Wana jamii wenzangu mimi ni mwanaume wa miaka 29 nimekuwa na uhusiano na msichana kwa miaka 3 mwishoni mwa mwaka niligundua kuwa ana uhusiano na mtu mwingine na nilipombana kwa maswali alikubali na kusema wamekuwa pamoja kwa miezi 8 ila wameachana wiki mbili zilizopita nimeumia sana maaana nilimwamini mno, nimeamua kuachana nae ila nilimpa laptop yangu ya gharama sana ya laki 9 kwa makubaliano nitamnunulia ya kwake ila baaada ya usaliti aliofanya nimeona anipe mali yangu .Cha ajabu anang'ang'ania kwa kusema anaitumia na kwa sasa hawezi kunipa,kipekee sipendi fujo nafikiria kutumia nguvu ila naona ni utoto na naweza kusababisha matatizo.Naombeni ushauri nifanyeje?