Anna Abdalah: Makanisa yamekuwa mengi

Anna Abdalah: Makanisa yamekuwa mengi

Status
Not open for further replies.
Kwa kiasi fulani nakubaliana na huyu mama.
Nyumba za kuabudia zimekuwa zikijengwa ovyo bila mpangilo maalum, alafu unakuta wanapiga miziki sijui nini siku nzima. Yaani zimekuwa kero kwa kweli.
Mi nafikiri sheria ya ku regulate nyumba za ibada zitungwe. Yes tunataka Uhuru wa kuabudu, lakini basi tusibughuziane.

yaani mara nyingine unakuta kanisa ndani lina watu 2, lakini wamefungulia maspika mpaka mtaa wa tatu huko, ina bore sana

Suala la ujenzi mbovu ni tofauti, hayo ni mambo ya urban planning. Kama kuna tatizo makanisa yanajengwa ovyo, then Anna Abdallah anaongea na Anna Tibaijuka wanapeleka muswada wa kuimarisha urban planning.

Urban planning tuna matatizo sana, si makanisa tu, kuna mabaa, gereji etc. Zipo kama utitiri. Sasa kwa nini tuzungumzie makanisa tu badala ya kuzungumzia urban planning in general?

Lakini kusema "makanisa yamekuwa mengi sana" is so imposing.

Nchi yenyewe masikini, watu wanaona wanapata "therapeutic relief" makanisani ndo maana makanisa mengi nchi masikini.

Kama unataka kuyamaliza makanisa leta maendeleo ya kiuchumi, leta elimu, utaona makanisa yanaisha yenyewe bila hata ya mkono wa serikali.
 
Uhuru wa kuabudu hauwezi kutumika pale baadhi ya wachungaji wanapogeuza taasisi za dini kuwa vyombovya ufisadi.
Tukumbuke mfano wa JOSEPH Kibwetere ,alipoangamiza wafuaso wake,aliuwa wafuasi wake wanaofilia elfu moja,kwa kuwachoma moto kanisani.Na aliyafanya haya akiwa na viongozi wenzake,maaskofu wawili,na mwanamke mmoja wa kanisa hilo.
Jambo kama hilo liliwahi kutokea nchini Guyana,ambapo mchungaji,James Warren,alianzisha kanisa lake na kuua waumini wake 900 kwa sumu ya cyanide,akawambia mkifa mwaenda kumuona yesu.
Kutokana utapeli wa namna hii,lazima viongozi wenye dhamana wawe na waswas.
 
Sasa kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria hao matapeli? Kwa nini tunapenda general sweeping statements za "makanisa mengi sana" badala ya kuwa specifically focused kwenye matatizo?

Ukipunguza idadi ya makanisa kutoka laki tano kwenda elfu hamsini, halafu hao matapeli wote wakajilundika kwenye hayo elfu hamsini na kujipa uaskofu, utakuwa umetatua nini sasa?
 
huu upumbavu wa makanisa hata kenya walikuwa nao baada ya kuona usanii umezidi ikabidi wapige stop kuregister mapya nakubaliana na mama anna, upuuzi tu na maneno yao ya toa ndugu toa uku watoaji wakibaki choka mbaya na wapokeaji wakitembelea ma vogue
 
Huyu mama yuko frustrated baada ya mzee kuandaliwa mashitaka na PCCB juu ya rushwa na ufisadi pale TANAPA

Leo nilimsikiliza bungeni huyu mama akitoa wimbo mpya. Kwamba makanisa yamekuwa mengi na nadhani kwa kauli yake hiyo anahitaji yapunguzwe, sijui kiasi gani anajua mwenyewe. Jamani, kila siku tunaomba viongozi wetu hawa wa weigh out kauli zao kabla ya kuzitoa.

Hivi ngoja nimuulize tena mama Anna Abdalah, mbona sijawahi kusikia akilalamika kuwa vituo vya polisi vimekuwa vingi? Hivi anajua kazi za makanisa? Naona sasa anataka kuleta hoja kuwe na makanisa mangapi nchini??

