Anachokifanya Rais Magufuli si sawa

Anachokifanya Rais Magufuli si sawa

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,587
Reaction score
14,356
Wakuu nawasalim.

Nimefuatilia ziara za Rais alizozifanya katika mikoa mbali mbali na hata hii ziara yake anayoifanya Mbeya.

Rais akitembea na pesa nyingi sana tena cash kwa ajili ya kugawa njiani baada ya kuelezwa na wanachi kero mbali mbali.

Mathalani Rais akisikia kero ya kutomaliziwa ujenzi wa madarasa , choo cha shule au Zahanati basi haraka sana hutoa pesa taslim milioni kadhaa.

Wakati Rais akitembea na cash kubwa ushahidi upo kwamba wizara kadhaa zimekuwa hazipewi pesa kulingana na bajeti zake zilizowasilisha bungeni ili kuweza kutatua changamoto mbali mbali za zinazogusa wizara husika.

Kero ambazo Mh. Rais anataka tuone akizitatua na hivyo kujijenga yeye binafsi na kujizolea umaarufu ni kero ambazo anazisababisha yeye mwenyewe kwa namna anavyotumia vibaya pesa za umma.

Wizara zina ukata ilihali yeye anatumia mapesa mengi kwa utashi wake binafsi kujenga au kununua vitu visivyokatika plans za wizara yoyote ile na wala pesa hizo hazijaidhinishwa na bunge matumizi yake.

Nasema hii si sawa na anachokifanya mh. Rais ni political entrepreneurship kwa maslahi yake binafsi. Kwamba tuone kwamba Mawaziri hawana msaada na ni bogus ilihali yeye ndio kikwazo.

NAWASILISHA.
 
Ukimsema leta pia suluhisho. Usibaki kulaumu tu wakati suluhisho hutoi. Mnataka apeleke bungeni idhini ya milioni 5 hii si sawa. Hivyo ni vijisenti tu

Vituo vya polisi hata karatasi tu za dhamana, za kuchukua maelezo nk hawana unaambia katoe kopi stationary hizo zinazogawa zingesaidia kununua rim ngapi,ili kuepusha aibu
 
Vituo vya polisi hata karatasi tu za dhamana, za kuchukua maelezo nk hawana unaambia katoe kopi stationary hizo zinazogawa zingesaidia kununua rim ngapi,ili kuepusha aibu
Kwani jeshi la polisi halina bajeti ya stationaries?

Kama ipo, hiyo pesa imeenda wapi?
Kama haitoshi na bunge linapitisha hiyo bajeti nani wa kulaumiwa kati ya raisi, wizara na wabunge?
 
Suluhisho ni yeye kufuata katiba ya nchi.
Kama anatoa zake sawa ila kama ni za serikali sio sawa. Matumizi ya pesa huidhinishwa na bunge.
Ndo maana CAG hakuruhusiwa kukagua ununuzi wa ndege
Hizo zilizopangia huko nyingi zinaliwa tu na hakuna kinachofanyika......afadhali hata hizo anazosaidia hadharani zinajenga na haziliwi.
Ukimsema leta pia suluhisho. Usibaki kulaumu tu wakati suluhisho hutoi. Mnataka apeleke bungeni idhini ya milioni 5 hii si sawa. Hivyo ni vijisenti tu
 
Kwani jeshi la polisi halina bajeti ya stationaries?

Kama ipo, hiyo pesa imeenda wapi?
Kama haitoshi na bunge linapitisha hiyo bajeti nani wa kulaumiwa kati ya raisi, wizara na wabunge?
Unaonaje Rais awe anagawa pesa yeye mwenyewe kwenye miradi ya maendeleo na bunge liache kuidhinisha hizo pesa maana zinapotea tu?
 
Hebu tusaidie kidogo mkuu,piga hesabu tangu aanze ziara kule Mbeya kashagawa kiasi gani....
 
Kwani jeshi la polisi halina bajeti ya stationaries?

Kama ipo, hiyo pesa imeenda wapi?
Kama haitoshi na bunge linapitisha hiyo bajeti nani wa kulaumiwa kati ya raisi, wizara na wabunge?
Labda hufuatilii mirejesho ya bajeti zilizopita.. Kwa taarifa tu, bajeti iliyopitishwa na bunge kwa mwaka 2017/2018, pesa zilizolewa hazikuzidi nusu bajeti iliopitishwa.. That means, kama Wizara ya mambo ya ndani iliomba bilioni 500, basi pesa iliyotolewa haikuzidi bilioni 250.. Kwa hiyo shida haiko kwa bunge, shida iko huko Hazina, ambapo pesa zinapotakiwa zitoke..
 
Kwa hiyo akiwa na za kwake nazo apeleke wizalani?
 
Labda hufuatilii mirejesho ya bajeti zilizopita.. Kwa taarifa tu, bajeti iliyopitishwa na bunge kwa mwaka 2017/2018, pesa zilizolewa hazikuzidi nusu bajeti iliopitishwa.. That means, kama Wizara ya mambo ya ndani iliomba bilioni 500, basi pesa iliyotolewa haikuzidi bilioni 250.. Kwa hiyo shida haiko kwa bunge, shida iko huko Hazina, ambapo pesa zinapotakiwa zitoke..
Nakubaliana nawe kuhusu kutotekeleza bajeti kwa asilimia kubwa.

Turudi ktk swali langu la msingi kwanini wabunge wanapitisha bajeti ya wizara husika?

Bunge kwa maana ya wabunge wana wajibu wa kuiwajibisha serikali ktk utekelezaji na uwajibikaji ktk mambo yanayo pitishwa na wabunge au yaliyopo kisheria.

Wabunge hasa wa CCM hawajitambui au hawajui majukumu na wajibu wao kwa wanao wawakilisha.
 
Sasa hapo ndo tunaporudi kwa Bwana CAG.. aliposema bunge dhaifu alimaanisha pamoja na hili.. Bunge linaweza kuhoji kwanini bajeti waliopitisha, haikutekelezwa.. Mbaya zaidi ni pale pesa zinapobadilishwa matumizi na Raisi wakati tayar bunge wameshapitisha.. Wabunge wa sisiemu hao..
 
Kwani jeshi la polisi halina bajeti ya stationaries?

Kama ipo, hiyo pesa imeenda wapi?
Kama haitoshi na bunge linapitisha hiyo bajeti nani wa kulaumiwa kati ya raisi, wizara na wabunge?
Pumbavu! Unaambiwa wizara hazipewi fedha! Huelewi nini hapo? Anatembea na fedha za umma mfukoni kama zake binafsi!!

Shithole!
 
Back
Top Bottom