Jumanne naenda kumuangalia rafiki yangu jela nini vya kuzingatia?

Wamamba

Senior Member
Jan 5, 2024
125
231
Heshima kwenu wakuu

Nimembebea pesa ya kutosha ya kumpa mwamba,

Sipo Tanzania, umri 26-30 (code) sababu ya hali yangu mbaya ya kiuchumi nimejikuta nipo nje ya taifa langu pendwa lenye amani na upendo TANZANIA sijilaumu naamini katika kujifunza na kukomaa katika utafutaji, kuongeza ujuzi mbali mbali na uzoefu katika kuvuka boda najua ipo siku nitakaa pahala pazuri nakujipongeza jitihada zangu za utafutaji, sifanyi magendo ya aina yeyote na naishi kuzingatia sheria za nchi kuanzia vibali na kila kitu kwa mujibu la taifa hili nilipo ila binafsi naona bora nyumbani, wajuzi wa mambo wanakwambia bora hamsini nzima kuliko mia mbovu au bora ugali maharage kwenye amani kuliko wali nazi na mikuku kuku kwenye vita, ila sijutii naamini kwenye mwanaume kula kwa jasho. Mtanambia niongeze nyama hapo kama kuna kitu kimepungua najaribu kuficha wanaonijua sanaa washindwe kuleta umbea maana hakuna kitu ninachokichukia kama umbea umbea

KUHUSU RAFIKI YANGU

Ana 23- 28, ana kesi ya kulawiti mtoto mdago , sijui kama ni kweli au amesingiziwa, huku ugenini tulipokuwepo kama hawakukubali wanakupa kesi ya ubakaji na kwa hiyo kesi kutoka ni maajaliwa aisee, amekaa jela mwaka na nusu sasa kesi inarushwa tu, mtaani tunatoka mtaa mmoja ila sina na ukaribu naye toka nyumbani, kinachonipeleka kumuona ni wote ni watanzania tu basi maana hata hatujawahi kuelewana hata alivyokuwa uraiani alikuwaga mtu wa kunipinga sanaa yaani namaanisha hakuwa ananikubali kabsa by the way sijui kwanini? Labda mimi ndio nilikuwa tatizo, mwisho wa siku niliona bora niwe mbali naye maana niligundua tutakuja kugombana bila sababu - hapo kwa huku ugenini

Kitanzania tanzania yaani tulipokuwa nyumbani sikuwa na tabia ya kukaa na vijana wa umri wake yaani na vijana umri kama wake kwani ni mdogo kwangu , nilikuwa nakaa na watu walionizidi umri na pia na niliyokuwa nao umri sawa , nikikaa na dogo kumzidi ilikuwa anakuja kuniomba ushahuri wa kimawazo au wa kumsaidia kwa kipesa kama atakuwa anahitaji lakini kwa yeye hatujawahi kuwa Karibu hata kidogo nadhani ndio maana hatukuwa na muunganiko hata huku ugenini? Cha ajabu ni kutoniheshimu kabsa ndicho kilichokuwa kinanishangaza

Kilichonichelewesha kwenda kumuona ni nilisafiri kurudi nyumbani baada ya miaka 5 ya mkimbizane ya hapa ughaibuni, ila yeye aliwahi kuja huku kabla yangu lakini hakuwahi kurudi nyumbani, binafs akili ilichoka ikanibidi nirudi nyumbani na kiuhalisia sikuwa na pesa ya kutosha lakini niliona bora nirudi nyumbani kwanza maana kuna mda unabidi uisikilize akili yako inakwambia nini?

Sijui kuhusu baba yake ila mama yake namfahamu, lawama nyingi kwa mama yake kuwa vipi? rafiki yenu mbona hajali kuhusu mimi mama yake na alikuwa anaomba niende nimwambie kuwa mama yako anakukumbusha kuwa hana kitu hali mbaya ila binafs sikuweza kwenda kumwambia maana nilijua itakuwa vita Coz jamaa hatakagi kunisikiliza kabsa yaani nilikuwa namwambia tu mama yake ajaribu kumpigia na kumuelekeza, hapo ilikuwa kabla ajaenda jela wala mimi sijarudigi Tanzania

Binafsi nilikuwa najiumiza sanaa kuhusu kuwazingatia nyumbani coz nilivyosafiri niliacha nyumbani hali tete sanaa na nilikuwa najitahidi kutuma pesa nyumbani na kwa maelekezo na kwa sheria kali ya matumizi ya hiyo pesa ila nashukuru niliporudi nyumbani nilikuta kama nilivyotarajia

Maana nilikuwa nawatumia pesa wanunue vifaa vya ujenzi pia na pesa ya fundi na walikuwa wanaendelea na ujenzi kila ninapobahatika kutuma pesa, niliwapongeza sanaa na hawajaniangusha japo kuwa walikuwa wanajenga kwao wao wenyewe, ila niliumia sanaa na kama nisingekuwa nawajali hata kwa udogo ulee ningekuwa na hata kiupande hata cha vyumba vinne huko chanika ila niliona sina sababu ya kuwa na kwangu wakati wazazi wangu hawana pahala pazuri pakuishi na ni watu wazima, waliushukuru sanaa wazee niliporudi ila nilikuwa nawaambia nastahili kuwafanyia hivi so hamna haja ya kunishukuru yaani nilikuwa naona haya watu wazima kama wazee wangu kunishukuru

