wa Nyamagana, Stanislaus Mabula

9. Mkiti wa UVCCM Taifa, Heri James

10. RPC wa Mwanza, Ahmed Msangi

Mbunge wa Ilemela (Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Angelina Mabula, HAKUWA KIKAONI

Kinondoni

Walijadili Kinondoni kwa kifupi sana, kwamba:

- Dalili zinaonyesha kuwa Salum Mwalimu atashinda. Hivyo, CCM wameamua kutumia mbinu waliyotumia kwenye Kata za Arumeru mwezi Novemba 2017. Kuzuia au kuondoa mawakala wa UKAWA.

Siha haikujadiliwa kabisa.

Lakini waliambizana kuwa serikali imeamua kufanya chaguzi ndogo kwa awamu ili wapinzani wenye kiherehere wapate fursa ya kukusanyika mahali pamoja, washughulikiwe mmoja mmoja. Kufikia 2020 upinzani utakuwa umekosa watu wa kuuamsha kwa sababu wenye nguvu watakuwa wameondolewa.

Pili, walikiri kwamba mgomo wa Chadema kutoshiriki uchaguzi uliopita umewaonyesha kwamba wapinzani wana nguvu, wanaungwa mkono na umma, kwa kuwa wapigakura walipungua sana.

Kwa hiyo, shabaha ya CCM sasa ni kuwashugulikia kijeshi ili viongozi wa upinzani wapotee.

Tatu, walilaumiana kwamba kuna watu wanapewa majukumu makubwa yanawashinda kukamilisha.

Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa walifanya makosa.

Isamilo, Mwanza

Kuhusu Kata ya Isamilo, wamekiri kwamba mgombea wao hauziki, na kwamba wakazi wengi wa kata hiyo ni washashi (watu wa Mara). Lakini wakasema amri imetoka juu kwamba lazima CCM washinde kwa kuwa kata hiyo ipo eneo na makazi ya mkuu wa mkoa na ndipo Ikulu ndogo inakohamishiwa, na kwamba rais hapendi kuishi kwenye kata inayoongozwa na wapinzani.

Waliazimia yafuatayo:

1. Kuteka mgombea wa Chadema wakati wowote kuanzia sasa, hasa nyakati za asubuhi.

2. Kuanza patrol za polisi usiku ili kukamata vijana wanaodhaniwa kuwa wanaunga mkono Chadema.

3. Kazi ya kuteka mgombea imekabidhiwa kwa mtu anaitwa Banny, mkazi wa Lucherere, ambaye sasa amepewa makazi ya muda katika kata hiyo, akiwa mgeni wa aliyekuwa mwenyekiti wa Kata ya Nyakabungo, ambaye sasa hivi ana uongozi katika ngazi ya kata.

4. Usiku wa tarehe 16 kuamkia 17, polisi na green guard watafanya doria maalumu kwa ajili ya kukamata wana Chadema na kuwatisha.

Magari matatu yamepangwa kutumika - Noah, na Landcruiser mbili.

Moja itakuwa maeneo ya Kwa Malisa, katika mpaka wa Nyamanoro na Isamilo. Nyingine itakuwa gengeni kwa Wahema. Nyingine itakaa kwenye makutano ya Isamilo na Thaqafa.

5. Noah itatumiwa kubeba sukari na sabuni kwa ajili ya kuhonga wapigakura (kipande cha sh. 300 na robo kilo ya sukari sh.650).

6. Land cruiser moja itabeba green guard ili kukamata watu wa Chadema watakaokuwa kwenye patrol usiku. Magari hayo yataegeshwa kwa Wahema na Mikoroshini.

7. Siku ya kupiga kura, green guard, ambao katika mikutano ya mgombea wamekuwa wanajitokeza kama wasanii, ndio watatumika kutisha, kupiga na kuzuia watu njiani wanaokwenda kupiga kura.

Kikundi hiki kinafadhiliwa na mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula. Na jana alitoa taarifa kikaoni kuwa kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya posho, lakini sasa amefaulu kuimaliza.

INFORMATION IS POWER. TUJIPANGE.

Ansbert Ngurumo
Makamu Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Victoria
14.02.2018
 
Mmeanza drama!

Fictional short story mixed with propaganda!

Ukiisoma habari yenyewe utagundua ni habari iliyojaa uwongo ambao kama hutumii fikra pana huwezi kugundua.

Ukiangalia kwa jicho la pili utagundua kuna uwezekano CHADEMA wanataka kufanya maovu au kumteka/kumficha mgombea/wagombea wao ili waseme, mmeona tuliwaambia mapema kuwa haya yatatokea.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wameanza kuwajenga kisaikologia ''makamanda'' katika mipango yao.

Wajumbe aliowataja ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ambayo ni kawaida kukaa ili kutathmini hali ya usalama katika mkoa.

Tokea mwaka 1996 mmnatuambia taifa linaelekea kubaya! huko kubaya ni wapi ambako hatufiki?

Ninajua baada ya uchaguzi mtakuja na nyimbo zilezile za kuibiwa kura.
 
Kiukweli mimi ni kama Tomaso, siiamini taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, lakini hoja hii ya Lissu,

"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.

