Anna Makinda: Natambua Zitto Kabwe bado ni mbunge

Anna Makinda: Natambua Zitto Kabwe bado ni mbunge

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anna Makinda amesema anamtambua Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zubeir Kabwe kuwa ni mbunge halali kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa rasmi kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusiana na ubunge wake kutenguliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge Spika Makinda amesema kuna taratibu zilitakiwa kufuatwa ambapo mpaka sasa taratibu hizo hazijakamilika na kumfanya kumtambua kuwa ni mbunge halali wa jimbo hilo la Kigoma Kaskazini.

Chanzo: ITV

bongo movie bado inaendelea.....
 
Katibu wa Uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Longido Ndugu Onesmo Steven Maarufu kwa jina la SIMON amekihama Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, katika viwanja vya Eworendeki, Namanga.

Mwenezi huyo wa Chadema amefikia hatua hiyo baada ya kuona kuwa CHADEMA ni chama cha kibabaishaji ambacho hakina mwelekeo na wanatumia siasa za kilaghai kudanganya wananchi na kuifarakanisha jamii.

Kinana amempokea Mwenezi huyo kutoka CHADEMA na kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi kinawakaribisha wale wote ambao wamegundua ulaghai wa Upinzani na kwamba CCM haina ubaguzi kwani kila mwanachama ana haki sawa na mwingine, hakuna kuoneana wala upendeleo.

Sasa wale jamaa zangu waliozoea kukanusha waje wakanushe na hii.
paperclip.png
Attached Thumbnails
 
Jaman mbona huyo spika na nec wanacomplications hivo..?? Chama kimeshasema hatumtambui huyu mtu tena na taarifa najua imeshawafikia..ivi maana ya media ni nini hasa.zitto anauhusiano uliofichika na CCM...na ndo maana wanamtetea..!!
 
Nilitegemea yafuatayo kufanywa na Chadema.
Kumwandikia Zitto barua ya kuvuliwa uanachama.
Kulitaarifu bunge kuwa Zitto kaondoleewa uanachama.
Afu mengine yatafata.
Ila waliongea kwenye radio tu, yakawa yameishia hapo

Una uhakika na ulichokiandika hapa kwamba hayo hayajafanyika?

Tiba
 
Ila kuna kitu najiuliza hapa tume ilisema inasubiri taarifa toka bungeni na bunge linasubiri taarifa toka NEC.Hapa imekaeje?

chadema wamesha ziaandikia barua hizo mamlaka kuzijulisha au unataka wafanye kazi kwa taarifa za magazeti???
 
Manyanyaso anayofanyiwa Zitto hayapaswi kushabikiwa na watu wazalendo,wapenda maendeleo na wanaopinga matumizi mabaya ya fedha.
 
Spika wa bunge ni msomi jamani afanyi kazi kinafiki hata sikumoja
kwanini chadema msifwate sheria inavyotaka pelekeni taarifa muone kitakachofwata
si mmeshamvua mnaogopa nini kujulisha bunge......au mnataka aende mahakamani kudai barua ya kuvuliwa ubunge ...?????

Mkuu leo haupo katka ubora wako au kuna mtu kahack a/c yako?
 
Hatuna haja ya kuwalazimisha chadema wafanye haya yanayotakiwa kufanyika sasa, ni watu wanaojielewa sana na ndio maana hata haya maamuzi waliyochukua hatukuwashawishi sisi wana jf. Tungoje kusikia tena kutoka kwao.
 
Nilitegemea yafuatayo kufanywa na Chadema.
Kumwandikia Zitto barua ya kuvuliwa uanachama.
Kulitaarifu bunge kuwa Zitto kaondoleewa uanachama.
Afu mengine yatafata.
Ila waliongea kwenye radio tu, yakawa yameishia hapo
Kamati kuu lazima ikae,ipokee taarifa,imjadili kwa kua ilizuiliwa na mahakama kumjadili ndipo imtimue
 
Wana mazingaumbwe ndivyo wanavyo cheza michezo yao. Mahali sensitive ka bungeni anaingia mtu asiye stahili, Spika anasema ati sijapewa barua.
Chadema tulieni tuli, mmesha mwambia kajifukuza mwenyewe, na zzk kama hajui tafsiri za katiba ya chama chake basi hafai hata kujiita mwanachama.
Kama anaijua katiba ya chama chake, hata huko bungeni hata kanyaga kwani hana chama na ubunge pia hana. Akitaka kuwatendea haki wana jimbo, awaambie yeye si mbunge,
 
Nilitegemea yafuatayo kufanywa na Chadema.
Kumwandikia Zitto barua ya kuvuliwa uanachama.
Kulitaarifu bunge kuwa Zitto kaondoleewa uanachama.
Afu mengine yatafata.
Ila waliongea kwenye radio tu, yakawa yameishia hapo

Dogo una haraka kama cha-kwanza
 
Back
Top Bottom