Amegundua Mchumba anatembea na Mchungaji

Gwesefe

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
680
377
Jamaa yangu amenieleza jambo nimeshindwa kumjibu chochote nisije nikakosea kumshauri akanilaumu hapo baadae.

Iko hivi, huyu bwana ana mahusiano na msichana wake takribani miezi sita sasa. Anasema anampenda sana huyo msichana na msichana anampenda jamaa sana kiasi kwamba ameshawishika ikiwezekane aje kuwa mke.

Katika mahusiano yao amekuwa akimdodosa kujua kama huyo msichana ameshakuwa na mchumba kabla au mwanaume mwingine kabla yake kwa hapa Dar, msichana kasema hajawahi kuwa na mwanaume toka afike Dar mwaka wa pili sasa, akamuuliza kwanini akasema kwasababu aliamua kuokaka na anasali kanisa moja la kilokole maeneo ya kinyerezi-kifuru japo jamaa hajawahi kufika hapo kanisani. Jamaa akafurahi sana kwamba hapa nimepata mke sahihi.

Lakini baadae akawa anamtilia mashaka kwamba mbona anaonesha kuwa ana mawasiliano ya siri sana na mtu asiyemjua, alipo kuja kumbana haswa na kumtishia kumuacha akakiri kuwa alikuwa akitembea na Mchungaji wake ila aliona hatia moyoni mwake kutembea na mchungaji akaamua kumuacha japo mchungaji anaendelea kusumbua.

Akamuuliza ulianza nae lini na umemuacha lini ili ajue wanawasiliana kama mpenzi au kama mtumishi wake tu maana wanawasiliana mara kwa mara na mchungaji wake mpaka usiku maana binti anaimba kwaya na anahusika hapo kanisani kwa shughuli zingine za kanisa.

Anasema akadai kwamba amekuwa nae toka akiwa mkoani miaka miwili iliyopita huyo mchungaji ana kanisa huko mkoani nae alikuwa anasali hapo. Pia amefungua lingine huku Dar, Binti yeye alitangulia kuja dar kwa shughuli zake za kutafuta maisha ndipo mchungaji alihamia Dar akafungua kanisa nakuwatafuta watu wake aliokuwa nao mkoani ili waendeleze kanisa ndo akamtafuta na yeye.

Pia akadai kuwa mchungaji amekuwa akimlazimisha tu kufanya hivyo japo yeye hapendi na amefanya nae kama mara tano tu nyumbani kwake maana mtumishi anaishi mwenyewe familia yake yaani mke na watoto amewaacha mkoani huwa anaenda na kurudi, kwa utetezi wake akadai mara ya mwisho wamefanya na mchungaji kama miezi mitatu iliyopita baada ya ibada ofisini kwake kwasababu alimlazimisha tu akashindwa kukataa. Ila sasa ameamua kumuacha huyo mchungaji rasmi na kuwa na jamaa, japo mshikaji majuzi kaona meseji ya mchungaji kwa binti akimwambia nakupenda sana ila binti hajajibu lolote.

Anaomba ushauri aendelee na mipango yake maana hivi karibuni mwezi wa saba alitaka kwenda kujitambulisha au asikilizie kwanza kwa miezi kadhaa kama kweli ameachana na mchungaji wake, au amteme tu, japo anadai anampenda sana huyo binti na binti ameomba asimuache bali amsaidie ili aweze kutoka kwenye hiyo hali maana na yeye haipendi Pia binti anasema kuokoka ameanzia hapo kwa huyo mchungaji wakati wakiwa mkoani, kwahiyo mchungaji amekuwa kama mlezi wake kwa muda mrefu kama miaka minne sasa.

Je atafanikiwa kuachana na huyo mchungaji.?

Ushauri wenu tafadhali.
 
Jamaa yangu amenieleza jambo nimeshindwa kumjibu chochote nisije nikakosea kumshauri akanilaumu hapo baadae.

Iko hivi, huyu bwana ana mahusiano na msichana wake takribani miezi sita sasa. Anasema anampenda sana huyo msichana na msichana anampenda jamaa sana kiasi kwamba ameshawishika ikiwezekane aje kuwa mke...
Amakamatishe
 
Ukweli usiosemwa ni kwamba wake za watu wengi wanamegwa na wachungaji. Tena kiulaini mno.

Ila Kuna kosa ndugu yako kalifanya,

Si sahihi kumuuliza mwanamke wako huko alikotoka ametembea na wanaume wangapi. Akikuambia ukweli Kuna uwezekano mkubwa wa kuanza kumchukulia tofauti na hasa kumchukulia Malaya wakati Ni wewe mwenyewe ulitaka kujua.

Na wanawake ogopeni Sana kujibu Hili swali la mtego. Hili swali halina afya kwa mustakabali wa mahisiano yenu. Tatizo mnapenda kujibu hili swali kwa kigezo Cha "nampenda wacha nimwambie ukweli".
 
Mchungaji mwenyewe sasa!
20220923_000146.jpg
 
Huyo jamaa yako au Kama ni wewe mwenyewe umekuja kwa mgongo wa nyuma,ningekuwa Mimi nisingetoa ushauri wowote.

Mambo ya Mapenzi ya watu ukijifanya baba ushauri unakuja kuonekana snitchi na mchawi wakati wepenzi wawli waliogombana wakipatana.

Wapenzi waliogombana wakipatana huwa wanapiga Sana umbea wa kuwateta watu waliosuruhisha ugomvi,wale waliokuwa wanakaza muachane au umuache moenzi wako huwa mnasimangwa na kutukanwa Sana kitandani.

Maneno yangu ni mafupi tu Kama Smart911 . Mambo yao waachie wenyewe.
 
Jamaa yangu amenieleza jambo nimeshindwa kumjibu chochote nisije nikakosea kumshauri akanilaumu hapo baadae.

Iko hivi, huyu bwana ana mahusiano na msichana wake takribani miezi sita sasa. Anasema anampenda sana huyo msichana na msichana anampenda jamaa sana kiasi kwamba ameshawishika ikiwezekane aje kuwa mke...
Huyu jamaa yako ni mjinga na mpumbavu kwa 100%.
Jambo kama hilo halihitaji hata kutafakari mara mbili kwa mwanaume sembuse kuja kuomba ushauri hapa JF.

Kwa kifupi sana, hili ndio ninaloweza kumshauri. Aende sasa akapime Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa, na kama atakutwa hujaambukizwa chochote, baada ya miezi mitatu aende akarudie tena kupima.

Mengine kuhusu huyo mwanamke hayahitaji hata kujadili, muda huu ninaandika hapa ingepaswa huyo binti awe hospitalini akiwa anatibiwa majeraha mazito yaliyotokana na kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa huyo jamaa. Kifupi sana huyo hahitajiki tena kwenye maisha yake toka siku amegundua tu anapigwa miti na mchungaji wake. Binti ni malaya anayejiuza na mchungaji ni muhuni wa kawaida anayenunua malaya.
 
Watoto wa mjini hapo ndipo pa kupiga pesa na kumkomesha mchungaji.

Aende kanisani Jumapili, amtambulishe jamaa yake kwa Mchungaji kuwa huyu ndiye mtarajiwa wangu. Na jamaa naye amsalimie. Hapa tunatafuta justfication ya mchungaji kukosa namna ya kujitetea huko mbeleni.

Kisha, waondoke kwenda nyumbani. Kama mchungaji atadhubutu tena kumtafuta binti, hapo ndipo maangamizi hufanyika. Jamaa anamuingiza mchungaji kingi naye atajaa.

Siku binti anaenda kukutana na Mchungaji iwe kanisani au popote, jamaa anaunga tela. Anawafumania na kuwarekodi. Jamaa atamtishia mchungaji kutaka kumlala kondoo wake.

Vizuri awe na namba ya Mama Mchungaji. Anamtishia kufoward hizo video kwa Mama Mchungaji na kumthibitishia anamuonesha na namba zake.

Mchungaji toa Million 5 (aangalie na hali ya kanisa. Kama ni kubwa dau liwe kubwa, and vice versa) vinginevyo hili ni soo. Chukua hela alafu binti akome mara moja kwenda hapo.

Mpe jamaa ID yangu anitafute.
 
Huyo jamaa yako au Kama ni wewe mwenyewe umekuja kwa mgongo wa nyuma,ningekuwa Mimi nisingetoa ushauri wowote.

Mambo ya Mapenzi ya watu ukijifanya baba ushauri unakuja kuonekana snitchi na mchawi wakati wepenzi wawli waliogombana wakipatana. Wapenzi waliogombana wakipatana huwa wanapiga Sana umbea wa kuwateta watu waliosuruhisha ugomvi,wale waliokuwa wanakaza muachane au umuache moenzi wako huwa mnasimangwa na kutukanwa Sana kitandani.

Maneno yangu ni mafupi tu Kama Smart911 . Mambo yao waachie wenyewe.
Hakika...
 
Back
Top Bottom