darcity
JF-Expert Member
- Jul 20, 2009
- 8,721
- 16,932
Kipindi cha miezi mitatu iliyopita nilikuwa katika mikoa hi, na hiki ndicho nilichoshuhudia.
Dar- Daraja la juu ( flyover) ya Uhasibu inajengwa. Shule zote za kata zina madarasa.
Mbeya- Kyela ,Shule za kata karibu zote zina majengo/ madarasa mapya. Mafundi wa kawaida wametumika.
Mwanza- Kisesa pamejengwa kambi ya ujenzi wa reli ya Mwendokasi)umeme inayoanzia Mwanza-Shinyanga-Tabora-Singida. Nahisi ni wachina
Dodoma- Bahi reli ya umeme inajengwa, tuta limepandishwa na reli imewekwa. Nembo za vifaa vya muhandisi vinasoma Yap Merkaz
Mara- Barabara za Bunda-Ghuta -Chisorya, Bunda- Nyamswa, Salama - Nata- Mugumu mkandarasi wa kichina yupo kazini.