Anahitajika Gynaecologists mzuri Jijini Dar

Dynamics

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2024
Posts
249
Reaction score
352
Habari ya asubuhi wadau.

Tafadhali nahitaji msaada wa kufahamu wapi ninapoweza kupata Daktari bingwa mzuri wa magonjwa ya wanawake (Gynaecologists) , either ana hospitali binafsi , Polyclinic au anahudumu katika hospitali binafsi au serikali. Nikipata Jina au hata mawasiliano yake nitashukuru sana.

Natanguliza shukrani

UPDATE.

Habari wadau, nashukuru kwa maoni na michango yenu, hatimaye kisa changu kimepata suluhu, baada ya kupima mimba kwa Rapid test imeonekana matokeo kuwa POSITIVE. Japo ataenda hospitali kuthibitisha rasmi.
20260814_083754.jpg
 
Habari ya asubuhi wadau.

Tafadhali nahitaji msaada wa kufahamu wapi ninapoweza kupata Daktari bingwa mzuri wa magonjwa ya wanawake (Gynaecologists) , either ana hospitali binafsi , Polyclinic au anahudumu katika hospitali binafsi au serikali. Nikipata Jina au hata mawasiliano yake nitashukuru sana.

Natanguliza shukrani
Una shida gani kwani?
 
Dr.Colman,Muhimbili!
 
Uhitaji wa Gynaecologist mzuri anayeweza kumsaidia mtu mwenye changamoto ya hormonal imbalance, kuanzia kwenye kumsikiliza vizuri mgonjwa na kujua shida yake haswa, vipimo mpaka kutafsiri majibu na kutoa matibabu sahihi.
Umejuaje ana tatizo la hormonal imbalance?

Na kama kweli ana shida ya hormonal imbalance ,mbona hilo tatizo dogo sana hata daktari wa kawaida tu anatibu sio lazima kuonana na daktari bingwa.
 
Kipindi cha nyuma amewahi kwenda hospitali na kuelezwa kuwa na hiyo hali baada ya siku zake za hedhi kuvurugika , lakini hilo tatizo halijawahi kufuatiliwa kwa undani kwa maana ya kuonana na wataalamu husika pamoja na vipimo
 
Aanzie kwenye hospitali za kawaida, kukiwa na haja ya referral watampa.
 
Fix hormonal imbalance kwa kufanya ketogenic diet,mama hata kama utafanya hormonal therapy lakini bado unakula hovyo tatizo halitaisha.
 
Back
Top Bottom