Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Wapendwa wanajukwaa ni takribani miezi sita (6) tangu nilipoleta hoja za kuanzisha mfuko wa kusaidia kuongeza wigo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kuongeza idadi toka pale bodi ya mikopo ilipoishia.

Napenda kuwajulisha kuwa taratibu za kisheria na kiofisi zimekamilika, kutokana na majukumu yangu ya sasa ofisi itaendeshwana watendaji wafuatao Maryconsolata Shao kama mtendaji mkuu mwenye taaluma ya Microfinance, wakili Elizabeth Mamba kama mwanasheria wa kampuni pia Peter Shedrack kama mtaalamu wa ICT.

Kuna uhitaji mkubwa wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ukiachilia mbali ile inayotolewa na bodi ya mikopo, kuna akaunti namba ya kampuni katika benki ya crdb 0150294113400 karibuni kuchangia kama tulivyojadili huko nyuma.

Ahsanteni na Bwana awabariki kwa kutoa kwenu
 
Baada ya miezi sita ndiyo unakumbuka kuhusu huu uzi?

Inatia shaka sana kuhusu hili ombi lako kama ulikuwa na dhamira ya kweli kusaidia au kufanya yako. Huwezi kuwa na dhamira ya kweli halafu ukapotea miezi sita.

Wachangiaji akili mkichwa.

Wapendwa wanajukwaa ni takribani miezi sita (6) tangu nilipoleta hoja za kuanzisha mfuko wa kusaidia kuongeza wigo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kuongeza idadi toka pale bodi ya mikopo ilipoishia.
 
Hapana Dereck,

Mjadala umeendelea lakini pia taratibu za kisheria ni ndefu sana mpaka kupata kibali cha kuchangisha, kupata watu wa kuendesha, kufanya usaili nk.

Licha ya majukumu yangu ya sasa, watendaji hawa wamejitahidi kukamilisha kazi hii kutokea pale tulipokuwa mwezi wa 5 mwishoni. Pia kuwasiliana na mamlaka zote husika: Wizara ya Elimu, Baraza na Bodi ya mikopo, pia wadau wengine wa elimu, kupata wahitaji halisi nk. Kuna shirika la aina hii lilianzishwa lakini muda mfupi walikuta wanakopesha wafanya biashara si wanafunzi.

Kwa hiyo miezi 6 ni muda mdogo kwa kukamilisha taratibu hizi na kuwa na taarifa sahihi za kila hatua. Tumepata pia wanafunzi wenye uhitaji wa kutosha na isingekuwa vema kuwapa matumaini kabla ya kukamilisha hatua hizi zote.

Kwa sasa tuna akaunti ya benki, na namba ya voda za kuchangisha ambayo nitaileta hapa muda si mrefu. Asanteni wote.
 
Kipi bora kwanza kuwekeza zaidi kwenye elimu au airport, ndege, serikali kuhamia Dodoma?

Keben,

Huu siyo moja ya program za serikali. Ni wazo ambalo halina mfungamano wowote na serikali wala siasa. Ni juhudi za mtu binafsi na wadau wengine wote wa maendeleo bila ubaguzi wa itikadi za vyama, vya siasa, dini, rangi wala Kabila katika kuhakikisha mtoto wa kitanzania anapata elimu iliyo bora hata kama anatoka katika familia zenyewe changamoto za kiuchumi.

KWA PAMOJA TUTAWEZA.
 
Mh. Anna,

Kwanza nakupongeza sana kwa kuja na wazo hili,kwa miaka mingi Africa ikiwemo Tanzania yetu tumekuwa na matumaini kwa wanasiasa kwamba wao peke yao wa naweza kutatua matatizo yetu na ndio fulumai za kisiasa haziishi na umasikini haukomi,hapa wapo watakaosema umekuja kisiasa lakini suala sio la kisiasa kabisa.

Idadi hiyo ya vijana walikosa mkopo ukijumlisha na udadi kubwa ya walio nje ya masomo inamtosha mwanasiasa kumwingiza bungeni na kumuacha akilalamika shida yake. Wakati umefika wa kutatua changamoto zetu wenyewe.

Geofrey Julius Lweshabra
Africa's youth first network
 
Mpango uko pale pale. Wenye uhitaji ndio wanaoweza kuona. Wazo lilipoanza na kuonekana linafaa, ilibidi lifanyiwe kazi za ziada kukamilisha taratibu zinazohusika. Si rahisi kupata namba za kuchangisha kutoka kamampuni ya simu na hata benki. Sasa tumekamilisha, tunaweza kuanza na wanafunzi wachache kwa muhula huu. Watakaokuwa tayari kuchangia ni hiari na kwa faida ya wenye uhitaji.

Asanteni wote kwa michango ya hali na mali, maoni na ushauri.

Angalau unakuja hapa kushirikiana na vijana na kuwapa mawazo japo unamajukumu mengine.
 
Wapendwa wanajukwaa ni takribani miezi sita (6) tangu nilipoleta hoja za kuanzisha mfuko wa kusaidia kuongeza wigo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kuongeza idadi toka pale bodi ya mikopo ilipoishia.

Napenda kuwajulisha kuwa taratibu za kisheria na kiofisi zimekamilika, kutokana na majukumu yangu ya sasa ofisi itaendeshwana watendaji wafuatao Maryconsolata Shao kama mtendaji mkuu mwenye taaluma ya Microfinance, wakili Elizabeth Mamba kama mwanasheria wa kampuni pia Peter Shedrack kama mtaalamu wa ICT.

Kuna uhitaji mkubwa wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ukiachilia mbali ile inayotolewa na bodi ya mikopo, kuna akaunti namba ya kampuni katika benki ya crdb 0150294113400 karibuni kuchangia kama tulivyojadili huko nyuma.

Ahsanteni na Bwana awabariki kwa kutoa kwenu
Unajua mama Mimi sijawahi kukuelewa na huu Uzi wako,Jana Rais wako katangaza kuwa hela ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu imeongezeka,na idadi ya wanafunzi wanaochukua mikopo imeongezeka.

Kwa harakaharaka tafsiri ya hili ni kwamba, huduma za mikopo ktk kwenye serikali ya awamu ya tano zmeboreka ukilinganisha na serkali ya awamu ya NNE.

Sasa ikiwa zimeboreshwa, tunawachangiaje hawa watu walioboreshewa huduma wakati huu kitu ambacho hakikujitokeza katIka awamu ya NNE na wakatI huo huduma ya mikopo ulikuwa haijaboreshwa?!!!!
 
Wazo LA mama ni zuri ,na linaweza kutekelezeka. Ila tatizo ni kwamba huyu mheshimiwa wa huku karibu na bahari ni mwepesi mno kubadilisha matumizi ya pesa ,utasikia pesa zilizopatikana tumewalipa engineers waliokuwa wanabomoa jengo ra tanesco ili tuwasaidie wanyonge
 
Mama naomba usimame na mjadala huu uendeleee, kweli kuna vjiana wenzetu wameacha masomo kwa kukosa fedha zitzkazo mudu gharama za masomo yao,zipo baadhi ya taasisizinazotoamikopokweli lakini masharti yao ni magumu mno kwaraiamkulima, nakuomba mama uendeleekupaz sauti na Mungu muumba wa mbingu na nchi ataiinua sauti yako na kufikia masikio ya wenye moyo kama wako wengi,nijambo muhimu sana kwa zama hizi jamani.
 
Hapana Dereck,

Mjadala umeendelea lakini pia taratibu za kisheria ni ndefu sana mpaka kupata kibali cha kuchangisha, kupata watu wa kuendesha, kufanya usaili nk.

Licha ya majukumu yangu ya sasa, watendaji hawa wamejitahidi kukamilisha kazi hii kutokea pale tulipokuwa mwezi wa 5 mwishoni. Pia kuwasiliana na mamlaka zote husika: Wizara ya Elimu, Baraza na Bodi ya mikopo, pia wadau wengine wa elimu, kupata wahitaji halisi nk. Kuna shirika la aina hii lilianzishwa lakini muda mfupi walikuta wanakopesha wafanya biashara si wanafunzi.

Kwa hiyo miezi 6 ni muda mdogo kwa kukamilisha taratibu hizi na kuwa na taarifa sahihi za kila hatua. Tumepata pia wanafunzi wenye uhitaji wa kutosha na isingekuwa vema kuwapa matumaini kabla ya kukamilisha hatua hizi zote.

Kwa sasa tuna akaunti ya benki, na namba ya voda za kuchangisha ambayo nitaileta hapa muda si mrefu. Asanteni wote.
Mods Toeni huu Uzi.Huyu Mama yetu KeshaShiba.Uzi ndo umekufs hivo
 
Nauza vifaranga contact 0754890286
b96d9101bd5e15a590cde8920a3f3d9a.jpg
 
Nakushauri uendelee kutumikia chama chako, Haya mengine waachie wanaotaabika nayo!
Ushauri wangu kwako ni huo Kwan Nakuona mnafki sana
 
Back
Top Bottom