Anna Makinda: Natambua Zitto Kabwe bado ni mbunge

Anna Makinda: Natambua Zitto Kabwe bado ni mbunge

Nadhani Chadema hawana shida na ubunge wake chadema wana shida na Uanachama wake
 
Ila kuna kitu najiuliza hapa tume ilisema inasubiri taarifa toka bungeni na bunge linasubiri taarifa toka NEC.Hapa imekaeje?

Kadiri ya uelewa wangu Mkuu kyumana, CHADEMA wanapaswa kutoa taarifa kwa Spika wa Bunge.Halafu Ofisi ya Spika itamuarifu Mwenyekiti wa NEC kuwa kuna jimbo liko wazi kw hatua za kiuchaguzi kama inawezekana. Kuna tetesi kuwa kinasubiriwa kikao cha CC ya CHADEMA cha Mei mwaka huu ili ki-note na halafu taarifa kamili ya kikatiba itolewe kwa Spika
 
Ninachokiona hapo ni kuwa .tuna viongozi ambao wanaendesha vyama kwa kutumia emotions zao zaidi na hivyo kujikuta wakiacha kanuni,taratibu na sheria za chama. Hata mfanyakazi anapofukuzwa kazi ni lazima apewe barua ambayo itaelezea kuachishwa kwake kazi na sababu zilizopelekea yeye kuachishwa kwake.
Kama hayo hayajafanyika unategemea Spika amzuie Bungeni kwa kigezo gani? Ni lazima awe na ushahidi wa maandishi ambayo ni barua toka Chama husika.

Tukiacha haya mambo yaendelee hivi hivi,je,siku CDM ikishika dola ndo itakavyofanya hivi huko serikalini unamfukuza Waziri kwenye TV na wala humuandikii barua?!!

Hawachelewi kutangaza bajeti Twitter.

I get more disappointed with CDM by the day, inabidi nikubaliane na Pasco, hawa watu hawajajiandaa kuchukua nchi. ni muda muafaka wakae chini watulize vichwa na kujenga mifumo ya kueleweka kwenye chama chao, sio kila siku kupoteza kujenga mifumo ya kutafuta wasaliti na kufukaza tu. wajenge mifumo positive itakayowapa watanzania taswira ya CDM pindi itakaposhika nchi. So far am not impressed.
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini Zitto kama Zitto asione haya na kutoka mwenyewe?

Anag'ang'ania nini? Si anajifanya mara jembe mara kichwa kwa nini asiondoke tu.

CHADEMA haitaki, nasi hatukutaki nenda ACT yako basi.
Broo zzk anakunyima usingizi daaah pole sana
 
Bunge likianza tu Makinda anapewa barua ili awatangazie na wabunge wote kwamba jamaa alitimuliwa CDM?

Hakuna haraka.
 
Je kwanini Chadema hawajapeleka hizo taarifa hadi sasa?

Umeambiwa Tume ya Uchaguzi ndio yenye jukumu la kulitaarifu Bunge sio CHADEMA. Pia usisahau kuwa CHADEMA watapeleka taarifa kwenye tume kama watakuwa wamepata hukumu ya mahakama.
 
Kadiri ya uelewa wangu Mkuu kyumana, CHADEMA wanapaswa kutoa taarifa kwa Spika wa Bunge.Halafu Ofisi ya Spika itamuarifu Mwenyekiti wa NEC kuwa kuna jimbo liko wazi kw hatua za kiuchaguzi kama inawezekana. Kuna tetesi kuwa kinasubiriwa kikao cha CC ya CHADEMA cha Mei mwaka huu ili ki-note na halafu taarifa kamili ya kikatiba itolewe kwa Spika

Tatizo letu tuna haraka kuliko taratibu walizojiwekea CHADEMA.
 
