Anachokifanya Rais Magufuli si sawa

Anachokifanya Rais Magufuli si sawa

ndio hizohizo zinakamilisha zile 4 Tr za CAG
Ukimsema leta pia suluhisho. Usibaki kulaumu tu wakati suluhisho hutoi. Mnataka apeleke bungeni idhini ya milioni 5 hii si sawa. Hivyo ni vijisenti tu
 
Unaonaje Rais awe anagawa pesa yeye mwenyewe kwenye miradi ya maendeleo na bunge liache kuidhinisha hizo pesa maana zinapotea tu?
Ni kweli fedha anagawa yeye lakini hafuati bajeti iliyoidhinishwa na bunge!!
 
Hizo zilizopangia huko nyingi zinaliwa tu na hakuna kinachofanyika......afadhali hata hizo anazosaidia hadharani zinajenga na haziliwi.
Green devil are always blind
 
Ukimsema leta pia suluhisho. Usibaki kulaumu tu wakati suluhisho hutoi. Mnataka apeleke bungeni idhini ya milioni 5 hii si sawa. Hivyo ni vijisenti tu
Suluhisho lipo wazi kama umesoma bandiko lote utaona nimesema kwamba kero anazozitatua mh. Rais zimesababishwa na yeye mwenyewe kwa kutotumia vizuri pesa za umma kulingana na taratibu na sheria tulizojiwekea juu ya matumizi ya pesa za umma.

Suluhisho ndio hilo mh. Rais afuate sheria juu ya matumiz ya pesa za umma.
 
Anazogawa hadharani ndio rahisi zaidi kuliwa kuliko bajeti za wizara maana anagawa pasipo sttong written record na hakuna chombo rasmi cha kuhoji na kufuatilia matumizi yake.
Hizo zilizopangia huko nyingi zinaliwa tu na hakuna kinachofanyika......afadhali hata hizo anazosaidia hadharani zinajenga na haziliwi.
 
Ukimsema leta pia suluhisho. Usibaki kulaumu tu wakati suluhisho hutoi. Mnataka apeleke bungeni idhini ya milioni 5 hii si sawa. Hivyo ni vijisenti tu

Haha😁😁😁😁 wewe utakuwa mama leproffesori Tibaijuka!!!!
 
Bajeti kuwepo ni jambo moja, kupewa pesa kutekeleza hiyo bajeti ni jambo lengine.
Kwani jeshi la polisi halina bajeti ya stationaries?

Kama ipo, hiyo pesa imeenda wapi?
Kama haitoshi na bunge linapitisha hiyo bajeti nani wa kulaumiwa kati ya raisi, wizara na wabunge?
 
Ni kweli fedha anagawa yeye lakini hafuati bajeti iliyoidhinishwa na bunge!!

Nashauri Bunge lisiwwepo kabisa,maana pesa hupotea Sana kwa kuendesha Bunge afu Bunge kwa kipindi cha Mr stone ni useless kabisa!

Haliisimamii serikali,likitunga Sheria ni kwa maelekezo toka juu,likiidhnisha bajeti haifuatwi!

Bunge halijakosa Meno Tu Bali hata miguu ila Lina tumbooo kuubwa!
 
Kuna ile asante mh raisi umefanya hivi....
 
Kama ana Fedha mbona analialia na kishindwa kuwapa watumishi stahiki zao! Nadhani anatafuta sympathy tu kwa watu wa mitaani kua anajali
 
Suluhisho lipo wazi kama umesoma bandiko lote utaona nimesema kwamba kero anazozitatua mh. Rais zimesababishwa na yeye mwenyewe kwa kutotumia vizuri pesa za umma kulingana na taratibu na sheria tulizojiwekea juu ya matumizi ya pesa za umma.

Suluhisho ndio hilo mh. Rais afuate sheria juu ya matumiz ya pesa za umma.

Hataki mivutano wakati wanyonge wake wanaumia
 
Wakuu nawasalim.

Nimefuatilia ziara za Rais alizozifanya katika mikoa mbali mbali na hata hii ziara yake anayoifanya Mbeya.

Rais akitembea na pesa nyingi sana tena cash kwa ajili ya kugawa njiani baada ya kuelezwa na wanachi kero mbali mbali.

Mathalani Rais akisikia kero ya kutomaliziwa ujenzi wa madarasa , choo cha shule au Zahanati basi haraka sana hutoa pesa taslim milioni kadhaa.

Wakati Rais akitembea na cash kubwa ushahidi upo kwamba wizara kadhaa zimekuwa hazipewi pesa kulingana na bajeti zake zilizowasilisha bungeni ili kuweza kutatua changamoto mbali mbali za zinazogusa wizara husika.

Kero ambazo Mh. Rais anataka tuone akizitatua na hivyo kujijenga yeye binafsi na kujizolea umaarufu ni kero ambazo anazisababisha yeye mwenyewe kwa namna anavyotumia vibaya pesa za umma.

Wizara zina ukata ilihali yeye anatumia mapesa mengi kwa utashi wake binafsi kujenga au kununua vitu visivyokatika plans za wizara yoyote ile na wala pesa hizo hazijaidhinishwa na bunge matumizi yake.

Nasema hii si sawa na anachokifanya mh. Rais ni political entrepreneurship kwa maslahi yake binafsi. Kwamba tuone kwamba Mawaziri hawana msaada na ni bogus ilihali yeye ndio kikwazo.

NAWASILISHA.
Unahisi amekwisha gawa billion ngapi kwa mkoa wa mbeya peke yake?
 
Labda hufuatilii mirejesho ya bajeti zilizopita.. Kwa taarifa tu, bajeti iliyopitishwa na bunge kwa mwaka 2017/2018, pesa zilizolewa hazikuzidi nusu bajeti iliopitishwa.. That means, kama Wizara ya mambo ya ndani iliomba bilioni 500, basi pesa iliyotolewa haikuzidi bilioni 250.. Kwa hiyo shida haiko kwa bunge, shida iko huko Hazina, ambapo pesa zinapotakiwa zitoke..
LIPENI KODI SIYO KULALAMIKA
 
Back
Top Bottom