Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua | Page 13 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anna Mghwira, Feb 22, 2017.

 1. Anna Mghwira

  Anna Mghwira Verified User

  #1
  Feb 22, 2017
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 203
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 80
  Ninaikumbuka vema kauli ya mama Salma Kikwete kuwa nanukuu: " Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako." Leo watoto wa wenzetu wameingia tatizo la kukosa mikopo ya elimu ya juu; tuwasaidie kama watoto wetu.

  Ninapenda kuwaomba akina mama wote nikianza na Mhe mama Salma Kikwete aliyeasisi usemi na hatua hii, tushirikiane kunusuru maisha ya elimu ya watoto walioko vyuoni wenye sifa ya kuwa na mikopo lakini hawakufanikiwa kupata mkopo. Tuwahamasishe vijana waliobakia mitaani na majumbani kujiunga na vyuo vikuu kuanua akili zao changa kukidhi ushindani wa sasa kimaisha.

  Naomba akina mama wote viongozi, wazazi, walezi, wafanya bishara, waajiriwa, wanaharakati bila kujali itikadi zetu za aina yoyote tusimame kama wanawake wazazi wenye nia kuejnga taifa la watu walioelimika tuunde mfuko wa kuwasiadia watoto wetu wafanikiwe kumaliza masomo yao kwa ujenzi wa taifa letu.

  Nikitoka na mama Kikwete ninaomba wake za marais wote waliopita kuanzia na mama Karume (mzee marehemu na Rais aliyemaliza mda wake) mpaka mama Janet Magufuli anayenivutia sana kwa kuonesha moyo wa amani sana kwa taifa letu.

  Baada ya hao nimuombe mama Anna Makinda na wabunge wanawake wote waliopo na waliomaliza tangu uhuru wa nchi yetu tuungane kumsaidia kila mtoto wa Tanzania mwenye uwezo wa kusoma asome.

  Kisha kwa niaba ya wanawake wafanya bishara niombe kitengo cha wanawake cha TCCIA, Baraza la Biashara la wanawake...tukubali wito huu: Tuungane kama wazazi na walezi chini ya kauli mbiu: Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako...tuunde mfuko wa elimu kwa ajili ya vijana wetu.

  Niombe vyama vya wana-taaaluma: waalimu, madaktari, wahandisi, watumishi wa umma, mabenki, makampuni yote ya ndani na ya kigeni, asasi za kiraia za ndni na za kimataifa, balozi zetu zote, tuungane kuunda chombo hiki kuwasaidia vijana wetu.

  Nimeguswa sana na mahangaiko ya vijana wa vyuo vikuu. Ninawashukuru wachache waliofika kwangu kueleza changamoto zao. Mmenihamasisha kuchangia kidogo elimu yenu lakini ninaomba hili liwe suala la kitaifa.

  Ninaomba wanawake wenzangu popote tulipo tuwasiliane tuunde umoja huu kuwaimarisha na kuwapa tumaini vijana na janga la kukosa elimu ya juu kama wana sifa za kuipata.

  Tuweke kando siasa, dini, kabila, ukanda ama aina yoyote ya kigezo kufanikisha jambo hili. Ninawashukru sana. Kesho kuna wanafunzi watashindwa kufanya mitihani kwa kukosa ada kidogo tu ya laki kuanzia 5-8. Mfuko wa mama Salma, Mfuko wa mama Mkapa wa Fursa sawa kwa wote, Taasisi ya Benjamini mkapa, Taasisi ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na zingine, tusaidiane kukamilisha azima hii. Na mimi nimeanzisha Taasisi ya Mama Anna Mghwira kwa ajili ya kushughulikia masuala ya aina hii.

  Nitawashukuru sana kwa niaba ya vijana wetu, tuenzi elimu yao kwa kuunganisha nguvu zetu hivi. Mnisamehe kwa kuandika mtandaoni. Nimejaribu njia za kawaida za simu sikufanikiwa sana. Hapa ninajua kila moja atapata taarifa. Mapungufu yangu yasizuie jambo hili kutendeka. Jinsi tulivyo changia madawati, sasatuchangie elimu ya juu.

