Serikali ya Awamu ya 6 na siasa zilizotamalaki

Dkt Mwijuma

Senior Member
Apr 9, 2023
198
561
Mimi ni mtu ambaye sijawahi kuielewa kauli ya "Kazi Iendeleee" kwa sababu kazi sio ile ya Awamu ya 5.

Mama anajinasibu kuendeleza kazi zote alizoachiwa, ni kweli zinaendelea lakini kwanini zinaenda kwa mwendo huo?

Mungu alimuchukua Magufuli mradi wa SGR kipande cha Dar-Moro kikiwa zaidi ya 80%, toka Magufuli ameondoka tunakaribia miaka mitatu sasa lakini mradi bado haujakamilika na kila siku tumekuwa tukipangwa utaanza kutumika mwezi wa tano, mara wa saba hapa tunaelekea mwezi wa tisa sasa bado ni kimya!

Mliopo Dodoma mnaweza kutuambia Mradi wa Ring Road umefikia asilimia ngapi? Mwanza kulikuwa na Ujenzi wa Meli mpaka sasa hivi holaaa, upo nje ya muda, Daraja, vile vile Soko Kuu la Mwanza ndio usiseme hakuna chochote kinafanyika.

Kwa kufuatilia kwangu masuala ya ujenzi na miundo mbinu Dodoma, mradi pekee upo hai mpaka muda huu ni Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Msalato, na nasikia ujenzi huo unatekelezwa kwa fedha za Benki ya Dunia.

Mama Samia akiwa Mwanza alizindua Awamu ya Pili ya ujenzi wa Hoteli ya NSSF five star toka amezindua mpaka muda huu tunaelekea Septemba hola, hakuna kitu kinafanyika pale.

Kuna mtu anaweza kutuambia fedha alizotoa mama za ruzuku ya mafuta zilisaidia nini? Siasa kwenye awamu hii zimekuwa nyingi sana ni uongo kila mahali, ongezeko la mshahara hola.

Yaani mama ameingia akajaa kabisa kwenye mfumo wa Jakaya Kikwete, ufisadi umerudi kama zamani, kucheleweshewa mishahara kupandishwa daraja la kazi bila ongezeko la mshahara kwa wakati, kutowabana mafisadi, mikataba mibovu ya kinyonyaji nk.

Nakumbuka mwaka 2014 Kinana akiwa katibu Mkuu wa CCM alikuwa akifanya mikutano nchi nzima, kwa bahati nzuri alinikuta wilayani Biharamulo sehemu moja panaitwa Nyakahura au Mzani pale kulikuwa na shida ya maji kubwa sana, akaagiza litatuliwe lakini hakuna kilichofanyika.

Nilirudi kule 2015 kipindi cha kampeni za uchaguzi, hilo suala la maji liliwasumbua sana wagombea wa CCM kata (Diwani) na jimbo (Mbuge) maana hakuna agizo lililotekelezwa.
 
DIKTETA magufuli alikuwa muongo WA Dunia . Aliendesha siasa zenye
Ni kweli lkn pamoja na uongo wake ni yeye ndio alienunua ndege hata kama alitudanganya ni yeye ndio alianzisha mradi wa SGR, ni yeye ndio aliazisha ujenzi wa bwawa la Nyerere, Vipi kuhusu vituo vya mabasi? Hospitali za rufaa za kanda, serikali kuhamia Dodoma nk

Siwezi kukata kuwa JPM alikuwa muongo ni kweli mfano kwenye idadi ya samaki ziwani nk lkn mwamba alikuwa anadanganya huku akufanya kiasi chake tofauti na Mama
 
Ni kweli lkn pamoja na uongo wake ni yeye ndio alienunua ndege hata kama alitudanganya ni yeye ndio alianzisha mradi wa SGR, ni yeye ndio aliazisha ujenzi wa bwawa la Nyerere, Vipi kuhusu vituo vya mabasi? Hospitali za rufaa za kanda, serikali kuhamia Dodoma nk

Siwezi kukata kuwa JPM alikuwa muongo ni kweli mfano kwenye idadi ya samaki ziwani nk lkn mwamba alikuwa anadanganya huku akufanya kiasi chake tofauti na Mama
Ccm ni ile ile mkuu
 
Back
Top Bottom