I'm at Old Trafford.
Huyu mama wakati anahesabu hayo makanisa alijumuisha pia makanisa ya nyumbani? Kama vipi mwambieni huyo mama asilete za kuleta makanisa siyo majengo bali ni watu waaminio.
Naamini ni hivyo hivyo kwa Waislamu pia maana ni majuzi tuu wakati wa mapinduzi ya Misri, tuliona Waislamu wa huko wakiswali live katikati ya barabara bila kuguswa na polisi au washawasha. Hawakuhitajiji kwenda kwenye majengo ya msikiti kuswali.
Ajaribu kujiuliza mwenyewe mbona huwa wanasali/swali mle mjengoni kabla ya vikao vyao vya bunge, kwani ni jengo la kanisa/msikiti lile?
Kwa wale wanaofuata maandiko ya Bibilia, kwenye Agano la Kale kulikuwa hakuna majengo ya kuombea. "Naye alipotambua hilo, alikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Mariamu, mama yake Yohana aliyeitwa Marko pia, ambapo watu wengi walikuwa wamekusanyika pamoja, wakiomba" (Matendo 12:12).
"Wasalimuni Priska na Akwila pamoja na kanisa lililo nyumbani mwao
" (Warumi 16:3-5).
"Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, pamoja na Nimpa, na kanisa lililo nyumbani mwake (Wakolosai 4:15).
Na kwa dada yetu Afia, na Arkipo, mtenda kazi mwenzetu, na kwa kanisa lililo nyumbani mwako
" (Filemoni mstari wa 2).
Hata Agano la Jipya ni vile vile. Yesu alisema kuwa "Mahali popote ambapo wawili au watatu wamekusanyika pamoja katika Jina langu, nipo katikati yao" (Mathayo 18:20).
Yesu hakusema chochote kuhusu mahali pa waamini kukutanika. Hata kama wapo waamini wawili tu, aliahidi kuwepo kama watakusanyika katika jina lake. Full stop, nukta!
Sasa huyu mama analeta gozi gozi wakati hata hajui maandiko yanasemaje? Huyu mama anaweza akaongoza mpango mzima wa kuvunja majengo yote ya makanisa nchini lakini makanisa bado yataendelea kuwepo majumbani mwa waamini, ikwezekana hata kwenye miili yao.
Sasa hapo itambidi awauwe kabisa ili kuyamaliza hayo makanisa. Kwa vile mtu akila nyama ya mtu ataendelea kula tuu, basi atageukia majengo ya misikiti na pale Waislamu watakapokuwa wanaswali barabarani, basi ataiangamiza miili yao.
Hebu mwambieni huyo mama aache gozi gozi, afanye kilichompeleka mjengoni. Asitupotezee muda tuko bize tunauguza waamini wa kule Old Trafford wengine wapo intensive care unit ati na hali zao ni mbaya sana.