Mama Anna kwa hili ulichemka kabisaaaaaa na tukisema ni udini unakusumbua utakataa? najua utakataa kwa kigezo cha majina yako lakini rohoni umejaza udini.:angry:
 
huu upumbavu wa makanisa hata kenya walikuwa nao baada ya kuona usanii umezidi ikabidi wapige stop kuregister mapya nakubaliana na mama anna, upuuzi tu na maneno yao ya toa ndugu toa uku watoaji wakibaki choka mbaya na wapokeaji wakitembelea ma vogue

Watu wavivu ndio wanapenda mitego ya panya inayonasa wanaotakiwa na wasiotakiwa.

Watu makini wenye kuelewa maana ya uhuru wa kuabudu hawawezi kuacha ku register makanisa mapya kwa sababu ya zamani yamefanya utapeli.

That's like kukataza kutoa leseni za udereva mpya kwa sababu madereva wa zamani wanaendesha vibaya sana na wamesababisha ajali.

Kwa nini usi deal na hao wahalifu na badala yake unataka ku punish watu wengine ambao hawana nia ya kufanya uhalifu kabisa? Na pengine wanaweza hata kusaidia katika vita dhidi ya uhalifu?

Tukianza kuiachia serikali ituambie makanisa mangapi yanatututosha leo, kesho ikisema "magazeti mengi sana, tuyapunguze" tutasemaje? Tutaikatalia? Precedent tutakuwa tushaweka.

Ukiweka habari ya serikali kutupangia idadi ya makanisa haina tofauti na serikali kutupangia idadi ya magazeti. Vyote viwili vinavunja haki za mwananchi za kikatiba.

Na huwezi kuwa na sheria itakayosimama kama imevunja katiba, kwa sababu katiba ndiyo sheria mama.
 
yana uozo mwingi sana haya makanisa ya kukurupuka hao hao ndio matapeli haitoshi mitandao ya madawa ya kulevya ndo wao jamani me ntabaki huku nilipo sitaki kabisa vinyesi hivi
 
yana uozo mwingi sana haya makanisa ya kukurupuka hao hao ndio matapeli haitoshi mitandao ya madawa ya kulevya ndo wao jamani me ntabaki huku nilipo sitaki kabisa vinyesi hivi

Tatua tatizo husika basi.

Kuna makanisa yanaendesha biashara ya mihadarati? Kamata wahalifu washtaki mahakamani, waadhibu.

Sio kuleta habari za jumlajumla ambazo hazitasaidia lolote zaidi ya kuleta totalitarianism tu. Utawala wa serikali kuwapangia wananchi wake mpaka makanisa yawe mangapi nchini.

Mwisho watasema wakristo mmezidi sana, tunataka kuweka balance nchini kati ya wakristo na waislam, kwa hiyo wewe na wewe na wewe mnatakiwa musilimu.

Kwa amri ya serikali.

Mtapinga vipi na mshaanza kukubali serikali iamue makanisa yawe mangapi nchini?

Hivi hii serikali ndo ya chama na chi vile vile vya Nyerere? Nyerere aliyekuwa anajivunia kwamba hata hajui mawaziri wake ni dini gani?

Leo ndo tumefika hapa serikali inataka kuweka quota ya idadi ya makanisa kama mzazi anavyompimia maziwa mtoto?
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana na huyu mama.
Nyumba za kuabudia zimekuwa zikijengwa ovyo bila mpangilo maalum, alafu unakuta wanapiga miziki sijui nini siku nzima. Yaani zimekuwa kero kwa kweli.
Mi nafikiri sheria ya ku regulate nyumba za ibada zitungwe. Yes tunataka Uhuru wa kuabudu, lakini basi tusibughuziane.

yaani mara nyingine unakuta kanisa ndani lina watu 2, lakini wamefungulia maspika mpaka mtaa wa tatu huko, ina bore sana

Naona mnagusa mboni ya ya jicho la Mungu,hamtakaa salama.Biblia inasema Mungu hazihakiwi chochote apandacho mtu atavuna.

wewe na huyo mama ambaye nadhani mapepo yanamsukuma kusema hivyo mnahitaji mkono wa Mungu uwaguse.

kuna machangudoa wamejaa kwenye mitaa ya Shikilango,mpaka kwenye nyumba za watu,kwanini asikemee uhuni huu kuongezeka,kuna baa kila kona,nyingine zina wateja 2,kwanini halalamiki.

nadhani huyu mama ndiyo wanaoleta udini,misikiti ipo kila kona,inapiga adhana alfajiri,mbona wakristo hawajapiga kelele kuwa wanatupigia kelele?