ALikuwa mbuge wa mahakama sasa ni mgombea huru imeanzia kwake japo kwenye katiba yetu hakuna mgombea huru hii ni fadhila ya chama cha zamani
 
Ikipelekwa barua atajiona mshindi. Mwache aendelee kuishi kwa hofu ndani ya Ubunge kwa hisani ya Chadema hadi ajione mpu-mbavu. Unacheza na ma-intelectuals waliojazana hapo Ufipa wewe! Ndio anauwawa kisaikolojia hivyo; itafika mahali akiona rangi kama za Chadema atakuwa anapiga mayowe na kukimbia kama mwendawazimu. Adhabu kali kabisa kuliko kuandikiwa hicho kibarua ambacho magamba wanaweza kupiga nacho danadana kumlinda mtu wao. Mwacheni hivyo hivyo!

ha ha ha ha ha! Te teh Teh Teh teh. kwa Jf mnafurahisha
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anna Makinda amesema anamtambua Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zubeir Kabwe kuwa ni mbunge halali kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa rasmi kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusiana na ubunge wake kutenguliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge Spika Makinda amesema kuna taratibu zilitakiwa kufuatwa ambapo mpaka sasa taratibu hizo hazijakamilika na kumfanya kumtambua kuwa ni mbunge halali wa jimbo hilo la Kigoma Kaskazini.

Chanzo: ITV

Anne Makinda ana busara sana anafaa kuwa Raisi wetu wa kwanza mwanamke.
 
Chadema pelekeni basi hiyo barua tuanze muvi yaZitto part 2.
 
Spika wa bunge ni msomi jamani afanyi kazi kinafiki hata sikumoja
kwanini chadema msifwate sheria inavyotaka pelekeni taarifa muone kitakachofwata
si mmeshamvua mnaogopa nini kujulisha bunge......au mnataka aende mahakamani kudai barua ya kuvuliwa ubunge ...?????
 
Hawachelewi kutangaza bajeti Twitter.

I get more disappointed with CDM by the day, inabidi nikubaliane na Pasco, hawa watu hawajajiandaa kuchukua nchi. ni muda muafaka wakae chini watulize vichwa na kujenga mifumo ya kueleweka kwenye chama chao, sio kila siku kupoteza kujenga mifumo ya kutafuta wasaliti na kufukaza tu. wajenge mifumo positive itakayowapa watanzania taswira ya CDM pindi itakaposhika nchi. So far am not impressed.
Tuliza boli acha uzandiki so far zitto si mwana chama wa chadema by merit ukipeleka chama mahakamani ukashindwa kesi you are out , baada ya kikao cha Mei wataamua waandishi wamesha sikia habari kibao zikieleza haya lakini wamekazana na spinning ha ha ha inachekesha mwache apate malupulupu ya ubunge kuhakikisha act inakuwa manake hatarudi bungeni by any means traitor
 
chadema pelekeni basi hiyo barua tuanze muvi yazitto part 2.

popoompo hawa unafikiri watapeleka leo wanajifikiria aibu inayoenda kuwakuta mahakamani tena...mi yangu macho kinachoumiza ni baadhi ya vichwa vyangu kudondokea kwenye usanii wa chady....
 
Tuliza boli acha uzandiki so far zitto si mwana chama wa chadema by merit ukipeleka chama mahakamani ukashindwa kesi you are out , baada ya kikao cha Mei wataamua waandishi wamesha sikia habari kibao zikieleza haya lakini wamekazana na spinning ha ha ha inachekesha mwache apate malupulupu ya ubunge kuhakikisha act inakuwa manake hatarudi bungeni by any means traitor

MPWA
CC KESI YA KAFULILA...Naogopakukupa majibu
 
Spika wa bunge ni msomi jamani afanyi kazi kinafiki hata sikumoja
kwanini chadema msifwate sheria inavyotaka pelekeni taarifa muone kitakachofwata
si mmeshamvua mnaogopa nini kujulisha bunge......au mnataka aende mahakamani kudai barua ya kuvuliwa ubunge ...?????
Good strategy chadema let them wait and wait for taarifaa rasmi he lost ha ha no body notices his presence I pity him atajijua mwenyewe Shibuda type
 
Back
Top Bottom