Anachokifanya Rais Magufuli si sawa

Anachokifanya Rais Magufuli si sawa

Waliokupa thanks nafikiri wana mtindio wa ubongo. Nilifikiri Rais wa mwisho kutembea akigawa pesa alikuwa ni Dikteta Gaddafi, kumbe bado kuna Marais wengine katika ukanda huu wa Afrika, kusini mwa jangwa la sahara wanagawa pesa kama karanga!!!!?

Hatembei na jiko hivyo wakimlilia njaa wataka akawapikie?? Usitutishe na maneno. Hataacha kuonesha pendo lake kwa walala hoi
 
sasa hizo kelele za ufisadi zinatoka wapi? au mawaziri wa chadema ndiyo wanaofisadi nchi?
Wasaidizi wake wengi ni njaa tupu hivyo anaona agawe mwenyewe ziwafikie moja kwa moja walengwa. Yaani, hana imani nao tena. Anangojea uchaguzi aunde wana miavuli wa kweli. Yaani mpaka mtaipenda hii nchi
 
Wasaidizi wake wengi ni njaa tupu hivyo anaona agawe mwenyewe ziwafikie moja kwa moja walengwa. Yaani, hana imani nao tena. Anangojea uchaguzi aunde wana miavuli wa kweli. Yaani mpaka mtaipenda hii nchi
hadi Ndugai kiongozi wa bunge ni njaa?
 
Ukimsema leta pia suluhisho. Usibaki kulaumu tu wakati suluhisho hutoi. Mnataka apeleke bungeni idhini ya milioni 5 hii si sawa. Hivyo ni vijisenti tu
Hivyo visenti vijumlishe kote aliko pitautapata sh ngapi ???

Halafu mwazo wa hesabu ya hela Ni sh. Ngapi huvi CCM mmelogwa na Nani ???
 
Hadi Magu atoke madarakani kama kweli atatoka nchi itakuwa ya kusikitisha sana.
 
Sio sawa kwani hakuna sehemu yeyote kwenye Katiba isemayo Rais atakuwa na pesa taslim kila afanyapo ziara ili kuweza kuchangia miradi iliyokwama kutokana na ufinyu wa bajeti. Hii ni kuidhalilisha Serikali yake anayoiongoza mwenyewe. Lkn kwa upande mwingine hatuwezi kushangaa kwani amekuwa akitamani kila nafasi.
 
Nakubaliana nawe kuhusu kutotekeleza bajeti kwa asilimia kubwa.

Turudi ktk swali langu la msingi kwanini wabunge wanapitisha bajeti ya wizara husika?

Bunge kwa maana ya wabunge wana wajibu wa kuiwajibisha serikali ktk utekelezaji na uwajibikaji ktk mambo yanayo pitishwa na wabunge au yaliyopo kisheria.

Wabunge hasa wa CCM hawajitambui au hawajui majukumu na wajibu wao kwa wanao wawakilisha.
Huo ndio ukweli. Hata ukifuatilia hoja hoja mbali mbali za baadhi ya wabunge kweli ni aibu kwa anao wawakilisha!!!
 
Mheshiwa hivi uliwahi kusikia kuwa mshambuliaji ndie hutendewa faulo na penati kuwekwa ila pia ndie mfungaji mzuri ndie mara nyingi kama sio zote hiicheza ile penati. Kwahiyo kusema matatizo anayasabisha mh. Vizur umetumia haki yako ya kikatiba sasa basi kwa kujua hilo ndio maana anazicheza hizo penati. Mungu tu atusaidie kwa kweli. Ingawa binafsi hizo pesa nazilinganisha na baba kwenye familia anapoamua kuja na pipi kwa watoto wake. Sio kwamba chakula ndani hakuna na majukum mengine ya kifamilia anatekeleza hizi pipi ni kama kuongeza upendo tu kwa watoto wake. Tumuombe sana Mungu viongozi wetu wamjue Mungu ili tawala zao zipate maelekezo toka kwake kesi itakuwa imeisha.
 
Wakuu nawasalim.

Nimefuatilia ziara za Rais alizozifanya katika mikoa mbali mbali na hata hii ziara yake anayoifanya Mbeya.

Rais akitembea na pesa nyingi sana tena cash kwa ajili ya kugawa njiani baada ya kuelezwa na wanachi kero mbali mbali.

Mathalani Rais akisikia kero ya kutomaliziwa ujenzi wa madarasa , choo cha shule au Zahanati basi haraka sana hutoa pesa taslim milioni kadhaa.

Wakati Rais akitembea na cash kubwa ushahidi upo kwamba wizara kadhaa zimekuwa hazipewi pesa kulingana na bajeti zake zilizowasilisha bungeni ili kuweza kutatua changamoto mbali mbali za zinazogusa wizara husika.

Kero ambazo Mh. Rais anataka tuone akizitatua na hivyo kujijenga yeye binafsi na kujizolea umaarufu ni kero ambazo anazisababisha yeye mwenyewe kwa namna anavyotumia vibaya pesa za umma.

Wizara zina ukata ilihali yeye anatumia mapesa mengi kwa utashi wake binafsi kujenga au kununua vitu visivyokatika plans za wizara yoyote ile na wala pesa hizo hazijaidhinishwa na bunge matumizi yake.

Nasema hii si sawa na anachokifanya mh. Rais ni political entrepreneurship kwa maslahi yake binafsi. Kwamba tuone kwamba Mawaziri hawana msaada na ni bogus ilihali yeye ndio kikwazo.

NAWASILISHA.
Kwani anabeba milioni ngapi? Ungetusaidia kama ungefuatilia na kuja na hesabu katoa hela kiasi gani kwenye mojawapo ya ziara zake. Kwangu mimi ni muhimu kama upo mpango kuhakikisha hela anazotoa zinatumika kwa shughuli zilizokusudiwa. Kila mahali tumeona ametoa hela kwa jambo la msingi. Angekua anatolea watu michango ya harusi au kufanya sherehe ndio tungesema hapana.
Inavyoonekana hela anayotoa sio hela nyingi kibaje na bila shaka imepangwa na ofisi yake kama matumizi halali.
 
Okay hadithi imefikia mwisho, nini tulichojifunza ?? Je hadithi yake imekuwa nzuri ??
 
Back
Top Bottom