Anna Abdallah usipobadilika na kulewa vyeo.utakutana na Mungu wa BWANA wetu Yesu Kristo na ndipo utajua Umuhimu wa makanisa unayoyadharau.

ASIKIAYE NA AFAHAMU
 
kiranga kama jina lako ntakupa data ufatilie na upeleke mahakamani me nitashindwa mana familia yangu inanihitaji sana tena
 
Katiba Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko hapa

http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

Soma vifungu hivi vinne ambavyo Anna Abdallah anataka kuvikiuka vyote kwa mpigo.

18.Uhuru wa maoni.
19.Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.
20.Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine.
21.Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.

Haki ya Uhuru wa Mawazo
Uhuru wa Maoni

Sheria ya
1984 Na.15 ib.6
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.

Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
Sheria ya 1992
Na.4 ib…
19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani
na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu
kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya
Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza
dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya nchi.
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike
kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na
maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo
nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.

wa mtu
kushirikiana na
wengine Sheria
ya 1984 Na.14
ib.6

20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria
za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani,
kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo
hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au
mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au
kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa
halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho
kutokana na Katiba au sera yake-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-
(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila pahala watu
watokeapo, rangi au jinsia;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya
Jamhuri ya Muungano;
(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano:
(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au
mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya
kisiasa;
(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake
za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya
Muungano;
(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na
kwa njia za kidemokrasia.
(3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti
yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na
vigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu
uhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika.
(4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku
kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au
shirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwa
kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma
Sheria ya 1984
Na.15
ib.6
Sheria ya 1994
Na.34 ya ib.4

21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67
ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya
kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki
katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya
Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa
nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi
waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia
utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu
katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha
yake au yanayolihusu Taifa
 
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike
kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na
maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo
nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.

Leo nikitaka kuanzisha kanisa langu la ma-atheist bongo (ambalo mpaka sasa halipo bado) nikaambiwa "Makanisa mengi sana, yametosha" nitakuwa nimenyimwa haki yangu ya kikatiba ya kuanzisha kanisa la ma atheist.

Ambalo halipo bongo kwa sasa na hivyo siwezi kwenda kwingine kokote kwenye kanisa hilo la ma atheist.

Papa kiranga lazima apinge habari za sheria za kizandiki kama hizi.

Makanisa mengi sana wakati mie sina langu hata moja?
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana na huyu mama.
Nyumba za kuabudia zimekuwa zikijengwa ovyo bila mpangilo maalum, alafu unakuta wanapiga miziki sijui nini siku nzima. Yaani zimekuwa kero kwa kweli.
Mi nafikiri sheria ya ku regulate nyumba za ibada zitungwe. Yes tunataka Uhuru wa kuabudu, lakini basi tusibughuziane.

yaani mara nyingine unakuta kanisa ndani lina watu 2, lakini wamefungulia maspika mpaka mtaa wa tatu huko, ina bore sana

Kwahiyo dawa yake yapigwe mabomu wakati wa ufunguzi ili waogope kufungua mengine? Sauti kubwa za kanisani, ni kelele, Vipi kuhusu ile inayoitwa AZANA, ambayo kispika chake hutoa sauti itakayo wafikia wakazi wote wa eneo hilo?

Ile dhana ya kuvumiliana na kupendana ndio muhimu kwa sasa, kwasababu hiyo ndo itakayoleta kusikilizana pale utakapo muomba mwenzako apunguze saut ya kispika/Music, Lakini ukisema WALE VILE na wenzako watasema NYIE VILE, na chokochoko zitaendelea, mwishowe NGUMI zitapigwa na Mabomu yataendelea kurushwa...!!

Huyo mama amechemka na kuna uwezekano akaeleweka vibaya na kuzidisha hasira za watu/waumini/waathirika, aombe Radhi mara moja.
 
Leo nilimsikiliza bungeni huyu mama akitoa wimbo mpya. Kwamba makanisa yamekuwa mengi na nadhani kwa kauli yake hiyo anahitaji yapunguzwe, sijui kiasi gani anajua mwenyewe. Jamani, kila siku tunaomba viongozi wetu hawa wa weigh out kauli zao kabla ya kuzitoa.

Hivi ngoja nimuulize tena mama Anna Abdalah, mbona sijawahi kusikia akilalamika kuwa vituo vya polisi vimekuwa vingi? Hivi anajua kazi za makanisa? Naona sasa anataka kuleta hoja kuwe na makanisa mangapi nchini??

Mama Anna kwa hili ulichemka kabisaaaaaa na tukisema ni udini unakusumbua utakataa? najua utakataa kwa kigezo cha majina yako lakini rohoni umejaza udini.:angry:

.
Anna Abdallah?? Huu ni aina ya mchanganyo wa uzao ambao kwa sheria na kanuni za Mungu hauna ukombozi. Ni mfano wa punda kihongwe. Punda kihongwe ni zao la kuchanganya uzao kati ya punda na farasi. Punda anaweza kukombolewa na ana uzao wake mwenyewe hali kadhali farasi lakini sii kwa kihongwe na tena hana uzao wake mwenyewe. Vivyo hivyo Anna(mkristo) Abdallah(msilamu).
.
 
This week I am partnered with some strange bedfellows.

First it was Glenn Beck on our shared distaste for .docx files.

And now I am in the unenviable position of being on the same side of the argument with religious zealots, for different reasons of course.
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana na huyu mama.
Nyumba za kuabudia zimekuwa zikijengwa ovyo bila mpangilo maalum, alafu unakuta wanapiga miziki sijui nini siku nzima. Yaani zimekuwa kero kwa kweli.
Mi nafikiri sheria ya ku regulate nyumba za ibada zitungwe. Yes tunataka Uhuru wa kuabudu, lakini basi tusibughuziane.

yaani mara nyingine unakuta kanisa ndani lina watu 2, lakini wamefungulia maspika mpaka mtaa wa tatu huko, ina bore sana

vile vipaza sauti alfajir havibughuzi?
 
Kama mleta mada alivyodhani kuhusu alichokisikia kikitamkwa bungeni,binafsi nadhani mtamkaji pengine alikuwa anatoa maoni yake binafsi kupitia bunge na si msimamo wa serikali.Na kama ni msimamo wa serikali kuhusu hatua ya kuyapunguza bungeni si mahala pake,mahala pake ni kuwashirikisha viongozi wa dini kwa karibu zaidi katika utungwaji wa katiba mpya.

Na ikumbukwe kuwa kuyapunguza pekee haitasaidia kuondokana na mmommonyoko wa maadili.Ningefikiri labda pawekwe vigezo maalum kwa madhehebu ya dini yawe na maeneo makubwa ikiwezekana ili isiwe tu kwa ajiri ya kuabudu bali kwa shughuli nyingine za kijamii.
 
Sasa kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria hao matapeli? Kwa nini tunapenda general sweeping statements za "makanisa mengi sana" badala ya kuwa specifically focused kwenye matatizo?

Ukipunguza idadi ya makanisa kutoka laki tano kwenda elfu hamsini, halafu hao matapeli wote wakajilundika kwenye hayo elfu hamsini na kujipa uaskofu, utakuwa umetatua nini sasa?
Ndio mana akasema kuwa na utaratibu wa kusajili makanisa.
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana na huyu mama.
Nyumba za kuabudia zimekuwa zikijengwa ovyo bila mpangilo maalum, alafu unakuta wanapiga miziki sijui nini siku nzima. Yaani zimekuwa kero kwa kweli.
Mi nafikiri sheria ya ku regulate nyumba za ibada zitungwe. Yes tunataka Uhuru wa kuabudu, lakini basi tusibughuziane.

yaani mara nyingine unakuta kanisa ndani lina watu 2, lakini wamefungulia maspika mpaka mtaa wa tatu huko, ina bore sana

waislamu wanapokuwa wanapiga kelele na vipaza sauti vyao hatuongei saa saba mchana na usiku
:angry:
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom