Anna Abdalah: Makanisa yamekuwa mengi

Anna Abdalah: Makanisa yamekuwa mengi

Status
Not open for further replies.
Sasa kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria hao matapeli? Kwa nini tunapenda general sweeping statements za "makanisa mengi sana" badala ya kuwa specifically focused kwenye matatizo?

Ukipunguza idadi ya makanisa kutoka laki tano kwenda elfu hamsini, halafu hao matapeli wote wakajilundika kwenye hayo elfu hamsini na kujipa uaskofu, utakuwa umetatua nini sasa?
Tatizo ni madhehebu ya kikiristo,yanazuka kila siku mapya,ndio yeye akasema makanisa mengi,nakupa mfano,waweza kuta eneo moja ,ypo makanisa matatu mpaka manne,ni madhehebu tofauti,na hawa wote wanaabudu tofauti,waingiliani ibada zao,Mkiristo huyu haingii kanisa hili na yule haingii kanisa lile,na wote ni waafrika,wa Tanzania.
Tofauti katika uislamu,waislamu wote,wa Tanzania,na wageni waafrika kwa waarabu,wote wanaingia msikti mmoja.
 
Utaratibu wa kusajili makanisa ufanyeje?
wawe na katiba yao,ionyeshe malengo na madhumuni ya kuanzisha kanisa,na wawe na wadhamini,na wanachama wenye majina na saini zao,idadi inayokubalika kuanzisha kanisa.Na eliku ya muanzishaji wa kanisa,iko kiwango gani cha dini.nk
 
Mwambie aende akamuulize baba yake Moh wapi alilipata jina la Abdallah. Akisha pata jibu amuulize Allah wapi alipo Moh. Then she can talk her bogus and diabolic words. Pathetic Anna.
Hapo hata wewe naona elimu unayotumia hajikusaidia kabisa, maana nikweli makanisa nimengi ukilinganisha na waumini waliopo.Lakini hayashangazi sana kwa kuwa ni misaada ya wazungu ili waeneze upuuzi wao kuptia makanisa maana misikiti wameshindwa kupenyeza upumbavu wao.Ndugu zangu misaada ya kondom na vidonge vya uzazi yanaenezwa na wazungu kupitia makanisani je huoni madhara ya utitili wa makanisa yasiyo na waumini.Nasema yapunguzwe.
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana na huyu mama.
Nyumba za kuabudia zimekuwa zikijengwa ovyo bila mpangilo maalum, alafu unakuta wanapiga miziki sijui nini siku nzima. Yaani zimekuwa kero kwa kweli.
Mi nafikiri sheria ya ku regulate nyumba za ibada zitungwe. Yes tunataka Uhuru wa kuabudu, lakini basi tusibughuziane.

yaani mara nyingine unakuta kanisa ndani lina watu 2, lakini wamefungulia maspika mpaka mtaa wa tatu huko, ina bore sana

Na vipi vipaza sauti vya misikiti vinavyo tusumbua alfajiri tukiwa kwenye "Morning glory"?
Nyie watu mna pika chakula msicho kijua,enough with ujinga wenu huu.
 
Naona mnagusa mboni ya ya jicho la Mungu,hamtakaa salama.Biblia inasema Mungu hazihakiwi chochote apandacho mtu atavuna.

wewe na huyo mama ambaye nadhani mapepo yanamsukuma kusema hivyo mnahitaji mkono wa Mungu uwaguse.

kuna machangudoa wamejaa kwenye mitaa ya Shikilango,mpaka kwenye nyumba za watu,kwanini asikemee uhuni huu kuongezeka,kuna baa kila kona,nyingine zina wateja 2,kwanini halalamiki.

nadhani huyu mama ndiyo wanaoleta udini,misikiti ipo kila kona,inapiga adhana alfajiri,mbona wakristo hawajapiga kelele kuwa wanatupigia kelele?

Anna Abdallah usipobadilika na kulewa vyeo.utakutana na Mungu wa BWANA wetu Yesu Kristo na ndipo utajua Umuhimu wa makanisa unayoyadharau.

ASIKIAYE NA AFAHAMU

kwa hiyo mungu munaye muabudu,ana hasira na kulipiza kisasi kwa yoyote anayemtaja.
 