KUHUSU RAFIKI YANGU
Uraiani ameacha mchumba na mtoto yaani alivyokuwa kabla hajaenda jela alikuwa na kasichana kanakaribia kujifungua na huyo msichana alimkuta na mtoto(2) kabla ya kumpa ujauzito, so now mtoto wao ana mika 1.5 huyo mtoto wake jamaa aliyekuwa jela, jamaa ni mbishi karibia jamii wa watanzania wote walikuwa wanamkataa maana alikuwa asikilizi mtu aisee hataki ushahuri kwa yeyote huku ugenini ana miaka 7, binafsi nimefunga zipu kwa huku na hawa wanawake/wasichana- watanzania wana tabia ya kupokezana na magonjwa mengi huku na mimi ni muoga sanaa wa kesi za hapa na palee naona bora nikaushe , nna njia maalum ya kuvumilia kutokufanya tendo ila ni ngumu sanaa maana kuna watoto wazuri hatari ila nashinda hii hali, vurugu niliporudi nyumbani mbona wakina mwajua walinijua mi nani’ jokes

Alishawahi kuwa na uhusiano na msichana fulani wakubwa wakanambia niende kumshahuri kuwa huyo msichana anaweza kuwa na virus vya ukimwi binafsi sikuenda niliwaambia wakubwa kuwa “ukitaka uishi vizuri na mtu usiingilie uhuru wake “ walinielewa

Jamaa alishawahi kudhurumu ofice ya watu na jamaa aliye mdhurumu alihaidi kumroga na alimroga Kweli na jamaa alipataga matatizo makubwa, kiufupi jamaa aliachiwa ofice na jamaa aliyemwachia alirudi Tanzania baada ya mda rafiki yangu akasema ofice ni yake so ikapelekea mwenye ofice akamdhuru, mwenye ofice ni mtu wa kigoma, baada ya kupona ndio alikaa mwaka mmoja ndio akapata kesi na kwenda jela

Msione kama nampondea ila jamaa ni kiburi na umri wake hafananii kabsa yaani ameshawahi kumtukana mbongo/mkubwa ambaye anasimamia matatizo ya watu wote hapa kitongojini, simkashifu ila hauwezi kukaa nayeye maana hata brother wake aligombana naye ,brother wake ambaye aliyemleta huku ughaibuni

Wakubwa walijaribu kwenda kumuomba aliyefungua kesi ili wampe pesa akafute kesi ila alikataa katu katu,
Wakubwa wanapitisha michango , mwanasheria anataka pesa ya kutosha ili jamaa atoke

Kibaharia NIMEMSAMEHE mwamba ila najiweka nayeye mbali kadri nnavyoweza maana nilijaribu kurudisha mawasiliano yetu alivyoumwa nilimpa sapoti sana kwa hali na mali ila alivyopona nilitofautiana naye tena so ntaenda kumtizama jela na kumpa salamu za kwao na akitoka sitazoeana nayeye.
 
Usimpe hela kinyemela/kwa kificho huwa ni kosa kubwa sanaaaaaa.Uliza wenyeji then watakuelekeza vitu vya kwenda navyo halali.Msaidie kwa kufikisha taarifa ubalozini ili atoke arudi Tanzania.

Mimi nipo Tandahimba nalima maisha yanaenda
 
Unaandika mambo mengi mtu anashindwa hata kuelewa unataka kusema nini
Stream of consciousness kupita rap za Wu-Tang Clan.

Unafunguliwa bomba full blast mpaka unashindwa kunywa maji.

Mtu anakwambia anataka kwenda kumuona baharia jela, halafu anamponda saana, halafu anamalizia kusema anataka kujiweka naye mbali.

Sasa kama anataka kujiweka naye mbali, kwa nini anataka kwenda kumuangalia jela?

Contradiction. Cognitive dissonance.
 
Daah.leo kuna kabinti kadogo kalikuwa kanauza moyai.kakaja nilipokuwa nimekaa.
Akaniambia "waoooo anko nauza mayai"
Haki ya mungu mwili ulinisisimka.
Nikasema ukisikia mtihani ndo huu.
Kakaniambia anko ninunulie mayai.nikasema tobaa. Majaribu haya.
Kukwepa mitego nikanunua moja tukamegeana nikamzuga na maswali ya unakaa wapi,unasoma wapi.
SHETANI AKAPITA.
 
Unaenda kumwona au kumchora tu? Afu mbona kama wewe ndo unalazimisha urafiki na huyo mwamba.

Tatizo analia lia na analaumu na anataja na majina watu ambao anatufahamu, disgn alizokuwa ananilete nisingeenda ila naenda tu kwa kuwa anataka apakazie watu lawama wakati anayataka na hayawezi
 
Una mambo ya kike, ushamba na umwinyi labda ndio maana jamaa anakukataa.

Kiuhalisia siwezi kumchekea mtu ambaye anafanya nikose raha ya maisha hata kwa kuzuga

Na kinachofanya niende ni anatangaza kuwa watoto wa mtaani tumemkataa naenda na ntamchana ukweli na ataenjoy hiyo situation
 
Back
Top Bottom