  Niombe wizara na Bodi ya mikopo ya wanafunzi kutoa ushirikiano tutakapouhitaji utaalamu muwe nasi bega kwa bega.

  Mungu atubariki wote, aibariki Tanzania.

  Asanteni tena, ni mimi mama Anna Mghwira
   
 2. k

  kamwamu JF-Expert Member

  #241
  Jun 7, 2017
  Joined: May 18, 2014
  Messages: 1,399
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri, na uwezo kupitia kwa wananchi wapenda maendeleo upo. Serikali kukwepa jukumu la kugharimia elimu ya juu ni ubinafsi wa viongozi wetu, na mgawanyo usio sawa wa raslimali zetu. Mafanikio ya elimu ya vijana wetu ndio mafanikio ya taifa. Elimu bure ya msingi mpaka f4 si mzigo mkubwa kwa familia. Uwezo kulipia chuo kikuu ni mgumu. Wingi wa mikopo inayotajwa kutolewa na sesikali ina mapambio, kuna wengi wamepata %ge ndogo sana. Wazo hili likijitangaza kwa wananchi, wengi watahamasika kuchangia. Mchango wa sh 1000 tu kwa mwezi, kwa watu 1m, kwa mwaka 1, mfuko wako utakuwa sh 12bn za kusomesha watoto elfu 6 kwa 2m.
   
 3. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #242
  Jun 7, 2017
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 17,592
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  Karibu Kilimanjaro mama, tuko pamoja!!
   
 4. Saytoti

  Saytoti Senior Member

  #243
  Jun 8, 2017
  Joined: Mar 7, 2014
  Messages: 160
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Wazo liendelee hata kama mama sahivi ni mkuu wa mkoa wa k/njaro
   
 5. DearCalen

  DearCalen Member

  #244
  Jun 9, 2017
  Joined: Jun 9, 2017
  Messages: 87
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 25
  hongera mama kwa wazo zuri kma lingeskka kwa wakuu lkatekelezwa ingekuwa vzur zaid
   
 6. Ze Heby

  Ze Heby JF-Expert Member

  #245
  Jun 9, 2017
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 3,946
  Likes Received: 2,139
  Trophy Points: 280
  Akirudi kwenye huu uzi mniite
   
 7. mwima

  mwima Member

  #246
  Jun 10, 2017
  Joined: Nov 24, 2014
  Messages: 10
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  SAFI SANA MAMA YANGU MPENDWA, NA MIMI NILIPATWA NA JANGA HILO NIMESAIDIWA NA MWANAMKE, SASA NINA DEGREE YANGU SAFI, NAWAPENDA SANA WANAWAKE WOTE.
   
 8. T

  Tulimumu JF-Expert Member

  #247
  Jun 10, 2017
  Joined: Mar 11, 2013
  Messages: 8,207
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  Kapewa uongozi sasa.
   
 9. Fundisi Muhapa

  Fundisi Muhapa JF-Expert Member

  #248
  Jun 10, 2017
  Joined: Nov 25, 2013
  Messages: 4,436
  Likes Received: 1,532
  Trophy Points: 280
  Unaweza kujiamini na kujitangaza wewe ni mtabiri. Yule RC uzuri hatakua ameiba wazo. Litakua lake. Kongole kwake.
   
 10. Weza

  Weza Member

  #249
  Jun 11, 2017
  Joined: Oct 24, 2013
  Messages: 67
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Marahaba mwanangu
   
 11. geophrey20

  geophrey20 JF-Expert Member

  #250
  Jun 12, 2017
  Joined: Feb 11, 2013
  Messages: 1,498
  Likes Received: 665
  Trophy Points: 280
  mmmmmmmmh
  umetoka k njaro saa ngapi
   
 12. Weza

  Weza Member

  #251
  Jun 12, 2017
  Joined: Oct 24, 2013
  Messages: 67
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Haahaaaa usishtuke mwanangu, bado nipo nilikuja kwenye report ya makinikia
   
 13. Daud1990

  Daud1990 JF-Expert Member

  #252
  Jun 12, 2017
  Joined: Mar 15, 2014
  Messages: 4,205
  Likes Received: 5,039
  Trophy Points: 280
  Akirudi kwenye huu Uzi Nitaruka kichurachura Manyoni mpaka Butimba
   
 14. Omulasil

  Omulasil JF-Expert Member

  #253
  Jun 13, 2017
  Joined: May 5, 2015
  Messages: 570
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 60
  Hili wazo utekelezaji wake siuoni. AU NI KUJADILI TU. hivi ni vikao vya manyani . msitucheke matako yatapokuwa mekundu.
   
 15. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #254
  Jun 20, 2017
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,730
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  Atarudi tena huku?
   
 16. bridalmask

  bridalmask JF-Expert Member

  #255
  Jun 20, 2017
  Joined: Jan 14, 2015
  Messages: 2,168
  Likes Received: 1,093
  Trophy Points: 280
  Huyu familia ya bshiete,ccm b hana uhalali wala haki ya kusema chochote tena,kwani ni tabia mbaya ukiwa msaliti na kuongea wakati wakula tena mbaya zaidi chakula kiko kinywani siyo ustaarabu kabisaa.
  Anyamaze kimya atuache wenye hofu ya Mungu,tuwasemee wenzetu na kujisemea not u and ua all family.
   
 17. Metakelfin

  Metakelfin JF-Expert Member

  #256
  Jul 2, 2017
  Joined: Mar 23, 2017
  Messages: 2,158
  Likes Received: 1,780
  Trophy Points: 280
  kweli usimuamini mwanasiasa mama kapata uongozi sahizi kimya
   
 18. Raykidd

  Raykidd Member

  #257
  Jul 20, 2017
  Joined: Sep 28, 2016
  Messages: 32
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  asante mama yetu kwa kulijua maana lilikuwa kimya kiasi cha kutaka kusahaulika maisha tunayoishi anajua mola tumeunga ndo tupo hapa mwaka wa kwanza umeisha hatujui hatujui hatima yetu kuendelea mwaka wa pili wengi wetuuu asanteeeeeee
   
 19. B

  BRIA JF-Expert Member

  #258
  Jul 22, 2017
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  ]
  Kaonanene na Polepole Lumumba kupata mikopo
   
 20. soine

  soine JF-Expert Member

  #259
  Jul 25, 2017
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 701
  Likes Received: 400
  Trophy Points: 80
  Ni kweli kipindi cha mwalimu yalifanyika hayo unayosema, tena kwa mafanikio makubwa sana. Ukiangalia hali ya sasa kiujumla, kuna maswali mengi unatakiwa ujiulize kabla ya kulinganisha maisha ya sasa na ya kipindi cha mwalimu. Je, vipi uwiano wa rasimali na idadi ya watuukoje? hali ya hewa ikoje? tulikuwa na mashirika mangapi ya umma yaliyokuwa hai na yenye tija kwenye uchumi? (Kumbuka kuwa Tanzania ilikuwa ya pili Afrika nyuma ya Msumbiji (1000)kwa kuwa na mashirika ya umma 400 ambayo yalikuwa productive in 1980s); Je, sera za biashara za kimataifa zikoje kwa sasa tofauti na kipindi cha mwalimu? Vipi kuhusu sera na sheria tulizo nazo juu ya usimamizi wa rasimali zetu?

  Ni ukweli usiopingika kuwa tulipaswa kuwa pazuri zaidi, ila tumekwamishwa na mipango yetu isiyothibitika na kudumu hata kuona matunda yake, pia sheria, sera, na mikataba yetu/zetu ni kitanzi kingine kwa maendeleo ya taifa letu.
   
 21. kelvin marcus

  kelvin marcus JF-Expert Member

  #260
  Jul 25, 2017
  Joined: Jun 24, 2017
  Messages: 2,626
  Likes Received: 7,261
  Trophy Points: 280
  Hii kwa wahenga tunaitaga prison break yaani ni game juu game...
  Kweli hakuna anayependa kuonekana mbaya
   
Loading...