HAPO Kagera ni wilaya zote kuanzia
Ngara,Muleba,biharamulo,Bk Rural and Urban na hata karagwe maaeno ya Nyakahanga,Mulushaka etc pote nilichafua.
Enzi nasaka Kahawa na ndizi nazisafirisha ki Magendo..
Nilikuwa sipendi ile pombe yao ya Ndizi.
Tukija Njombe Kule town maeneo ya kuazia Ramadhani,hagafilo,Chaugingi,Kibena,Uzunguni,Tanwat pote Nilikanyaga WAKATI tunasaka madalali wa mashamba ya mbao.
kule lupembe Na matembwe karibu na Shule ya manyunyu niliruka Sana na pipoz za Kule daah Enzi tunaenda lupembe kusaka maparachichi na kuyasafirisha nje.
Tumelangua Sana mpaka tukapata mashamba ya maparachichi kule.
Kufika maeneo ya makambako tulikuwa tunafanya udalali,na kuuza vitu coz makambako ilikuwa Ni centre ya wafanyabiashara karibu wa kusini.
Tukija Iringa daah.
Sitopasahau kule pagawa na maeneo ya mtandika lukosi,
maisha ya kulima vitunguu yalikuwa magumu na full ushirikina.
hapo Morogoro,Dar,Tanga na Pwani sisemi maana naendaga ZAIDI navyokwenda msalani.
Tour Ambayo Nili enjoy Ni ile niliyozunguka mikoa ya Kusini
Kule pesa Ngumu lakini people's za Kule bado hazijajanjaruka ilikuwa Ni full kuwalaghai.
mkoa wa Kigoma sikuupendelea Sana
coz ya wingi wa wakimbizi na muingiliano wa warundi,wacongo na waha
hahahaha utaomba pooo
Wewe mleta maada umezunguka mikoa less than 5 .Kati ya mikoa 30?!
bado SANAA
Kwa Sasa naisaka njia ya Tunduma kutokea Momba
Sent using
Jamii Forums mobile app