Anachokifanya Rais Magufuli si sawa

Anachokifanya Rais Magufuli si sawa

Wakuu nawasalim.

Nimefuatilia ziara za Rais alizozifanya katika mikoa mbali mbali na hata hii ziara yake anayoifanya Mbeya.

Rais akitembea na pesa nyingi sana tena cash kwa ajili ya kugawa njiani baada ya kuelezwa na wanachi kero mbali mbali.

Mathalani Rais akisikia kero ya kutomaliziwa ujenzi wa madarasa , choo cha shule au Zahanati basi haraka sana hutoa pesa taslim milioni kadhaa.

Wakati Rais akitembea na cash kubwa ushahidi upo kwamba wizara kadhaa zimekuwa hazipewi pesa kulingana na bajeti zake zilizowasilisha bungeni ili kuweza kutatua changamoto mbali mbali za zinazogusa wizara husika.

Kero ambazo Mh. Rais anataka tuone akizitatua na hivyo kujijenga yeye binafsi na kujizolea umaarufu ni kero ambazo anazisababisha yeye mwenyewe kwa namna anavyotumia vibaya pesa za umma.

Wizara zina ukata ilihali yeye anatumia mapesa mengi kwa utashi wake binafsi kujenga au kununua vitu visivyokatika plans za wizara yoyote ile na wala pesa hizo hazijaidhinishwa na bunge matumizi yake.

Nasema hii si sawa na anachokifanya mh. Rais ni political entrepreneurship kwa maslahi yake binafsi. Kwamba tuone kwamba Mawaziri hawana msaada na ni bogus ilihali yeye ndio kikwazo.

NAWASILISHA.
Bado miaka 6
 
Ukisikia uzumbukuku ndiyo huu wa kwako!

Kumbe hata hilo fungu lake (vote 20) linapitishwa na bunge?!

Shithole!!
Tatizo lako ni ufahamu(comprehension). Yaani kusoma na kuelewa kilicho andikwa.

Ndio maana unakimbilia matusi na misemo ya taarabu.

Sijisumbui kukufafanulia nilikusudia nini ktk jibu langu. Sababu ni kazi bure kwa uelewa wako wa mambo.

Endelea na mitusi na taarabu.
 
Sasa hapo ndo tunaporudi kwa Bwana CAG.. aliposema bunge dhaifu alimaanisha pamoja na hili.. Bunge linaweza kuhoji kwanini bajeti waliopitisha, haikutekelezwa.. Mbaya zaidi ni pale pesa zinapobadilishwa matumizi na Raisi wakati tayar bunge wameshapitisha.. Wabunge wa sisiemu hao..
Definitely bunge ni dhaifu tena dhaifu sanaa.
 
Bunge lipi la kuiwajibisha Serikali? Hili Bunge ambalo ni Bunge DHAIFU kama alivyosema CAG Assad!? Huyo kichaa yangu aingie madarakani anachota trillions bila idhini ya Bunge na Bunge LIKO KIMYAAAA!

Wabunge wa upinzani ambao wanajaribu kuiwajibisha serikali wananyimwa nafasi ya kuzungumza Bungeni pia kubambikiwa kesi FAKE na hata kufukuzwa bungeni.

Wabunge machachari wa ccm wanaambiwa hawakupikwa vizuri ina maana wale waliopikwa wanatumbua macho tu bungeni na kumuachia dikteta afanye vile apendavyo.
Bunge dhaifu sana.
Ukisema udhaifu wao tatizo wanamuogopa raisi, hivyo raisi ndio tatizo tutakuwa tunakosea.

Tunakosea sababu bunge linaweza kumuondoa raisi kikatiba kama wanaona anakosea jambo. Kumbe wabunge wana nguvu kuliko raisi.

Tatizo hapa sio raisi bali wabunge wanao ogopa waki mwajibisha raisi atavunja bunge na wanaweza wasirudi tena bungeni. Hapo utaona wabunge wapo kwa maslahi ya kulinda mkate wao na familia zao wala sio wawakilishi kamili wa wananchi.

Tanzania tuna wabunge dhaifu na bunge dhaifu mno kwa mtazamo wangu kulingana na maelezo ya CAG, Lema na Mdee. Pia kwa kuangalia baadhi ya mambo wanayopitisha bungeni kisha baada ya muda mfupi inaonekana dhairi walikosea inabidi yarudi bungeni kujadiliwa au kubadilishwa kama sheria ya takwimu na sakata la fao la kujitoa ktk mifuko ya jamii.

Nashikia msimamo wangu raisi sio tatizo bali bunge na wabunge wake ndio tatizo.
 
Kwani jeshi la polisi halina bajeti ya stationaries?

Kama ipo, hiyo pesa imeenda wapi?
Kama haitoshi na bunge linapitisha hiyo bajeti nani wa kulaumiwa kati ya raisi, wizara na wabunge?

Si huko tu ofisi nyingi hali mbaya kujiendesha,mkuu wa malaika kutoa zikalete tija udhani zinapigwa.
 
