Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua


Anna Mghwira

Anna Mghwira

Verified Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
203
Likes
341
Points
80
Anna Mghwira

Anna Mghwira

Verified Member
Joined Mar 9, 2012
203 341 80
Ninaikumbuka vema kauli ya mama Salma Kikwete kuwa nanukuu: " Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako." Leo watoto wa wenzetu wameingia tatizo la kukosa mikopo ya elimu ya juu; tuwasaidie kama watoto wetu.

Ninapenda kuwaomba akina mama wote nikianza na Mhe mama Salma Kikwete aliyeasisi usemi na hatua hii, tushirikiane kunusuru maisha ya elimu ya watoto walioko vyuoni wenye sifa ya kuwa na mikopo lakini hawakufanikiwa kupata mkopo. Tuwahamasishe vijana waliobakia mitaani na majumbani kujiunga na vyuo vikuu kuanua akili zao changa kukidhi ushindani wa sasa kimaisha.

Naomba akina mama wote viongozi, wazazi, walezi, wafanya bishara, waajiriwa, wanaharakati bila kujali itikadi zetu za aina yoyote tusimame kama wanawake wazazi wenye nia kuejnga taifa la watu walioelimika tuunde mfuko wa kuwasiadia watoto wetu wafanikiwe kumaliza masomo yao kwa ujenzi wa taifa letu.

Nikitoka na mama Kikwete ninaomba wake za marais wote waliopita kuanzia na mama Karume (mzee marehemu na Rais aliyemaliza mda wake) mpaka mama Janet Magufuli anayenivutia sana kwa kuonesha moyo wa amani sana kwa taifa letu.

Baada ya hao nimuombe mama Anna Makinda na wabunge wanawake wote waliopo na waliomaliza tangu uhuru wa nchi yetu tuungane kumsaidia kila mtoto wa Tanzania mwenye uwezo wa kusoma asome.

Kisha kwa niaba ya wanawake wafanya bishara niombe kitengo cha wanawake cha TCCIA, Baraza la Biashara la wanawake...tukubali wito huu: Tuungane kama wazazi na walezi chini ya kauli mbiu: Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako...tuunde mfuko wa elimu kwa ajili ya vijana wetu.

Niombe vyama vya wana-taaaluma: waalimu, madaktari, wahandisi, watumishi wa umma, mabenki, makampuni yote ya ndani na ya kigeni, asasi za kiraia za ndni na za kimataifa, balozi zetu zote, tuungane kuunda chombo hiki kuwasaidia vijana wetu.

Nimeguswa sana na mahangaiko ya vijana wa vyuo vikuu. Ninawashukuru wachache waliofika kwangu kueleza changamoto zao. Mmenihamasisha kuchangia kidogo elimu yenu lakini ninaomba hili liwe suala la kitaifa.

Ninaomba wanawake wenzangu popote tulipo tuwasiliane tuunde umoja huu kuwaimarisha na kuwapa tumaini vijana na janga la kukosa elimu ya juu kama wana sifa za kuipata.

Tuweke kando siasa, dini, kabila, ukanda ama aina yoyote ya kigezo kufanikisha jambo hili. Ninawashukru sana. Kesho kuna wanafunzi watashindwa kufanya mitihani kwa kukosa ada kidogo tu ya laki kuanzia 5-8. Mfuko wa mama Salma, Mfuko wa mama Mkapa wa Fursa sawa kwa wote, Taasisi ya Benjamini mkapa, Taasisi ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na zingine, tusaidiane kukamilisha azima hii. Na mimi nimeanzisha Taasisi ya Mama Anna Mghwira kwa ajili ya kushughulikia masuala ya aina hii.

Nitawashukuru sana kwa niaba ya vijana wetu, tuenzi elimu yao kwa kuunganisha nguvu zetu hivi. Mnisamehe kwa kuandika mtandaoni. Nimejaribu njia za kawaida za simu sikufanikiwa sana. Hapa ninajua kila moja atapata taarifa. Mapungufu yangu yasizuie jambo hili kutendeka. Jinsi tulivyo changia madawati, sasatuchangie elimu ya juu.

Niombe wizara na Bodi ya mikopo ya wanafunzi kutoa ushirikiano tutakapouhitaji utaalamu muwe nasi bega kwa bega.

Mungu atubariki wote, aibariki Tanzania.

Asanteni tena, ni mimi mama Anna Mghwira
 
Leonard Mwaisunga

Leonard Mwaisunga

New Member
Joined
Sep 25, 2017
Messages
2
Likes
0
Points
3
Leonard Mwaisunga

Leonard Mwaisunga

New Member
Joined Sep 25, 2017
2 0 3
Wazo zuri sana mfuko uitwe Anna Mghwira Education Support Trust Fund( AESTF) nitawaambia rafiki zangu pale kwa Mfalme kule redsea
Asante sana mama kwa wazo chanya,nitashukulu sana kama jambo hili litafanikiwa japo na mimi ni mmoja kati ya waathirika ambaye sina uhakika wa kumaliza masomo yangu na kwanza mwaka wa kwanza. Naomba Mungu awape nguvu katika kufanikisha jambo hili.
 
JUAN MANUEL

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Messages
1,171
Likes
1,102
Points
280
JUAN MANUEL

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2010
1,171 1,102 280
Kwanini hatutumii mapato ya gesi,mafuta kusomesha watoto,nchi hii inapesa nyingi sana,escrow walokomba 320billioni,pesa ya bodi ya mkopo itoke bandarini iende kwenye akaunti ya bodi moja kwa moja,tukipunguza ukubwa wa serikali,tuuwe wizara moja,watumishi wake wote wastaafishwe,tufanye kama sekta binafsi,kampuni ikifa,unachukua chako unasepa,
Mkoa mmoja ufe,viongozi wake wastaafishwe wore,kuanzia mkurugenzi,mpaka mkuu wa mkoa,
Pesa yote iliyokuwa inaperekwa huko,iende kwenye mfuko wa bodi ya mikopo,
Na hii ifanyike kila mwaka,vijana,Dada zetu,kaka zetu,wadogo zetu watasoma kwa raha
 
M

MCHARA

Senior Member
Joined
Jan 15, 2011
Messages
112
Likes
5
Points
35
M

MCHARA

Senior Member
Joined Jan 15, 2011
112 5 35
Mama naomba usimame na mjadala huu uendeleee, kweli kuna vjiana wenzetu wameacha masomo kwa kukosa fedha zitzkazo mudu gharama za masomo yao,zipo baadhi ya taasisizinazotoamikopokweli lakini masharti yao ni magumu mno kwaraiamkulima, nakuomba mama uendeleekupaz sauti na Mungu muumba wa mbingu na nchi ataiinua sauti yako na kufikia masikio ya wenye moyo kama wako wengi,nijambo muhimu sana kwa zama hizi jamani.
Kweli
 
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
8,488
Likes
6,047
Points
280
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
8,488 6,047 280
Wakuu! Mama leo ameniomba nimwombee kwa staff wa JF kama itawapendeza basi waifute kabisa thread hii!! Inamkosesha amani,inamtisha! Tafadhali jamani,yaliyopita si Ndwele!
 
maishapopote

maishapopote

JF Gold Member
Joined
May 28, 2009
Messages
2,136
Likes
1,198
Points
280
maishapopote

maishapopote

JF Gold Member
Joined May 28, 2009
2,136 1,198 280
Mikopo inatolewa kwa watoto waliosoma shule za Kata tu, huo ndiyo msimamo wa Serikali hii na ndiyo kigezo kikuu
Hivi haiwezekani kwamba mtoto ulimsomesha shule za english medium then alipofika Alevel mambo yakabadilika,labda ukafilisika au caregiver akafariki au akaumwa akawa hajiwezi na mtoto akawa hana uwezo wa kujilipia bila mkopo...najaribu kuangalia scenario kama hizi...na kujiuliza
 
ndyoko

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
4,982
Likes
312
Points
180
ndyoko

ndyoko

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
4,982 312 180
Kwani huyu si ndo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. mbona ni kama analalamika chakula kibaya wakati wapishi anakaa nao jikoni!!!???
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,865
Likes
50,208
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,865 50,208 280
Hivi haiwezekani kwamba mtoto ulimsomesha shule za english medium then alipofika Alevel mambo yakabadilika,labda ukafilisika au caregiver akafariki au akaumwa akawa hajiwezi na mtoto akawa hana uwezo wa kujilipia bila mkopo...najaribu kuangalia scenario kama hizi...na kujiuliza
Sema hivi, hivi hakuna wazazi wanaojinyima na wanakula mchicha na dona mlo mmoja ili kuwasomesha watoto wao english medium wakitegemea akifika Chuo kikuu na ufaulu mzuri atapewa mkopo?, jibu ni kwamba wapo wengi sana na mimi ni mmoja wao
 
mjumbe wa bwana

mjumbe wa bwana

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
3,516
Likes
2,930
Points
280
mjumbe wa bwana

mjumbe wa bwana

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
3,516 2,930 280
Kwani huyu si ndo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. mbona ni kama analalamika chakula kibaya wakati wapishi anakaa nao jikoni!!!???
kipindi hicho alikuwa anatumia akili zake kufikiri sahivi mwenyekiti ndo anamsaidia kufikiri nazani soon atamwomba mood wafute maana ashaenda kuunga mikono juhudi za mweshimiwa mwenyekiti
 
mtumishidc

mtumishidc

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Messages
509
Likes
23
Points
35
mtumishidc

mtumishidc

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2012
509 23 35
Tutakapokuwa tayari kuigawa vyema keki ya taifa na kuruhusu bodi ya mikopo itoe mikopo bila vigezo baguzi tutakuwa tumeliwezesha kundi linalohitaji elimu ya juu toka jamii yote liifikie ndoto hiyo bila vikwazo, mifuko, wakfu na taasisi zingine zitabaki kuhudumia makundi maalum kwa uchache wao!!
 
Meshe

Meshe

Senior Member
Joined
Nov 14, 2011
Messages
132
Likes
67
Points
45
Meshe

Meshe

Senior Member
Joined Nov 14, 2011
132 67 45
Samahani lakini naomba kuuliza!! Hivi huyu aliyeleta huu uzi ndio huyohuyo RC wa Kilimanjaro au mfanano wa majina?
 
S

S31

Member
Joined
Mar 15, 2018
Messages
27
Likes
15
Points
5
S

S31

Member
Joined Mar 15, 2018
27 15 5
Hahahahahahahahahahahahahah daah this is Tanzania ya viwandaaaaaaaaàaaaaà mnanichosha mm ujue
 
S

S31

Member
Joined
Mar 15, 2018
Messages
27
Likes
15
Points
5
S

S31

Member
Joined Mar 15, 2018
27 15 5
Kwanini hatutumii mapato ya gesi,mafuta kusomesha watoto,nchi hii inapesa nyingi sana,escrow walokomba 320billioni,pesa ya bodi ya mkopo itoke bandarini iende kwenye akaunti ya bodi moja kwa moja,tukipunguza ukubwa wa serikali,tuuwe wizara moja,watumishi wake wote wastaafishwe,tufanye kama sekta binafsi,kampuni ikifa,unachukua chako unasepa,
Mkoa mmoja ufe,viongozi wake wastaafishwe wore,kuanzia mkurugenzi,mpaka mkuu wa mkoa,
Pesa yote iliyokuwa inaperekwa huko,iende kwenye mfuko wa bodi ya mikopo,
Na hii ifanyike kila mwaka,vijana,Dada zetu,kaka zetu,wadogo zetu watasoma kwa raha
Pambaneni Na Hali zenu CCM mbele kwa Mbele mtaisoma namba mm cmo
 
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
18,542
Likes
24,906
Points
280
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
18,542 24,906 280
Wakuu! Mama leo ameniomba nimwombee kwa staff wa JF kama itawapendeza basi waifute kabisa thread hii!! Inamkosesha amani,inamtisha! Tafadhali jamani,yaliyopita si Ndwele!
tehteehh.....
 
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
18,542
Likes
24,906
Points
280
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
18,542 24,906 280
Kwani huyu si ndo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. mbona ni kama analalamika chakula kibaya wakati wapishi anakaa nao jikoni!!!???
Hapo alikua analalamika enzi zileeee.... kabla hajatunukiwa cheo (RC) huko Kilimanjaro
 

Forum statistics

Threads 1,238,883
Members 476,223
Posts 29,335,494