Anayejua anachokisimamia Dkt. Slaa kwa sasa atuambie

ndio alipinga hata sla alipinga ila tatzo la magufuli alipenda sana sifa na majivuno ukimkosoa lazma uwe adui yake, alikuwa apendi kukosolewa na ndo mana alitukandamiza sana upnzani na alikuwa mbinafsi
Ni Rais yupi aliyekubali kuokolewa hapa Tanzania kuanzia Nyerere,hadi Samia? Juzi tu Ndugai na Charamila unajua kilichowapata Wakati wanatoa maoni yao.
 
Ni Rais yupi aliyekubali kuokolewa hapa Tanzania kuanzia Nyerere,hadi Samia? Juzi tu Ndugai na Charamila unajua kilichowapata Wakati wanatoa maoni yao.
tatzo la marais wetu hawapendi kukosolewa ila magufuli alzd alikuwa yuko tyr kukuuwa kuliko kumwambia ukweli mwisho wa siku ujanja mwingi mbele gza yuko wap sasa hv japo hata ss tu nyuma
 
Wewe nilijua toka zamani sana kuwa ni mpuuzi..., , lakini naona matatizo yako yamezidi kadri unavyoendelea kuzeeka na kuchanganyikiwa kiakili.
Wajinga wanapokosa la kujibu hutoa matusi; nimekuwapo hapa JF siku nyingi sana kuelewa majibu ya watu wa namna hiyo.
 
Huyu babu ni ushahidi wa jinsi ambavyo demands za mwanamke zinaweza kuharibu akili ya mtu..
Lile jimama limempumbaza huyu babu mazima.
Akili yake inazidi kuwa mbovu kadri uzee unavyoongezeka..
 
tatzo la marais wetu hawapendi kukosolewa ila magufuli alzd alikuwa yuko tyr kukuuwa kuliko kumwambia ukweli mwisho wa siku ujanja mwingi mbele gza yuko wap sasa hv japo hata ss tu nyuma
Magufuri kauwa wangapi waliokuwa wakimkosoa? maana wengi walikuwa wakimtukana na bado wapo,akina Masudi kipanya walikuwa wananchora kwenye magazeti,lakini bado wapo,acheni Mambo ya kwenye vijiweni zungunza hualisia,akuna rais ambaye hajawahi kuhuwa hapa Tanzania na hatakuwepo,hata Sasahivi kuna watu wanapotea na kufa.
 
Inawezekana na wewe ni mmoja wa wanaomanini kuwa sera ni yale matamko ya viongozi wanayofanya majukwaani na kwenye maandamano. Tamko la Mbowe kama Mbowe au kama mwenyekiti wa CHADEMA ni kitu kimoja na sera ya CHADEMA ni kitu kingine. Linaloongelewa hapa ni sera ya CHADEMA siyo matamko ya Mbowe.
@Kichuguu unatetea nini ?
 
Na wewe umeishiwa unaaza kuleta hadithi za kuhisi na wala hujui maana ya sera.

Sera ni ahadi ambayo mwanasiasa anawapa wapiga kura wake kuwa mkinichagua nitafanya mambo yapi. Sasa basi, leta mfano wa mwanasiasa aliyehutubia wananachi akitangaza hayo unayosema kama siyo maneno yako ya uchochoroni tu. Hisia za namna hii huenda ndizo zinafanya CHADEMA inakosa sera, kwani wanadhani kulaumu ndiyo sera; ni afadhali hata mzee Rungwe ana sera zinazjulikana.
Usinifundishe upimbi kaa nao huko huko ccm.Yaani wapinzani wateswe,wauwawe halafu wakae kimya eti wanachostahili kukisema ni sera!kweli shetani yupo!
 
Usinifundishe upimbi kaa nao huko huko ccm.Yaani wapinzani wateswe,wauwawe halafu wakae kimya eti wanachostahili kukisema ni sera!kweli shetani yupo!
Unaandika kwa hisia na matusi huku ukichanganya mambo yasiyohusika; mada iliyopo hapa ni hiyo post ya Dr Slaa inayozungumza sera za wapinzani safari hii. Mimi sikuianzisha! Inawezekana wewe umeikutia katikati na kujiunga bila kuelewa ni nini kinaongelewa.
 
@Kichuguu unatetea nini ?
Swali lako zuri kama kweli unahitaji jibu langu; nitakujibu

Sitetei wala silaumu chochote ila nimesoma hiyo post ya Dr. Slaa na kuielewa vizuri kuwa anachosema ni wazi wapinzani hawana sera. Kwenye uchaguzi wa 2020, sera ya Lissu ilikuwa ni kutangaza mabaya ya Magufuli, siyo kwamba yeye atafanya lipi jema. Kwa vile Magufuli hayupo tena, na mama anawafanyia wanayotaka, basi hawatakuwa na la kutangaza tena. In fact watu wa CHADEMA wanatakiwa wachukue post hiyo kwa uzito sana kuliko kuuliza motive ya Dr. Slaa. Ikumbukwe kuwa ushindi wa kisiasa unatokana na kura ambazo pia zinatokana na sera.

Mwaka 2010, Dr. Slaa akiwa CHADEMA aliweza sana kuivurumisha CCM kwa vile wakati huo walikuwa wanasimamia sera zilizokuwa zinaeleweka vizuri sana, hawakuwa wanasimaia personalities. Alipoondoka, CHADEMA ikabaki ya personalities mpaka leo, na nadhani hilo ndilo analoonya. Mwaka 2015 sera yao ilikuwa ni kumtangaza Lowassa, na mwaka 2020 sera yao ikwa ni kumpinga Magufuli. Inaoekana sasa hivi sera imekaa kama vile ni Mbowe kubambikiwa kesi, halafu mama akamtoa; jambo linalowaweka kwenye njia panda kupambana na mama kwa personalities.

Kuna maeneo mengi ya sera ambayo CCM haijafanikiwa au imeyafanya vibaya, ambayo CHADEMA ingekuwa makini ingeyatumia vizuri kisiasa, lakini hawafanyi hivyo, badala yake wantumia muda mwingi kwenye mambo trivial tu.

Mfano mzuri sana ni uchaguzi wa 2020 ambao CHADEMA wanadai waliibiwa bila kutoa ushahidi wowote, kwani kuna utaratibu wa kimahakama kupinga wizi wa kura, lakini hakuna aliyewahi kutumia utaratibu huo. Iwapo CHADEMA ingekubali kuwa Magufuli na CCM yake kweli wamefanya mambo kadhaa mazuri,kama kusimamia utendaji wa serikali na vile vile wameanza kueneza huduma kadha vijijini. Hata hivyo utekelezaji wao umekuwa ni mbovu sana kwa sababu kadha kadha, na hiyo inatokana na uongozi mbovu wa Magufuli, hivyo CHADEMA itafanya mambo yanyofanana na hayo ila kwa ufanishi zaidi. Watu wengi wengeweza kuwaelewa, lakini wao sera yao ilikuwa ni moja tu "Magufuli, Magufuli" bila sera yoyote ya bread and butter. Mwisho wake wakaingia kwenye ule mtego wa CCM kuwa wapinzani ni wapingaji tu hawana lolote. Dr Slaa amewaonya, wakionyeka na kugeuza dira, wanaweza kufanikiwa wasipoonyeka na kuwa wa kufuata mtu, basi itapita miaka 30 mingine wakiwa upinzani tu.

Sijui kama umeelewa jibu langu vizuri
 
Wajinga wanapokosa la kujibu hutoa matusi; nimekuwapo hapa JF siku nyingi sana kuelewa majibu ya watu wa namna hiyo.
Kuwepo kwako hapa JF kwa muda mrefu hakujakusaidia chochote. Mabandiko yako ni yale yale ya kipuuzi tu siku zote! Rekodi hiyo nayo ni ya kujivunia?

Miaka yote hiyo umekuwa hapa JF, lakini michango yako ni ya kijinga kabisa, kama kule kung'ang'ania kwamba ule uwanja wa ndege Chato ndio ule ule uliokuwa umepangwa kujengwa Geita! Huu ni mfano mmoja tu wa mambo ya kipuuzi unayojaza humu kila unapojitokeza.
 
no mzuri sana ni uchaguzi wa 2020 ambao CHADEMA wanadai waliibiwa bila kutoa ushahidi wowote, kwani kuna utaratibu wa kimahakama kupinga wizi wa kura, lakini hakuna aliyewahi kutumia utaratibu huo
Hebu angalia, mtu mwenye akili timamu, kweli anaweza kutumia mfano wa kilichotokea 2020 kama mfano wa "uchaguzi", na kuujengea hoja?
 
Sasa hivi CHADEMA hawana sera tena baada ya punching bag wao magufuli kufariki.

Kabla ya magufuli sera za CHADEMA zilikuwa ni pamoja na kutoa elimu na huduma za afya bure, kuimarisha miundo mbinu ikiwa ni pamoja na ufufuaji wa relai na shirika la ndege.

Magufuli alipoyakamia hayo mambo kwa vitendo, CHADEMA wakamchukia kwa kuwanyangnaya sera, mara ya kwanza walisema "Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA." Baadaye wakashindwa kuvumilia kumwona anatifua kwa haraka vile wakageuka na kudai kuwa miradi hiyo ni "maendeleo ya vitu. Hiyo midege yatatusaidia nini!" Kosa la Magufuli pale alipouzia mikutano ya siasa basi wakapata kete kubwa ambayo mpaka leo bado wanaikumbuka, ambayo mama sasa kaifuta.

Slaa anasema kuwa upinzania hawana sera tena, yuko sahihi.

Nadhani wewe ulisoma ile post kwa kuangalia neno la "Magufuli aliwapa wapinzani hoja" ikakukera kwa vile ulitegemea aseme kuwa "Magufuli aliwanyima wapinzani demokrasi."
kwani chadema wapo si mlisema ishakufa ?
 
Hebu angalia, mtu mwenye akili timamu, kweli anaweza kutumia mfano wa kilichotokea 2020 kama mfano wa "uchaguzi", na kuujengea hoja?
Sawa; kama haukuwa ucahhguzi basi tusubiri uchaguzi halisi.Sasa hivi kuna Bunge na serikali iliyotokana na uchaguzi huo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom