Angalia: Zitto na dadaye, Lissu na dadaye, Ndesa na mwanawe, Dr Slaa na mkewe, Ndesa na mkwewe. Je, Viti Maalumu CHADEMA huzingatia mahusiano?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,875
Najaribu tu kuwakumbusha wale wanaomwandama Mbowe kwamba aliwanyanyasa kijinsia baadhi ya wabunge wa viti maalumu Chadema. Kiukweli mnamuonea bure kabisa mwenyekiti.

Utaratibu wa kuwapata wabunge wa viti maalumu umekuwa na sintofahamu tokea chama hicho kiasisiwe.

Nitoe mifano michache ya wabunge waliokuwa na uhusiano na viongozi wa Chadema na wakateuliwa kutumikia viti maalumu

Katibu mkuu Dr Slaa na " mama watoto" wake Rose Kamili

Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe na dada yake

Mwanasheria wa Chama mzee Marando na shemejie Chiku Abwao

Mjumbe wa CC/mwanasheria Tundu Lisu na dada yake rip

Mjumbe wa CC Ndesamburo rip na mkwewe Grace

Mjumbe wa CC Ndesamburo rip na mwanae Owenya

Katika mazingira kama hayo anayelalamika anapaswa kuzungumzia mfumo mzima na siyo kumsimanga Mbowe ambaye hajampa ubunge ndugu yake yoyote.

Kama huna mtu wa kukubeba basi ni lazima utatumia mbinu za ziada kwahiyo unapolialia baadae ni kwamba ama unajidharirisha au unatangaza biashara kwa chama chako kipya.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom