Ansbert Ngurumo: Taifa linaelekea pabaya sana

Hii nchi katika mwendo inaokwenda nao wa serikali ya awamu ya 5 siyo ile aliotuachia Mwalimu Nyerere, ambayo alituachia Umoja wa hali ya juu bila kujali itikadi ya kisiasa au dini aliyonayo mtu Fulani.

Lakini hii SERA ya Bwana Mkubwa ya kuwaona wapinzani kama WAHAINI, wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatamka wazi kuwa nchi hii itakuwa ya mfumo wa vyama vingi, hakika Mkuu wa nchi anaipeleka kubaya sana nchi hii!!!
 
Opposition wataoppose everything na kupropose nothing
Nimeuliza swali moja tu la misingi, hivi yule kada wa Chadema wa Hananasif jijini Dar ambaye siku chache zilizopita alitekwa na watu WASIOJULIKANA na baadaye mwili wake kukutwa amekufa, nayo ni fiction story??
 
Naona kamanda Ngurumo naye anajitafutia Kiki kwa nguvu sana. Ni afadhali angeitafuta kwa kujenga hoja badala ya kutumia udaku.
 
Chadema wanawekana sawa kisaikolojia.
Ubunge wa kinondoni unajadiliwa mwanza!
 
Naona kamanda Ngurumo naye anajitafutia Kiki kwa nguvu sana. Ni afadhali angeitafuta kwa kujenga hoja badala ya kutumia udaku.
Anatafuta kiki ipi??

Kwani kule jijini Dar yule kada wa Chadema hajafa katika misingi ya kisiasa??
 
hahahahaha kwani Da Mange kasemaje? ukiona chadema wanaanza haya mambo ya story ujue wameona dalili ya kushindwa sasa wana tafuta sababu ,,,,

Na ukiona maimamu wanatoweka kule Zanzibar tujuwe ndio dalili ya kushinda CCM??
 
Anaandika Ansbert Ngurumo

*Very important Tip:*

CCM na polisi jana usiku kuanzia saa 2:37 walijifungia katika ukumbi wa BoT Mwanza kupanga wizi wa kura.

1. Kikao kilianza saa 2:37
2. Washiriki walikuwa 36.
3. Kiliongozwa na John Mongela, mkuu wa mkoa.
4. Miongoni mwa washiriki ni hawa wafuatao:

1. Mkiti CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athumani

2. Mkuu wa mkoa, John Mongela

3. Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Mary Tesha

4. OCD Nyamagana, Ochieng Aiago

5. OCS wa kituo cha Mirongo, Ayub Khaji

6. Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa

7. Mbunge wa Nyamagana, Stanislaus Mabula

9. Mkiti wa UVCCM Taifa, Heri James

10. RPC wa Mwanza, Ahmed Msangi

Mbunge wa Ilemela (Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Angelina Mabula, *HAKUWA KIKAONI*

*Kinondoni*

Walijadili Kinondoni kwa kifupi sana, kwamba:

- Dalili zinaonyesha kuwa Salum Mwalimu atashinda. Hivyo, CCM wameamua kutumia mbinu waliyotumia kwenye Kata za Arumeru mwezi Novemba 2017. Kuzuia au kuondoa mawakala wa UKAWA.

*Siha* haikujadiliwa kabisa.

Lakini waliambizana kuwa serikali imeamua kufanya chaguzi ndogo kwa awamu ili wapinzani wenye kiherehere wapate fursa ya kukusanyika mahali pamoja, washughulikiwe mmoja mmoja. Kufikia 2020 upinzani utakuwa umekosa watu wa kuuamsha kwa sababu wenye nguvu watakuwa wameondolewa.

Pili, walikiri kwamba mgomo wa Chadema kutoshiriki uchaguzi uliopita umewaonyesha kwamba wapinzani wana nguvu, wanaungwa mkono na umma, kwa kuwa wapigakura walipungua sana.

Kwa hiyo, shabaha ya CCM sasa ni kuwashugulikia kijeshi ili viongozi wa upinzani wapotee.

Tatu, walilaumiana kwamba kuna watu wanapewa majukumu makubwa yanawashinda kukamilisha.

Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*

*Isamilo,* Mwanza

Kuhusu Kata ya Isamilo, wamekiri kwamba mgombea wao hauziki, na kwamba wakazi wengi wa kata hiyo ni washashi (watu wa Mara). Lakini wakasema amri imetoka juu kwamba lazima CCM washinde kwa kuwa kata hiyo ipo eneo na makazi ya mkuu wa mkoa na ndipo Ikulu ndogo inakohamishiwa, na kwamba rais hapendi kuishi kwenye kata inayoongozwa na wapinzani.

Waliazimia yafuatayo:

1. Kuteka mgombea wa Chadema wakati wowote kuanzia sasa, hasa nyakati za asubuhi.
2. Kuanza patrol za polisi usiku ili kukamata vijana wanaodhaniwa kuwa wanaunga mkono Chadema.
3. Kazi ya kuteka mgombea imekabidhiwa kwa mtu anaitwa Banny, mkazi wa Lucherere, ambaye sasa amepewa makazi ya muda katika kata hiyo, akiwa mgeni wa aliyekuwa mwenyekiti wa Kata ya Nyakabungo, ambaye sasa hivi ana uongozi katika ngazi ya kata.
4. Usiku wa tarehe 16 kuamkia 17, polisi na green guard watafanya doria maalumu kwa ajili ya kukamata wana Chadema na kuwatisha.

Magari matatu yamepangwa kutumika - Noah, na Landcruiser mbili.

Moja itakuwa maeneo ya *Kwa Malisa,* katika mpaka wa Nyamanoro na Isamilo. Nyingine itakuwa gengeni kwa Wahema. Nyingine itakaa kwenye makutano ya Isamilo na Thaqafa.

5. Noah itatumiwa kubeba sukari na sabuni kwa ajili ya kuhonga wapigakura (kipande cha sh. 300 na robo kilo ya sukari sh.650).

6. Land cruiser moja itabeba green guard ili kukamata watu wa Chadema watakaokuwa kwenye patrol usiku. Magari hayo yataegeshwa kwa Wahema na Mikoroshini.

7. Siku ya kupiga kura, green guard, ambao katika mikutano ya mgombea wamekuwa wanajitokeza kama wasanii, ndio watatumika kutisha, kupiga na kuzuia watu njiani wanaokwenda kupiga kura.

Kikundi hiki kinafadhiliwa na mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula. Na jana alitoa taarifa kikaoni kuwa kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya posho, lakini sasa amefaulu kuimaliza.

INFORMATION IS POWER. TUJIPANGE.

*Ansbert Ngurumo*
Makamu Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Victoria
14:02:2018

Kama haya yana ukweli, ni aibu aibu tena aibu sisi kujiita nchi ya demokrasia!! Tunatofautishaje ccm na ugaidi? Siku zote uwepo wa vyama vyingi ni chachu ya maendeleo, hapa kwetu imekua tofauti kabisa!
 
Haya yote yanatokea ndani ya utawala wa demokrasia! Viongozi wetu jana walikua makanisan wanapaka majivu, huku wakibariki haya yote!
 
Kiukweli mimi ni kama Tomaso, siiamini taarifa hii yote hivi hivi ilivyo. Kuna maeneo nakubaliana na Ngurumo, lakini hoja hii ya Lissu,

"Wakatoa mfano wa shambulizi dhidi ya Lissu (Dodoma) na mgombea wa Muleba; kwamba walipaswa kufa, lakini waliotumwa *walifanya makosa.*", sorry jamani siiamini kabisa kuwa hiki kilijadiliwa, kwa sababu siamini hawa watu wanaweza kuwa vichaa hivi!.

NB, karibu wote waliotajwa ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama, hivyo hii isijekuwa ni taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama imeleak kwa Ngurumo, naye kaileta JF, taarifa za kamati ya ulinzi na usalama ni siri!.

Tuwe makini na waangalifu sana na hizi taarifa za wanasiasa, tusije tukalishwa matango pori na kuingizwa ...cha kike!.
P

Paskal pamoja na shaka uliyo nayo, ila haya yanaweza pia kutokea.
 
Ninaposoma hii story majihisi machozi kunitoka, japo inaweza kuwa ya kutunga.

Una dhani kwa nini mimi nisiiamini hii story? Tunaona watu wanauwawa, tuna ona chaguzi zilizopita namna watu walivyofanyiwa, bado kiongozi anaweza kisimama hadharani bila woga wala aibu anatamka mambo ambayo labda yangezungumzwa chini ya uvungu wa kitanda, yeye anayasema hadharani kweupe mchana.

Hawa wenzetu wamekuwa wanyama, sio watu kama unavyoweza kuwafikilia. Kwa yanayoendelea mimi ninashawishika hayo maneno ni yakweli hakuna hata moja la uongo.
 
Aisee kungekuwa kuna mipango mizuri namna hii katika kuhakikisha uchumi wetu na Tanzania ya viwanda inafikiwa tungekuwa mbali sana.

Yote ya yote bado tuko katika Giza nene.
 
Hivi Leo pale kanisani aliposali mh,rais mapdri wametoa mahubiri gani?
Maana kuna watu wanakufa mitaani Kwa kuuwawa kama kuku
Pale alikuwepo padri? Au kwako wewe kila mvaa joho ni padri? Angalia sana, aliekuwepo pale ni mpinga kristo, kwake yeye damu ikimwagika ndio kafara!!!
 
Mmeanza drama!

Fictional short story mixed with propaganda!

Ukiisoma habari yenyewe utagundua ni habari iliyojaa uwongo ambao kama hutumii fikra pana huwezi kugundua.

Ukiangalia kwa jicho la pili utagundua kuna uwezekano CHADEMA wanataka kufanya maovu au kumteka/kumficha mgombea/wagombea wao ili waseme, mmeona tuliwaambia mapema kuwa haya yatatokea.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wameanza kuwajenga kisaikologia ''makamanda'' katika mipango yao.

Wajumbe aliowataja ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ambayo ni kawaida kukaa ili kutathmini hali ya usalama katika mkoa.

Tokea mwaka 1996 mmnatuambia taifa linaelekea kubaya! huko kubaya ni wapi ambako hatufiki?

Ninajua baada ya uchaguzi mtakuja na nyimbo zilezile za kuibiwa kura.
Kumbe lipo pazuri? Duh!
 
Si mjitoe tu mnaangaika nini sasa? Au mnapenda kuuwawa na kutekwa?
Hata Mimi nakuunga mkono. Ccm kwa sasa wako tayari mtu afe lakini wajitangaze wanapendwa. Kuendelea kuona watu wanakufa kwa kisingizio cha demokrasia ni kushiriki mauaji kwa mlango wa nyuma. Hivi kata zote zikiongozwa na ccm yatatokea mabadiliko gani ya kushangaza yatakayokuwa na faida zaidi ya maisha ya watu?
 
Hiki chama bila police kilishajifiaga zamani mno, police ni kama mashine yao ya kupumulia .
 
Back
Top Bottom