Anna Makinda: Natambua Zitto Kabwe bado ni mbunge

shalet

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
3,428
3,513
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anna Makinda amesema anamtambua Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zubeir Kabwe kuwa ni mbunge halali kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa rasmi kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusiana na ubunge wake kutenguliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge Spika Makinda amesema kuna taratibu zilitakiwa kufuatwa ambapo mpaka sasa taratibu hizo hazijakamilika na kumfanya kumtambua kuwa ni mbunge halali wa jimbo hilo la Kigoma Kaskazini.

Chanzo: ITV
 
mpaka zito atamilza muda wake kama mbunge halali.
 
Taarifa itapelekwa kwa ofisi ya bunge na spika ndiye wakumjulisha nec
 
sasa nani ni nani maana nec wanasema tunasubiri taarifa kutoka kwa spika na spika anasema anasubiri taarifa kutoka kwa nec sasa huu mgongano wa majukumu nan ni nan
 
Kwa nini Zitto kama Zitto asione haya na kutoka mwenyewe?

Anag'ang'ania nini? Si anajifanya mara jembe mara kichwa kwa nini asiondoke tu.

CHADEMA haitaki, nasi hatukutaki nenda ACT yako basi.
 
Kwa nini hampeleki barua nyie vichwa maji ma division zeros.kudos

Ikipelekwa barua atajiona mshindi. Mwache aendelee kuishi kwa hofu ndani ya Ubunge kwa hisani ya Chadema hadi ajione mpu-mbavu. Unacheza na ma-intelectuals waliojazana hapo Ufipa wewe! Ndio anauwawa kisaikolojia hivyo; itafika mahali akiona rangi kama za Chadema atakuwa anapiga mayowe na kukimbia kama mwendawazimu. Adhabu kali kabisa kuliko kuandikiwa hicho kibarua ambacho magamba wanaweza kupiga nacho danadana kumlinda mtu wao. Mwacheni hivyo hivyo!
 
Back
Top Bottom