Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
Ninakuunga mkono. Pia ni kama nilitabiri. Mama yetu keshachagua ua jingine la kurukia. Je, hapa jukwaani ataendelea kuwepo kama hapo awali,ili tutekeleze kwa mtizamo uleule wa awali hoja hii? Is she not just an opportunist of unknowns?Ni kweli kipindi cha mwalimu yalifanyika hayo unayosema, tena kwa mafanikio makubwa sana. Ukiangalia hali ya sasa kiujumla, kuna maswali mengi unatakiwa ujiulize kabla ya kulinganisha maisha ya sasa na ya kipindi cha mwalimu. Je, vipi uwiano wa rasimali na idadi ya watuukoje? hali ya hewa ikoje? tulikuwa na mashirika mangapi ya umma yaliyokuwa hai na yenye tija kwenye uchumi? (Kumbuka kuwa Tanzania ilikuwa ya pili Afrika nyuma ya Msumbiji (1000)kwa kuwa na mashirika ya umma 400 ambayo yalikuwa productive in 1980s); Je, sera za biashara za kimataifa zikoje kwa sasa tofauti na kipindi cha mwalimu? Vipi kuhusu sera na sheria tulizo nazo juu ya usimamizi wa rasimali zetu?
Ni ukweli usiopingika kuwa tulipaswa kuwa pazuri zaidi, ila tumekwamishwa na mipango yetu isiyothibitika na kudumu hata kuona matunda yake, pia sheria, sera, na mikataba yetu/zetu ni kitanzi kingine kwa maendeleo ya taifa letu.