Tatizo ni madhehebu ya kikiristo,yanazuka kila siku mapya,ndio yeye akasema makanisa mengi,nakupa mfano,waweza kuta eneo moja ,ypo makanisa matatu mpaka manne,ni madhehebu tofauti,na hawa wote wanaabudu tofauti,waingiliani ibada zao,Mkiristo huyu haingii kanisa hili na yule haingii kanisa lile,na wote ni waafrika,wa Tanzania.
Tofauti katika uislamu,waislamu wote,wa Tanzania,na wageni waafrika kwa waarabu,wote wanaingia msikti mmoja.

Kuna waislamu wa Sunni hawaingii msikiti wa Shia/ Ismaili/Bohora wala kushiriki sherehe zao. Kuna ma Sufi huko wana mysticism zao tofauti tofauti, etc etc.

Tatizo liko wapi makanisa/ madhehebu yakiwa mengi? Umesoma vifungu vya katiba hapo juu?

Kama serikali imeshindwa urban planning yenyewe hilo ni tatizo la makanisa?

Na kama wakristo wakiamua kuwa na kanisa kila mtaa wa pili serikali inapata wapi haki ya kuingilia uhuru wa wananchi kuabudu wanavyotaka?

This applies to misikiti. Misikiti/ makanisa mangapi yanatosha na mangapi yanakuwa yamezidi?

Na nani ana haki ya kusema hivyo?

Maana wewe unaweza kusema wakristo mna makanisa mengi, wakristo wanaweza kukwambia sie tuna makanisa mengi lakini wewe muislamu unasali mara tano kwa siku unatupigia kelele na muezzin wako.

Kwamba serikali ipunguze maudhi ya muezzin.

Unaona jambo la kuiingiza serikali katika ku regulate dini linavyoweza kukupeleka kubaya?

Ukishaanza kuihusisha serikali kwenye dini utaanzisha vita vya kidini, kwa sababu utaanzisha kitu ambacho kukisimamisha si rahisi.

Halafu habari hizo hizo unazozifurahia kwa sababu wametajwa wakristo leo, kesho utageuziwa kibao wewe muislamu, utaambiwa lolote tu, serikali inaweza kukuambia chochote cha kuingilia uhuru wako wa kuabudu.

Si ushaanza kutoa precedent kwenye idadi ya makanisa? na wewe utaambiwa jumuiya zote za kiislamu sikasajiliwe na mufti kibaraka wa CCM, ma sheikh ambao hawaipendi CCM wataminywa.

Unaanzisha vagi kwa kuipa serikali nguvu ya kuingilia mambo yasiyoihusu.

Mwisho utaambiwa misikiti ibadili kibra ielekee Dodoma mji wetu mkuu.

Si ushahalalisha serikali kuingilia mambo ya dini sasa?
 
Tatizo ni madhehebu mapya ya kikiristo kila siku,imekuwa dini ni biashara,mbona wakatoliki wanaabudu bila fujo,wala wa Angalikana,madhehebu ya zamani hayo,ni watu wazuri,na wanafanya ibada kiistaraabu
 
Tatizo liko wapi makanisa/ madhehebu yakiwa mengi? Umesoma vifungu vya katiba hapo juu?

Kama serikali imeshindwa urban planning yenyewe hilo ni tatizo la makanisa?

Na kama wakristo wakiamua kuwa na kanisa kila mtaa wa pili serikali inapata wapi haki ya kuingilia uhuru wa wananchi kuabudu wanavyotaka?

This applies to misikiti. Misikiti/ makanisa mangapi yanatosha na mangapi yanakuwa yamezidi?

Na nani ana haki ya kusema hivyo?

Maana wewe unaweza kusema wakristo mna makanisa mengi, wakristo wanaweza kukwambia sie tuna makanisa mengi lakini wewe muislamu unasali mara tano kwa siku unatupigia kelele na muezzin wako.

Kwamba serikali ipunguze maudhi ya muezzin.

Unaona jambo la kuiingiza serikali katika ku regulate dini linavyoweza kukupeleka kubaya?

Ukishaanza kuihusisha serikali kwenye dini utaanzisha vita vya kidini, kwa sababu utaanzisha kitu ambacho kukisimamisha si rahisi.

Halafu habari hizo hizo unazozifurahia kwa sababu wametajwa wakristo leo, kesho utageuziwa kibao wewe muislamu, utaambiwa lolote tu, serikali inaweza kukuambia chochote cha kuingilia uhuru wako wa kuabudu.

Si ushaanza kutoa precedent kwenye idadi ya makanisa? na wewe utaambiwa jumuiya zote za kiislamu sikasajiliwe na mufti kibaraka wa CCM, ma sheikh ambao hawaipendi CCM wataminywa.

Unaanzisha vagi kwa kupa serikali nguvu ya kuingilia mambo yasiyoihusu.

Mwisho utaambiwa misikiti ibadili kibra ielekee Dodoma mji wetu mkuu.

Si ushahalalisha serikali kuingilia mambo ya dini sasa?

Hujui kama jumuia za kiislamu zote zimesajiliwa serekalini?Na zinatambulikana kisheria?Usajili haufanyiki bila kuwa na idadi inayotakiwa kisheria,katiba,na wadhamini,nk.lakini utakuta kanisa lina watu wawili,hili limepata usajili wapi?
 
wawe na katiba yao,ionyeshe malengo na madhumuni ya kuanzisha kanisa,na wawe na wadhamini,na wanachama wenye majina na saini zao,idadi inayokubalika kuanzisha kanisa.Na eliku ya muanzishaji wa kanisa,iko kiwango gani cha dini.nk

Hilo sio tatizo.

Tatizo ushaambiwa makanisa yamekuwa mengi, kwa hiyo hata ukija na katiba na vitu ulivyovitaja muelekeo ni kupigwa stop kwa sababu mengi tayari.

Kama tatizo ni usajili hata yawe mengi vipi, wingi si hoja kwa sababu usajili ndio utakuwa hoja.
 
Jamani I was sitted at Home Ghafla msikitini wakaanza Mhadhara,wanawaiga Mapadri na wana kashifu ukristo mwanzo Mwisho,sasa nani wa kulaumiwa?wanakandamiza wakristo kwanini?kwanini wasianze na waislamu na kutoa mivipaza zauti,maana ma Imamu wanaongea Pumba?

Amani yangu Na wapeni,Sii kama ulimwengu utoavyo!
 
Hujui kama jumuia za kiislamu zote zimesajiliwa serekalini?Na zinatambulikana kisheria?Usajili haufanyiki bila kuwa na idadi inayotakiwa kisheria,katiba,na wadhamini,nk.lakini utakuta kanisa lina watu wawili,hili limepata usajili wapi?

Usajili na wingi ni masuala mawili tofauti.

Unaweza kuwa na makanisa mengi na yote yamesajiliwa.

Na unaweza kuwa na machache na yote hayajasajiliwa.

Kinachopigiwa kelele hapa ni wingi, si usajili.

Maana yake hata watu wakiamua kusajili makanisa yao yote, kama kinachopigiwa kelele ni wingi tu, suala la wingi halimalizwi na usajili.

Makanisa 500, yakiwa yamesajiliwa au hayajasajiliwa yatabaki kuwa 500 tu.

Huwezi kusema eti makanisa 500 yakisajiliwa yatageuka 50.

Usajili gani huu unaokiuka kanuni za hesabu?
 
Jamani I was sitted at Home Ghafla msikitini wakaanza Mhadhara,wanawaiga Mapadri na wana kashifu ukristo mwanzo Mwisho,sasa nani wa kulaumiwa?wanakandamiza wakristo kwanini?kwanini wasianze na waislamu na kutoa mivipaza zauti,maana ma Imamu wanaongea Pumba?

Amani yangu Na wapeni,Sii kama ulimwengu utoavyo!

Rwanda wenzetu wamechapana sasa wanaheshimiana kidogo. Na sisi ndo tunachotafuta sasa.

Amani ikizidi sana inalevya.
 
Mi nashangaa kuna watu humu udini hauwaishi hata wapigwe brush ya chuma...Sa umewahi kuona kanisa bila watu, kila mtu anaenda kusali katika imani yake...Mbona misikiti nayo kibao tu, tembea uone, kwa wao wanajua misikitini hela zinakotoka..?
 
Mi naona huyo mama ana dini, na hajui umuhimu wa dini katika maisha ya binadamu...

Hapa kuna kingine zaidi ya dini.

Serikali kuendekeza mfumo-imla katika nyanja ambazo haina mamlaka nazo kikatiba.

Wanawabeep polepole hapo.

Leo mtaambiwa makanisa mengi sana, tuyapunguze, mkikubalikubali kikondoo kondoo tu...

Kesho mnaambiwa magazeti mengi sana, tuyapunguze, keshokutwa vyama vya siasa vingi sana, tuvipunguze.

Tofauti kubwa ni nini?
 
Nasikia wale jamaa wanaotaka kujitoa kwenye katiba nao wanakanisa lao.
 
Anna Abdallah alishasikia hii hotuba?

Sikiliza kuanzia 5:10 ndipo panahusu sana

Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom