Anataka kumroga hadi kumuua aliyeachana naye

Habari za Eid pili, bila kuchelewa niingie moja kwa moja kwenye jambo lenyewe, nina rafiki yangu ambaye nilisoma naye Tabora TC (2011) baada ya kumaliza hatukuwahi kuonana tena kwani yeye yupo Dodoma mimi Tanga lakini tuna mawasiliano ya mara kwa mara, juzi kanipigia simu ananiambia alifanikiwa kumpata binti na akaoa wakawa wanaishi pamoja na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ghafra mkewe akabadilika ghafra na hataki tena kuendelea naye na ameondoka yuko kwa dada yake Babati jamaa anasema hadi sasa kesharudishiwa na mahari kabisa na kinachomuumiza zaidi hadi anishirikishe ni kwamba wamemkata pesa kibao wakidai za mtoto na mkwe anamtusi na kumtishia atakujwa kuchukua vitu wagawane wakati binti kaondoka mwenyewe, kibaya zaidi binti ana jamaa na anamrusha fb ili kumuumiza mshkaji wangu hasira zaidi kwa msela wangu ni kwamba alichukua kamkopo sasa maisha kidogo yanakuwa havy na anapata wakati mgumu akikumbuka baadhi ya pesa alitumia kumsomesha mkewe hadi akamaliza nursing, sasa ameamua liwalo na liwe kaniambia anataka kuja kwangu nimpeleke pangani madanga kuna mzee makata ni shida sana akamalize kabisa biashara bora wakose wote maba akimuona hajisikii vizuri, bado sijamjibu natafakari sijui nimwambieje kuua siyo mchezo wakuu, nipeni mawazo nimshauri.
Mara ngapi tumesema mke hasomemshwi?alilmsomesha wa nini?aachane naye atafute maisha mengine,nyie wagogo na wanyamwezi mna matatizo sana.
 
DAWA YAKE NI KUMSAMEHE TU HUYO MWANAMKE KWA CHOCHOTE ATAKACHOFANYA,

KINYUME NA HAPO NI KUJITENGENEZEA MJUKUU MAJUTO
 
Haina haja ya kumroga, amuombe tu Mungu amuondolee machungu na amfanyie wepesi kwenye mambo yake. Wema aliomtendea kisha kulipwa mabaya tayari bibie ashajiroga mwenyewe wala asihangaike.

Ashukuru maybe kaepushwa na balaa zito zaidi huko mbeleni.
Kisasi sio kizuri maana malipo yake huwa makubwa zaidi. Kuliko aishi maisha yake yote akujilaumu kwa kuua, ni bora aache tu.

Hilo nalo litapita.
 
Naamini kama atamkabidhi Mungu hilo jaribu naamini atalishinda kwa mganga hakuna suluhisho la matatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom