Anna Makinda: Natambua Zitto Kabwe bado ni mbunge

Anna Makinda: Natambua Zitto Kabwe bado ni mbunge

Watazungusha zungusha mambo weeeee, lakini ukweli ni kwamba ZZK sio mwanachama tena wa CHADEMA na kwa maana hiyo siyo mbunge tena

Ndio hivyo Mkuu! Ingekuwa ni Lema au Wenje walahi, Spika angetangaza kuvuliwa kwao ubunge siku hiyo hiyo tena saa sita usiku na ingekuwa breaking news vyombo vyote vya magamba.
 
Ikipelekwa barua atajiona mshindi. Mwache aendelee kuishi kwa hofu ndani ya Ubunge kwa hisani ya Chadema hadi ajione mpu-mbavu. Unacheza na ma-intelectuals waliojazana hapo Ufipa wewe! Ndio anauwawa kisaikolojia hivyo; itafika mahali akiona rangi kama za Chadema atakuwa anapiga mayowe na kukimbia kama mwendawazimu. Adhabu kali kabisa kuliko kuandikiwa hicho kibarua ambacho magamba wanaweza kupiga nacho danadana kumlinda mtu wao. Mwacheni hivyo hivyo!

Chezea CHADEMA wewe. Hujasikia hata yule "MSUKUMA" anaomba afukuzwe lakini hafukuzwi? Wajiondoe wenyewe
 
Spika atambue asitambue atajijua mwenyewe, Chadema kama chama kimeshasema Zitto sio mwanachama basi. Kama Makinda anataka kumtambua kama Mbunge wa CCM au TLP shauri yake. Lengo la Chadema sio kumvua ubunge bali kumtoa miongoni mwa Wanachadema kwa kukiuka katiba.
Ni aibu kwa Bunge kujifanya nao wanaingia kwenye malumbano badala ya kusoma katiba ya nchi inasema nini kuhusu wabunge.
 
Kwa nini Zitto kama Zitto asione haya na kutoka mwenyewe?

Anag'ang'ania nini? Si anajifanya mara jembe mara kichwa kwa nini asiondoke tu.

CHADEMA haitaki, nasi hatukutaki nenda ACT yako basi.
Taratibu lazima zifuatwe nchi haiendeshwi kwa matamko ya radio au TV. Andikeni barua
 
Wanamuogopa zitto sana hawa chadema.

Mtu amefukuzwa halafu matope yako kichwani yanakuambia anaogopwa nawe unayaamini? Anayeogwopwa ni Lowasa na miccm ambayo kila siku inamwita majina ya hovyo lakini hata kumkaripia tuu wanashindwa.
 
CHADEMA msimpe barua kabisaaa aendelee kuwaadaa watu wake wa ACT na nitafanya ziwe nyingi.
 
Kwa nini Zitto kama Zitto asione haya na kutoka mwenyewe?

Anag'ang'ania nini? Si anajifanya mara jembe mara kichwa kwa nini asiondoke tu.

CHADEMA haitaki, nasi hatukutaki nenda ACT yako basi.

Kwani kunaugumu gani wakumuandikia barua kumfamisha zitto spika nec viongozi wako wana gwaya nini wewe kifaranga kakimya tu
 
Hivi Lissu punguani uso wake atauweka wapi?
 
Wanamuogopa zitto sana hawa chadema.
alisema yeye ni zaidi ya chama, leo anahangaika kutafuta huruma za wanachadema. na kwa taarifa yako huku kitaa maccm tu ndiyo wanahangaika na zitto. sasa chama kwanini kisimdhalau? atatangaza mwenyewe kuondoka ni swala la mda tu.unajuwa inawezekana mpaka sasa haamini kilichotokea kwake. Mwacheni aenderee kuhangaika, taratibu ataelewa na atatowa taarifa mwenyewe kwa speker
 
Ninachokiona hapo ni kuwa .tuna viongozi ambao wanaendesha vyama kwa kutumia emotions zao zaidi na hivyo kujikuta wakiacha kanuni,taratibu na sheria za chama. Hata mfanyakazi anapofukuzwa kazi ni lazima apewe barua ambayo itaelezea kuachishwa kwake kazi na sababu zilizopelekea yeye kuachishwa kwake.
Kama hayo hayajafanyika unategemea Spika amzuie Bungeni kwa kigezo gani? Ni lazima awe na ushahidi wa maandishi ambayo ni barua toka Chama husika.

Tukiacha haya mambo yaendelee hivi hivi,je,siku CDM ikishika dola ndo itakavyofanya hivi huko serikalini unamfukuza Waziri kwenye TV na wala humuandikii barua?!!
 
Lisu anaakili sana,dr slaa bonge la jembe,mbowe anatisha yaani ujue wanajua mchezo utaishia wapi siunaona wamenyamaza lakini mwiguru anatokea hapa,makinda anaongea hili,wanaccm wanahaha wao wametulia wanasoma mchezo wao tu watahangaika weeee then utaona watakavyo tulizwa hawataamin.
 
Ninachokiona hapo ni kuwa .tuna viongozi ambao wanaendesha vyama kwa kutumia emotions zao zaidi na hivyo kujikuta wakiacha kanuni,taratibu na sheria za chama. Hata mfanyakazi anapofukuzwa kazi ni lazima apewe barua ambayo itaelezea kuachishwa kwake kazi na sababu zilizopelekea yeye kuachishwa kwake.
Kama hayo hayajafanyika unategemea Spika amzuie Bungeni kwa kigezo gani? Ni lazima awe na ushahidi wa maandishi ambayo ni barua toka Chama husika.

Tukiacha haya mambo yaendelee hivi hivi,je,siku CDM ikishika dola ndo itakavyofanya hivi huko serikalini unamfukuza Waziri kwenye TV na wala humuandikii barua?!!
hivi tiba aliandikiwa barua?? dawa ya kiburi ni kuwa kiburi zaidi yake
 
Hiyo iko wazi na wala haihitaji kukuza jambo kama hili.Taarifa rasmi ikifikishwa katika mamlaka husika jambo hilo litafikia mwisho

Ila kuna kitu najiuliza hapa tume ilisema inasubiri taarifa toka bungeni na bunge linasubiri taarifa toka NEC.Hapa imekaeje?
 
Back
Top Bottom