Sababu ya kutoiamini kauli hii ni kwa sababu inabeba criminal liability za aina mbili
Accessories After The Fact: Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, Jeshi letu la polisi limeshindwa kufanya chochote kwa sababu limekosa pa kuanzia baada ya kukosa shuhuda yoyote wa kumuhoji, na kuna camera za CCTV zilirekodi, zimetoweka, hivyo hakuna kabisa pa kuanzia uchunguzi!.

Kumbe kuna watu wamejifungia katika ukumbi wa BOT Mwanza akiwemo RC na RPC ambao ndio walihusika na shambulio lile!.They are all, accessories after the fact, wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa kuhusu sambulio la Lissu!.

Kwa vile RPC nae ni mhusika, hivyo hakuna mahali pa kuanzia, ila naamini kwa vile Mwigulu ni member wetu humu, atawatuma vijana wake wakawahoji wahusika waliotajwa, tena nawaomba wasimsumbue kabisa Ngurumo kumtaja source wake, kama ameitoa taarifa hii kwa kofia yake ya uandishi wa habari, kwa sababu sisi waandishi tuna kinga ya kihabari ya "the confidentiality of the source".

Kama ameitoa kama Makamo Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa, alipaswa kesho yake kuondoka Mwanza kwa ndege ya kwanza na kufikia mezani kwa Mwigulu, kisha kwenda mezani kwa Kipilimba kuripoti, halafu ndipo ailete humu!.

Criminal liability ya aina ya pili, ni accessories before the fact, ambapo watu wakubwa, wazito wa mkoa wamekutana kupanga kufanya jinai!.
Any good citizen akisikia ni wajibu wake kuripoti, kwa vile RC na RPC ni wahusika, waliosikia wakaripoti kwa Ngurumo, kwa vile Ngurumo sio Mlinzi wa Amani, tariffs hiyo ni very sensitive ilibidi Ngurumo amuongoze mtoa taarifa wake kwa mlinzi wa amani, Waziri aelezwe, IGP aelezwe, na Amiri Jeshi aelezwe, ili wahalifu hawa, watiwe mbaroni haraka kabla hawajatekeleza jinai hii!.

NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, ambao wana mamlaka ya kumkaribisha mtu yoyote kwenye kikao chao hata kama sio mjumbe. Hivyo hii isijekuwa ni leakage ya taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mila, imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!. Hivyo this leaves much to be desired, kumbe hizi ndizo kazi za kamati zetu za ulinzi na usalama za mikoa!. Nimemkumbuka Kamanda Mawazo!' RIP Kamanda Alphonce Mawazo, damu yako haitapotea bure, sasa imeanza kuchemka na kuibua madudu yanayofanyikaga!.

Ila pia sisi raia wema wa nchi hii, tufanye responsible blogging kwa self censorship ya sensitive info, tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, nyingine ni political capitalization tuu!, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.
P
Kuhusu madudu ya Kamati za Ulinzi na Usalama, nimeyazungumza hapa

TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!

Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Paskali
 
Hivi Leo pale kanisani aliposali mh,rais mapdri wametoa mahubiri gani?
Maana kuna watu wanakufa mitaani Kwa kuuwawa kama kuku

Kwanini hao wanaouwawa wasiretaliate???

dawa ya moto ni moto , hao watekaji wanajulikana kwanini wasivamiwe nao
 
Hayo maneno hata tumbili anayaandika

Teknolojia ya sasa ndio yote

Huyo mchochezi arushe kideo tuwasikie huku tukiwaona na sura zao zote na iambatane na audio pia kivyake.

Yaani chadema wamekuwa alosto kweli kweli..

Kesho mwingine atabeba picha baada ya kumuua mtu akidai kauliwa na chama tawala.. kumbe yeye ndie anahusika kisa kulilia kura kwa kuua wenzao.. ila mwisho wao uje haraka watu wajue maovu yao.. chama bomu kila siku uongo na kusingizia.
 
Mnatafuta kiki ya kudanganyia watu mkishindwa eeh. CHADEMA mko vizuri. Asiye kubali kushindwa si mshindani
 
Usipofuata sheria wewe ndio utakayeenda pabaya...kamwe Taifa haliwezi kwenda pabaya
 
Nachokisoma kinatokea Tanzania yangu hii hii au nimekosea ? " Watu wanapewa majukumu makubwa yanawashinda kukamilisha wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lisu (Dodoma) na mgombea Muleba kwamba walipaswa kufa "

Naona hii amani tuliyonayo tumeichoka haya endeleeni tu kuna siku watu watagawana fito
 
Ule mgogoro wa Mbeya uliopelekea Sugu aachiwe ulitakiwa usambae na maeneo mengine.

Labda kuna kitu wangejifunza.
 
ipo siku nchi hii itatumbukia kwenye umwagaji wa damu.
 

Attachments

  • CCM.jpg
    CCM.jpg
    3.8 KB · Views: 83
inteluginccia koko ya chadema isiyojua
Diwani yupi au mbunge yupi atahama oya oya oya mzushi at work hamjui yenu ndio mtayajua ya CCM?
 
Back
Top Bottom