Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 229
- 250
Anaandika Mo Mlimwengu
Uzalendo ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitolea kwa ajili ya nchi yake. Mwandishi na mwanafalsafa mmoja wa kifaransa ajulikanaye kama François-Marie Aroue(Voltaire) anasema anasikitika kuona mtu ambaye ni mzalendo anakua na maadui wengi.Kati ya jambo kubwa ambalo inabidi kumshukuru Rais wetu ni kutupatia Mh Dr Mwigulu kuwa mtendaji mkuu wa serikali.
Mapenzi ya Mwigulu kwa nchi yake hayana kipimo. Tanzania iko ndani ya moyo wake ndio maana popote pale anapokuwa lazima awe na nembo ya taifa lake ambayo ni Tanzania. Hii inaonyesha dhahiri shayiri kwamba huyu mtu ni mzalendo kweli kweli. Usipomkuta kavaa tisheti ya Tanzania, utamkuta kavaa skafu ya Tanzania na akivaa suti lazima tai yake itakuwa na bendera ya Tanzania. Hii ni ishara kubwa ya kuonyesha namna anavyouishi uzalendo.
Uchapakazi wake hautiliwi mashaka,tangu amekuwa mbunge ni mtu ambaye marais wa awamu zote waliweza kumteua kwenye nafasi za uwaziri. Siyo kwamba anapendelewa bali uchapakazi wake ndio umemfanya kuwa hivyo. Wizara zote ambazo alizipitia aliacha mchango chanya. Kama ni mchezaji wa mpira basi wewe mpe mpira utapata magoli.Uchapakazi wake ameuthibitisha zaidi kwa nafasi ya Uwaziri Mkuu. Ziara ambazo amekuwa akifanya kila mkoa na kila wilaya zimeleta matunda. Kwa sasa kila mkoa unatamani aje ili atatue kero ambazo zilikuwa sugu kwa wananchi.
Mwigulu ni mtu mwenye utu wa hali ya juu, hapendi kuona mwanadamu ananyanyasika, anatamani kuona kila mtu anaitufurahia nchi yake.Ndio maana huwa anaonekana mara zote akiguswa na changamoto za watanzania na anahakikisha zinaweza kutatulika kwa uharaka zaidi.
Uadilifu wake hautiliwi mashaka, ni nafasi nyingi ambazo amezitumikia kama kiongozi lakini hajawahi kupata doa la kuhusika na ufisadi wa aina yeyote. Ni muaminifu na uadilifu wa hali ya juu kwenye kusimamia rasilimali za nchi. Anapohubiri uadilifu kwa watanzania na wafanyakazi ni kitu ambacho yeye binafsi anakiishi.
Ubunifu kwenye uongozi, kiongozi mzuri ni yule ambaye anaweza kutumia njia mbalimbali ambazo zitarahisisha kwenye utatuzi wa changamoto. Hilo kwake amekuwa akiliishi na ndio inasababisha kupata matokeo chanya kwenye mambo tofauti tofauti. Atatumia njia shirikishi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuweza kutatua jambo husika.
Kufanya maamuzi sahihi, kulingana na ujuzi wake na uzoefu kwenye kufanya kazi kwenye sekta mbalimbali inapelekea kumuona akifanya maamuzi ambayo yanakuwa sahihi kwenye kutatua changamoto za watanzania. Hii inakuwa kete kubwa kwa Rais wetu kumpata mtu ambaye ni mfuatiliaji na anayehakikisha utekelezaji unafanyika kwenye sekta tofauti tofauti.
Waziri Mkuu Dr Mwigulu Lameck Nchemba ameonyesha uzalendo wa hali ya juu kwenye utendaji wake wa kazi, na hii inasaidia watendaji wengi lazima watabadilika ili kwenda na kasi yake. Amekuwa akisema mara nyingi kwamba watu wavivu, wazembe, wabadhilifu wa mali za umma kwenye hii awamu hawatakiwi. Inabidi waachie madaraka waje watu wengine ambao ni waadilifu.
Uthubutu wake, utendaji wake umejenga imani kubwa kwa watanzania. Tunaona ile falsafa ya kazi na utu ikitafsiriwa kwa vitendo.
#mwigulumzalendo
#kazinautu
#tanzaniayetu.