Huo ndiyo ukweli Bunge ni DHAIFU kutokana na kumuogopa huyo dikteta mwizi fisadi muongo na muuaji. Mbunge yeyote wa ccm anayeikosoa Serikali bungeni huonekana ni mkorofi husemwa hadharani na kutishiwa forms zake kutosainiwa na dikteta ili asirudi bungeni. Nape alifanya kosa lipi hadi kufutwaUwaziri? Bashite pamoja na madudu chungunzima hajafutwa kazi. Huhitaji Phd ili kuelewa hili

Bunge dhaifu sana.
Ukisema udhaifu wao tatizo wanamuogopa raisi, hivyo raisi ndio tatizo tutakuwa tunakosea.

Tunakosea sababu bunge linaweza kumuondoa raisi kikatiba kama wanaona anakosea jambo. Kumbe wabunge wana nguvu kuliko raisi.

Tatizo hapa sio raisi bali wabunge wanao ogopa waki mwajibisha raisi atavunja bunge na wanaweza wasirudi tena bungeni. Hapo utaona wabunge wapo kwa maslahi ya kulinda mkate wao na familia zao wala sio wawakilishi kamili wa wananchi.

Tanzania tuna wabunge dhaifu na bunge dhaifu mno kwa mtazamo wangu kulingana na maelezo ya CAG, Lema na Mdee. Pia kwa kuangalia baadhi ya mambo wanayopitisha bungeni kisha baada ya muda mfupi inaonekana dhairi walikosea inabidi yarudi bungeni kujadiliwa au kubadilishwa kama sheria ya takwimu na sakata la fao la kujitoa ktk mifuko ya jamii.

Nashikia msimamo wangu raisi sio tatizo bali bunge na wabunge wake ndio tatizo.
 
Anazogawa hadharani ndio rahisi zaidi kuliwa kuliko bajeti za wizara maana anagawa pasipo sttong written record na hakuna chombo rasmi cha kuhoji na kufuatilia matumizi yake.
Alizokugawia hadharani nenda kazile ndiyo utajua kilichomnyoa kanga manyoya shingoni....
 
Those Are The Characteristics Of A Living Dictator.
A Dictator, Respect Not The Rules.
But He Is The Rules To Be Respected.
Unanikumbusha moja aliyeitwa Dr., Al Haj. President Idi Amin Dada. Alikuwa anatembea mifuko yake ikiwa imetuna kwa kujaa pesa taslimu za Uganda. Alikuwa na mazoea ya kuzigawa mara kwa wajane, mara kwa waathirika wa matukio mbali mbali tofauti.

Rais wetu Dr., Mkuu wa Malaika na Rais John Pombe Magufuli anafuata tu nyayo za madikteta wengine wa Kiafrika. Huona fahari sana kutembea na pesa za walipa kodi mfukoni na kuzigawa kama njugu bila kufuata taratibu!

Tatizo la hawa madikteta ni kwamba kwa uelewa wao mdogo hawajifunzi. Idi Amin alikuwa jirani yetu na tuliona na kushuhudia alivyoikimbia Uganda. Kwa kuwa hakuna nchi ya Kiafrika ilithubutu kumpa hifadhi...alikimbilia Uarabuni!

Yangu macho!
 
Bajeti ijayo hakuna haja ya Wabunge kukaa na kupoteza muda wa kugawa pesa za serikali katika wizara na taasisi zake hapa nchini kwetu Uzuvendi.
Wamwachie tu mfalme wetu wa Uzuvendi azipeleke anapoona yeye panafaa.
Maana sasa hivi oc haziendi ziliko elekezwa wala pesa za miradi.
Badala yake zinachukuliwa na kusambazwa na yeye mbinafsi anakotaka ziende.
Tena kwa nguvu na c.a.g.hatakiwi kuzikagua, mfano haieleweki nani alinunua mndege kwale na ni kwa shilingi ngapi.

Eeeh Mungu Utuhurumie, ni janga gani hili tunalolipitia.
 
Hakika hakika.
 
akija kiongozi mwingine naye akatumia mfumo huo huo msianze kulalamika
Hatuta lalamika kama huyo ajaye atakuwa katokea ccm kwa sababu viongozi wa ccm wameelimika na wanatenda kwa staha na uadilifu sana. Umewahi kuwaona wakiwa kwenye mikutano yeyote?? Ni watu wastaarabu sana
 
sasa hizo kelele za ufisadi zinatoka wapi? au mawaziri wa chadema ndiyo wanaofisadi nchi?
 
Ukimsema leta pia suluhisho. Usibaki kulaumu tu wakati suluhisho hutoi. Mnataka apeleke bungeni idhini ya milioni 5 hii si sawa. Hivyo ni vijisenti tu
Waliokupa thanks nafikiri wana mtindio wa ubongo. Nilifikiri Rais wa mwisho kutembea akigawa pesa alikuwa ni Dikteta Gaddafi, kumbe bado kuna Marais wengine katika ukanda huu wa Afrika, kusini mwa jangwa la sahara wanagawa pesa kama karanga!!!!?
 
Inashangaza sana
 
Back
Top Bottom