Uhuru usio na mipaka ni sawa na fujo na ghasia nyingi, thru churches rotten deals kibao zimekuwa zikifanyika zikiwemo za madawa ya kulevya. kuna ukweli mkubwa sana kwenye kitabu na movie ya Davince Code... Anyway nashindwa kuielewa nukushi yako "Banda limesha vunjika, Jogoo kashaondoka, Vifaranga mkazane kumtoa nyoka"! Huoni kuwa vifaranga vingi sana vitafariki?...Opium?
Uhuru una mipaka. Mipaka ya uhuru ni sheria. Ndiyo maana nikarejea kwenye sheria mama, katiba.
Serikali yetu imekataa hata kuweka kifungu cha kumuhesabu mtu kwa dini Tanzania, kwa kutambua "separation of church and state".
Sasa huyu mama anavyotaka kuja kutuambia leo makanisa mengi sana wakati hata hana jinsi ya kujua idadi ya Wakristo Tanzania kiserikali, kwa sababu serikali ilikataa kuwahesabu watu kwa dini, anajuaje kama makanisa ni mengi sana? Anaielezeaje ile principle ya "separation of church and state" iliyoifanya serikali ikatae kuhesabu watu kwa dini?
Serikali gani hii kigeugeu? Jana imekataa kuhesabu wakristo, kwa sababu haitaki kujiingiza kwenye dini, leo imehesabu makanisa na kuyaona mengi sana, hata bila ya kujua wakristo wako wangapi.
Inaingia akilini kweli hii?
Kama una matatizo na rotten deals, target rotten deals, usi target idadi ya makanisa ukafanya mtego wa panya unasao waliokusudiwa na wasiokusudiwa.
Unaweza kusema makanisa mwisho 500 nchi nzima, na bado hayo 500 yakawa na rotten deals vile vile kama huangalii rotten deals specifically. What has rotten deals to do with the number of churches?
Kama nina matatizo yoyote na waumini, kitu kimoja sina tatizo nao. Pale inapokuja haki yao ya kikatiba ya kuabudu naiheshimu, na naitetea.
Nakataa totalitarianism. Tukikubali serikali ituwekee namba ya makanisa leo, kesho serikali hiyo hiyo itarudi na kusema "magazeti mengi sana sasa, inabidi tuyapunguze"
Unaweka precedent ya kuipa serikali nguvu ya kuvunja katiba. Kuondoa uhuru wa kuabudu, kuondoa uhuru wa habari etc.
Tushaanza kusikia habari kwamba wanataka kutunga sheria kali dhidi ya maandamano, ambayo nayo ni haki ya kikatiba.
Ingawa sifagilii makanisa, sifagilii wananchi kunyimwa haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kuabudu zaidi.
Where
EMT at ?